Orodha ya Vigogo Wazalendo watakaohutubia Mkutano wa hadhara Temeke

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
123,081
232,778
Screenshot_2023-07-21-11-53-16-1.jpg


Taarifa kutoka kwa Wazalendo wanaoandaa Mkutano wa hadhara utakaofanyika Temeke, ambao umelenga kuueleza umma wa Wananchi kuhusu Ubovu na makando kando ya Mkataba wa Bandari za Tanganyika na DP WORLD, Wametoa orodha ya vigogo watakaohudhuria na kutoa mada kwenye Mkutano huo kabambe.

Kiukweli tangu nirejee Tanzania kutoka US sijawahi kuona Mkutano uliounganisha watu wa dini , itikadi na Makundi tofauti kama huu , Hongereni sana mlioandaa jambo hili.

Habari zaidi zinadokeza kwamba wamo viongozi wastaafu, mawaziri na majaji wastaafu, wamo wanasiasa wa vyama vyote vyenye nguvu, wamo Mashehe , Manabii na Maaskofu, Mkutano huu umepangwa kuanza saa 3 asubuhi hadi machweo ili kuwapa nafasi kwa vigogo wote kuhutubia na kutoa nafasi kwa wananchi kutoa madukuduku yao.

Mungu ibariki Tanganyika.

View attachment 2696173
 
Kumbe mnachofurahia ni burudani ya kukusanya mnaowaita maarufu.

Basi endeleeni wakt serikali ikikaza buti kwenye jambo lake.
 
Back
Top Bottom