Ondoeni Kinga ya kutoshtakiwa ndipo msaini hizo HGA na DP World

Mpinzire

JF-Expert Member
Jan 18, 2013
7,224
12,946
Serikali na Bunge imeonekana mna nia kabisa na ili dubwasha la DP World mliendeleze bila kujali wananchi wanasemaje!

Basi mimi nawaomba kwa dhati kabisa Rais Samia Suluhu uondoe kinga ya kutoshtakiwa kuanzia kwako mpaka kwa wasaidizi wako na spika wa bunge na Jaji Mkuu wote wawajibike.

Hata kama walishatoka madaraani kwa makosa yenu ambayo mlisababisha Taifa eidha kupata hasara au kupolwa chochote.

ilo tu.
 
Then mnaambiwa mumkumbuke nyerere. Kwa katiba hii ya kipumbavu ??
Mzee aliharibu sana nchi hii , hastahili hata kukumbukwa.
 
Then mnaambiwa mumkumbuke nyerere. Kwa katiba hii ya kipumbavu ??
Mzee aliharibu sana nchi hii , hastahili hata kukumbukwa.
We ni kichwa cha kuku hizo kinga zina kua amended na vichwa vya kuku enzenu uko bungeni .
 
Hata wakiondoa haitasaidia. Serikali Afrrica haziogopi wananchi kwa kuwa wananchi wanatatuliana shida zao. Hauna chakula unagongea kwa ndugu, hauna kazi unapata msaada kwa jirani.

Kwenye nchi ambazo Huna kazi huli, Huna pa kukaa serikali ziko makini sana. Hapo ndio tatizo lilipo.
 
Hapo tutaelewana.
Tunaona Trump anashitakiwa na serikali hadi ya Jimbo kwa madudu aliyofanya akiwa na madaraka.
 
Serikali na Bunge imeonekana mna nia kabisa na ili dubwasha la DP World mliendeleze bila kujali wananchi wanasemaje! basi mi nawaomba kwa dhati kabisa Mh Rais Samia Suluhu uondoe kinga ya kutoshtakiwa kuanzia kwako mpaka kwa wasaidizi wako na spika wa bunge na jaji mkuu wote wawajibike ata kama walishatoka madaraani kwa makosa yenu ambayo mlisababisha Taifa eidha kupata hasara au kupolwa chochote.

ilo tu.
Hapo ndio utaona Tulia Jackson rangi yake halisi. Mkataba ataubwaga chini😆😆
 
Ipo hivi, jinai haina expire date..wacha walipitishe tu hayo madudu yao
Siku katiba mpya ipo mjengoni wataisoma namba hata kama watakuwa watoto wao watatapika tu zote..
 
Watu watastaafu na kuandika vijitabu vyao kujibaraguza na kukiri walivurunda hapa na pale basi.

Hapo wamelitia hasara taifa billions kodi ambazo zinakusanywa kikatili na maafisa kutoka kwa watu masikini wa kutupwa.
 
Unaposema bila kujali wananchi wanasema nini unakuwa na maana gani? Yaani kisa DP world mbowe haitaki na misukule ya michache ndo umejumuisha wananchi wote? Asilimia 98 ya wananchi tumelidhishwa na DP world na tunaomba serikali isaini haraka HGA na DP world maendeleo yaanze kukimbizwa mbio mbio!!
 
Then mnaambiwa mumkumbuke nyerere. Kwa katiba hii ya kipumbavu ??
Mzee aliharibu sana nchi hii , hastahili hata kukumbukwa.
Nyerere alileta Katiba hii kulingana na mazingira ya wakati huo lakini hajazuia mabadiliko ya Katiba maana Katiba ni mali ya Wananchi na siyo mali ya Rais
 
Serikali na Bunge imeonekana mna nia kabisa na ili dubwasha la DP World mliendeleze bila kujali wananchi wanasemaje! basi mi nawaomba kwa dhati kabisa Mh Rais Samia Suluhu uondoe kinga ya kutoshtakiwa kuanzia kwako mpaka kwa wasaidizi wako na spika wa bunge na jaji mkuu wote wawajibike ata kama walishatoka madaraani kwa makosa yenu ambayo mlisababisha Taifa eidha kupata hasara au kupolwa chochote.

ilo tu.
Tuondoe kinga thubutu! Mje mtunyoe kwa chupa 🤣🤣🤣🤣
 
Hata wakishitakiwa unaona hio ni faida kwa taifa ? Mahakama zenyewe ndio hizi za mwenye pesa kupata utetezi kuliko vinginevyo....

Dawa ni kwamba makubaliano / mikataba yoyote ya kipuuzi isifanyike na ili tujue kama kuna upuuzi au hakuna mikataba hii iwe wazi (Full Transparency when it comes to Public Property)
 
Then mnaambiwa mumkumbuke nyerere. Kwa katiba hii ya kipumbavu ??
Mzee aliharibu sana nchi hii , hastahili hata kukumbukwa.
Wewe ndio unayemlaumu babu yako kwa sura yako mbaya sababu hakumchagua bibi mzuri zaidi...

Kwahio na hizo mali ambazo hawakuzifuja then wewe leo unazikuta na kuzifanyia udalali umewakumbuka kwa kiasi gani ?
 
Trump leo yupo jela
Released on bond, aliingia kwa backdoor, akakaa kwa dakika zisizofika 20 akishughulikia taratibu za bond akatokea front door akasepa.
Screenshot_20230825-170817_Chrome.jpg
 
Back
Top Bottom