JokaKuu
Platinum Member
- Jul 31, 2006
- 30,441
- 55,018
..orodha ya wabunge wa bunge lililopota la EAC.Current Members: 2007-2012
....
By :
CCM's Publicity and Ideology Secretary, Nape Nnauye allayed members fears saying that matter had been discussed earlier, with reference to Uganda's case and that Tanzania is on the right track. Announcing the results of the election, Prime Minister Mizengo Pinda the following women from Zanzibar won; Septuu Nassor with 177 votes. Safia Ali Rijaal and Mariam Usi Yahaya won with 169 and 179 votes respectively.
By :
The men from Zanzibar who were declared winners included; Said Bilal, 197 votes. Abdallah Ali Mwinyi scooped 187 votes while Zuber Ali Maulid came through with 176 votes. Dr Haji Mwita Haji with 168 votes beat Amada Khatibu by one vote. Last but not least was Hamis Jabir Makame with 143 votes.
From the mainland Angela Kizigha topped the list with 160 votes was followed closely by Fancy Nkuhi, and Shyrose Bhanji with 147 1nd 145 votes respectively. Janeth Mmari won 133votes while Janet Mbene and Godberha Kinyondo almost came to a tie with 116 and 115 votes respectively.
For the men from mainland Adam Kimbisa garnered 196 votes. Dr Edmund Mndolwa came second with 159 votes. Siraju Kaboyonga with 153 votes, beat Bernard Mulunyaby ten votes. Even tighter was the four votes William Malecela had over Elibariki Kingu's 132 votes. Likewise Evance Rweikiza's 125 votes against Mrisho Gambo's 121. Charles Makongoro Nyerere came through with 113 votes.
All the contestants had to express themselves in English for three minutes each before the delegates and party leaders.
The endorsement of CCM's members Parliament came at a time when Uganda's Attorney General was at the EAC Secretariat in Arusha seeking court guidance and interpretation of how the Ugandan Parliament should elect members to represent the country at EALA
Baada ya kupima vigezo nilivyovieleza, hebu tuangalie hapo juu jinsi kura zilivyopigwa na hao ni wabunge wa CCM ambao ndio wengi bungeni, utaona kuna kila dalili matokeo yakafanana sana na hayo hapo juu na tofauti ikawa ndogo kulingana na karata za mwisho watakazocheza wagombea na zaidi maelezo ya mwisho mbele ya wabunge wote na hatari inaweza kuwakumba watakaoteleza katika kujibu maswali dakika za mwisho. Siasa za makundi ndani ya CCM nazo zinaweza kuwaumiza wagombea vijana kama hapatakuwa na umakini na Utaifa zaidi katika upigaji kura.
Ubunge wa Afrika masharaiki ni uwakiishi wa nchi katika jumuiya. Kwa mtazamo wangu Tunahitaji watu wa kusimamia masilahi ya nchi kuliko vyama. Ukifuatilia kuna agenda kwa baadhi ya wanachama kuhusu mweleko wa Jumuiya.
Tunahitaji watu wenye uweledi wa hali ya juu ambao peke yao wanaweza kusimama bila kutegemea hadidu rejea za serikali
Tunahitaji watu wanaoweza kusoma alama za nyakati, mwelekeo wa dunia na thamanai za taifa letu. Watu watakaoweza kujenga hoja na hoja zikasimama zenyewe. Hapa hatuhitaji majina bali wasifu wa mgombea ambaye si CCM, CDM n.k
Nakiri kuwa baadhi ya wagombea sijui sifa zao, lakini haitaniuzuia kutaja baadhi ya sifa za wagombea
Awali niseme sikubaliani na hoja ya 'young or energetic'. Tuzingantie uwezo kwanza. Nina mifano kila siku kuwa bunge la sasa lina vijana wengi, je wamefanya kitu gani tofauti na lile la zamani? Vijana wenyewe si akina Lusinde!!
Adam Kimbisa: Huyu amewahi kuwa Meya wa jiji la Dar es Salaam. Hakuna chochote anachoweza kutonyesha kuhusu uwezo wake wa kazi. Muda wake wote hali ya jiji imezidi kuwa mbaya. Meya asiyeweza kutafuta suluhu ya maji kujaa Pamba house hawezi kutusadia katika medani kubwa ya uwakilishi.
Twaha Issa Taslimu: Huyu ni mwanasheria aliyebobea. Mtazamo wake juu ya Tanzania ni mdogo kuliko Uzanzibar.
Sina hakika kama yupo kwa masilahi ya nchi au sehemu ya nchi
Dr Bilal: Huyu ni msomi anayeweza kujenga hoja. Hata kama ana mizigo mingine lakini kiwango chake cha ufahamu na uzooefu katika siasa za pande zote za nchi ni kitu muhimu sana.
Siraju Kabuyonga: Huyu alikuwa mbunge wa CCM, katika michango yake sijaona mahali alipowahi kusimama kidete kwa masilhai ya taifa zaidi ya majibu mazuri ya mh waziri..... Sidhani kama atatusaidia.
Shyrose Bhanji: Amegombea nafasi nyingi ndani ya chama chake na mara nyingi amebwagwa. Sifa yake kuu ni kutokata tamaa katika kulekea ndoto zake za kisiasa.Huenda analo jambo analotaka kulifanya kwa taifa bahati mbaya hajapata nafasi. Ana uzoefu kama afisa mahusiano na sijui hilo linawezaje kulisaidia taifa. Sijui uelewa wake wa mambo ya kitaifa ua kimataifa. Mahusiano yake binafsi na wana jamii yaliyowekwa wazi yanatia wasi wasi ingawaje kila mtu ana maisha binafsi.
C.Makongoro nyerere: Pamoja na kubebwa na jina kubwa la baba yake, uenyekiti wa chama mkoani Mara umempa nafasi nyingine ya kujidhihiri. Kwa sasa amekuwa mwiba mkali kwa chama chake hasa mafisadi. Ameonekana kusimamia utaifa zaidi kuliko chama. Swali ni je elimu yake inatosha kupambana na magwiji wa nchi jirani katika hoja?
W.Malecela( Le Baharia): Huyu kama makongoro anajina kubwa nyuma yake. Sina wasifu wake kwa undani hata hivyo.
Advantage aliyo nayo ni kuwa amejijenga kama yeye kwa kuchanganyika na makundi ya kijamii. Mwingiliano wake na jamii unamweka mahali pa kuwa mtu anayewasiliana na jamii. Pengine hilo pamoja na exposure yake vunaweza kuwa plus.
Tatizo lake ni pale uchama unapotangulia utaifa, na hapa tunahoji, je anaweza kusimamia thamani za taifa hata kama zinapingana na masilahi ya chama chake?
Ni mtazamo binafsi kwa uchache
Inasikitisha kuona mtu kama wewe unaleta siasa ati mama Janet Mbene na Mndolwa hawafai...Hebu angalia CV zao kwanza na si kupelekewa watu wasiojua chochote kuhusu economic blocks! Kama wakina Fancy Nkuhu na Shyrose Banji
Ahsante Mkuu. Makosa tunayafanya hapahapa kesho tunakuja kujilaumu na kuwalaumu wakenya. Kesho tunapeleka watu ambao hawajui chochote wanasaini miswada ya kutumaliza tunaanza kuwalaumu wenzetu waliopeleka watu makini. EAC inahusu zaidi mambo ya kiuchumi hivyo ni bora tukapeleka watu watakaotusaidia katika hilo na wala si wapiga tarumbeta. Kwamba mtu anajua.publicity basi anafaa, hee kwani EAC wanaenda kugawa madawati.
Sorry, hii thread ilikuwa inasumbua techinical, hivyo nimeihamishia hapa
https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...nge-wa-afrika-mashariki-washindi-ni-hawa.html
Sorry for any inconveniences caused!
Pascal.
Wanabodi,
Nimekuwepo mjini Dodoma kwa siku mbili tatu. This is my opinion kuhusu Uchaguzi wa nafasi ubunge wa Afrika Mashariki, wagombea gani wana chances zaidi za kushinda na sababu zao za kushinda zikiwemo strength na weaknesses za baadhi yao!.
1. WAGOMBEA WALIOTEULIWA
KUNDI A: WAGOMBEA WANAWAKE
S/ JINA CHAMA
1. Nd. Angela Charles Kizigha CCM
2. Nd. Fancy Haji Nkuhi CCM
3. Dkt. Godbertha Kokubanza Kinyondo CCM
4. Nd. Janet Deo Mmari CCM
5. Nd. Janet Zebedayo Mbene CCM
6. Nd. Maryam Ussi Yahya CCM
7. Nd. Rose Daudi Mwalusamba CUF
8. Nd. Sebtuu Mohamed Nassor CCM
9. Nd. Shy-Rose Sadruddin Bhanji CCM
10. Nd. Sofia Ali Rijaal CCM
My Opinion
Kundi hili wanatakiwa wawili (3). Mbunge bora wa kundi hili ni Fancy Nkuhi kwa sababu ya elimu bora na Shyrose Bhaji kwa sababu ni bingwa wa publicity hivyo kusaidia Watanzania kuifahamu vizuri hii jumuiya. Chances kubwa zimewalalia Janet Mmari na Janet Mbene simply because kuna wazito wanene wanawabeba!. Mmari alikuwepo amefanya nini kustahili kurejea?. Mbene aliteuliwa kuwa mbunge wa kuteuliwa siku chache kabla bunge lililopita halijamalizika, nani anajua sababu ni zipi?, hivyo atachaguliwa Eala kuzikamilisha!. Most unfortunate ni Dr.Godbetha ambaye ni msomi wa Ph.D kwa sababu she belongs to the elite class "mshomile"!
KUNDI B: WAGOMBEA WA ZANZIBAR
S/N JINA CHAMA
1. Nd. Abdullah Ali Hassan Mwinyi CCM
2. Dkt. Ahmada Hamad Khatib CCM
3. Dkt. Haji Mwita Haji CCM
4. Nd. Khamis Jabir Makame CCM
5. Dkt. Said Gharib Bilal CCM
6. Nd. Zubeir Ali Maulid CCM
My Opinion
Kundi hili anatakiwa wawili (2), Dr. Ahmada anasimama more chances na ndiye the best, ila kwa vile siasa za Zanzibar majina ya ubini yana matter sana, kama ilivyokuwa kwa Karume, hakuwa na lolote zaidi ya jina, hivyo naomba msishangae jina la Gharib Bilal ndilo litakapita!.
KUNDI C: WAGOMBEA WA VYAMA VYA UPINZANI
S/N JINA CHAMA
1. Nd. Antony Calist Komu CHADEMA
2. Dkt. Fortunatus Lwanyantika Masha UDP
4. Nd. Juju Martin Danda NCCR-MAGEUZI
5. Nd. Micah Elifuraha Mrindoko TLP
6. Nd. Mwaiseje S. Polisya NCCR-MAGEUZI
7. Nd. Nderakindo Perpetua Kessy NCCR- MAGEUZI
8. Nd. Twaha Issa Taslima CUF
My Opinion
Hapa anatakiwa mmoja (1) the best option ni Komu wa Chadema akifuatiwa na Dr. Fortunatus Masha ila atakayechaguliwa ni Taslima wa CUF kufuatia wabunge wengi ambao ni CCM kuwajibika kumchagua mgombea wa CUF ambaye ni mwana ndoa wao kwenye ile ndoa ya CCM na CUF!.
KUNDI D: WAGOMBEA WA TANZANIA BARA
S/N JINA CHAMA
1. Nd. Adam Omar Kimbisa CCM
2. Nd. Bernard Musomi Murunya CCM
3. Nd. Charles Makongoro Nyerere CCM
4. Dkt. Edmund Bernard Mndolwa CCM
5. Nd. Elibariki Immanuel Kingu CCM
6. Dkt. Evans Mujuni Rweikiza CCM
7. Nd. John Dunstan Lifa-Chipaka TADEA
8. Nd. Mrisho Mashaka Gambo CCM
9. Nd. Siraju Juma Kaboyonga CCM
10. Nd. William John Malecela CCM
My Opinion
Hapa zinatakiwa nafasi 3. The best options hapa ni William, Mrisho na Dr. Rweikiza (The young, vibrant and energetic). Watakao chaguliwa ni Kimbisa, Edmund Mndolwa for connections na Makongoro Nyerere kumuenzi tuu Baba wa Taifa!. (Inaonyesha kuna watu wamekuja na fungu la kufa mtu huwezi amini hata wale ambao huwezi amini kuwa wana vuta, wamevutishwa!).
Hitimisho
Haya ni maoni tuu, matokeo sio lazima yatokee hivi hivyo nawaombeni msinitolee mimacho kama nlivyomtabiria Sioi ushindi kule Arumeru halafu aliyeshinda ni Nasari. Na wewe unaruhusiwa na kutoa maoni yako nani unadhani anafaa zaidi na kwa sababu zipi?, kama kuna mtu unaona hafai au hakupaswa hata kuwepo miongoni mwa wagombea pia unaweza kumtaja na sababu.
NB. Naomba kusisitiza sana, tuwajadili kila mmoja based on the their own merit na sio kuwajadili kwa majina ya baba zao!, baba zao ni baba zao, na wao ni wao ndio maana wamesimama!.
Natanguliza Shukrani.
Pasco.
William,
1. hili suala la elimu ya wa-Tanzania unapendekeza lishughulikiwe namna gani? naomba ueleze exposure unayoizungumzia ktk muktadha wa elimu ya Mtanzania.
2.kuhusu suala la sarafu, kama hela yetu ni ya chini kuliko ya Kenya maana yake, theoretically, ni kwamba tunaweza kuuza bidhaa nyingi zaidi kwao, kuliko wao wanavyoweza kuuza kwetu. Kitu cha kushangaza ni kwamba mambo ni kinyume na hicho nilichokieleza hapo juu. Je, Tanzania itaweza vipi kubadili mazingira ambapo nchi yetu ni "dampo" la bidhaa za Kenya.
3.Suala la free movement. Kwanini tusifuate model ya NAFTA ambapo Mexicans hawaruhusiwi kuingia USA hovyo-hovyo bila kufuata taratibu za USA? Kwanini unafikiri EU[ulisema unaunga mkono free movement] model ni nzuri kwetu ukizingatia kwamba Tanzania hatuna mfumo wa utambulisho kama SSN na national ID??
4.Ni hatua gani unafikiri zinapaswa kuchukuliwa wakati tuna-slow down the process? wasiwasi wangu ni kwamba tunaweza kufika mahali tukaishiwa sababu na visingizio vya kusema twende polepole.
5.Kuhusu Non-Tariff Barriers[NTB] isiishie kwenye uzito wa magari ya mizigo tu. Kenya wanalazimisha mpaka wa Golongoja ufunguliwe ili waweze kuvusha watalii wao kuingia Serengeti bila Tanzania kupata chochote kile.
Mkuu Wiliam nimesema tupeleke watu watakaotusaidia katika mambo ya uchumi na sijasema tupeleke wasomi wa uchumi.Mtu anaweza kujua mambo ya uchumi kwa kufanya kazi katika mashirika mbalimbali yaani anakuwa na experiance ama hata exposure tu kwenye mambo hayo. Si lazoma uwe na PHD ya uchumi bali uelewa wa mambo hayo. Ukiamua kugombea nafasi yoyote ya kisias basi wewe ni mwanasiasa hivyo mambo ya political lobbying yanaanzia hapo. Hatutaki kupeleka watu ambao hawajui kiuchumi Tanzania tunataka nini ndani ya JUmuiya, Rwanda, Kenya nk wanataka nini. Ukiyajua hayo basi unaweza kujenga hoja ya kiasiasa na siyo kujenga hoja ya kisiasa bila kujua unaijenga kwenye misingi gani hasa ya kiuchumi.
Tuking'ang'ania siasa tutapigwa bao manake wenzetu watajenga hoja zilizoenda shule siye tunapeleka kiswahili mingi. Tutajikuta tunapwaya. Uchumi ni siasa.
pasco ningeulizwa na Mungu sasa hivi unataka nini ningemwambia, anionyeshe kwa cv za wanaochaguliwa kuwa wabunge wa hili bunge kutoka kwa wenzetu. pia anionyeshe commitment walizonazo katika kazi hii ndipo sasa ningerudi kuwadiscuss hawa wakwetu.
all in all tunahitaji watu ambao ni committed, na wenye exposure na well educated. pia watu wenye experience kwenye maswala ya kimataifa katika nyanja za uchumi, social, health na communication. lakini shy rose banji kwa kweli hafai kabisa hapa kwanza elimu yake haikumkomboa. manake kama hapa Jaffarai alimzingua hadi ikawa skendo akienda huko akina kidumu si ndo watampagawisha zaid??????????