On Channel 10: Mwigulu afunguka juu ya Uzalendo, Gesi Mtwara, Bomu Arusha...

Mbona wameweka kipindi cha Dr. Mwaka? Kwanini mnadanganya tumekaa tunasubiria bhana
 
Hizi media za Tanzania nazo ni sehemu ya tatizo tu.....huu unafiki na uovu kumpa muuaji kama Mwigulu jukwaa la kendeleza dhihaka dhidi ya Tanzania na raia wake.

I'm gutted to be Tanzanian. I'm ashamed to be Tanzanian.

usipende kuropoka una uhakika na unachokisema.
 
Mjulishe kwamba KAMPENI za uchaguzi zimeshafungwa na haziruhusiwi tena kwa uchaguzi wa madiwani Arusha.

Waambie Chanel Ten kwamba endepo wata mpa nafasi ya kuzungumzia uchaguzi Arusha wakati kampeni zimesha katazwa ni kinyume na sheria za uchaguzi. Hivyo nao watakuwa wamevunja sheria. Kwa maana kwamba upande utakao athirika na mazungumzo kwenye hicho kipindi una haki ya kuchukua hatua za kisheria.

Ni tahadhari tu. Maana kwa jinsi hali ilivyo, Mwigulu Nchemba anaonekana ndio Raisi wa JMT kwa wakati huu ambapo tuliye mchagua yupo busy na mikutano, kusafiri, na kupokea wageni.
Lets wait...tuone kama AMG imekuwa jukwaa la kampeni baada ya kufungwa muda wa kampeni
 
Kampeni arusha zimeisha,swali la tindikali lipo mahakamani,swala la bomu polisi wanafanya upelelezi,sasa haoni kwamba anavunja utaratibu..huyu goon wala hata siwezi kumsikiliza.

Maadamu ameamua kuongea nje ya bunge, wanaCDM wamsikilize ujinga wake ili kama ni kushitakiwa basi iwe ni hapohapo maana nje ya bunge hana kinga.
 
Hizi takataka sijui By Juliana Shonza na mwenzie ambaye alikuwa anapika uji huku kakata tamaa...CDM waliwapa nafasi wasizo stahili.....walikuwa bado kustaarabika vya kutosha kuweza realize "humanity" ktk CDM comunity.


Hawa ni laana ya nchi...si muda wasipotubu na kuwa watu wata regret maisha yao yote..wasipotubu.wataishia kuisema vibaya CDM hata wakiwa ktk gongo.

Hii type ya vijana huwa si muda hufulia hadi kuishia kwenye taputapu.
 
Ni rahisi sana kupanda mbegu za chuki; lakini, ni ngumu sana kuziondoa mbegu hizi kwenye jamii. Wakati umefika kwa Watanzania wote, wanaoitakia nchi hii mema, kupinga siasa zinazofanywa na Mwigulu Nchemba. Siasa hizi ni za muda mfupi na hazitusaidii kujenga nchi yetu. Nani anayempa uhuru wa kuingilia jambo linalochunguzwa na vyombo vya dola? Kama anajua ni chama cha siasa kilichousika na hilo bomu, jee ameshaisaidia Polisi?

Kama ingekuwa ndani ya CCM kunae watu watano tu wenye uwezo wa kufikiri kama wewe basi nchi hii tusingefika hapa tulipo leo.
Hakika wengine watafurahia anachokifanya Mwigulu lakini siku moja tutajutia hii nafasi tunayompa huyu CHIZI kuendelea kutugawa kwa Maslahi yake Kisiasa.
Mauaji ya kimbali huko Rwanda ilichangiwa kwa kiasi kikubwa na wanasiasa uchwara kama Mwigulu na Media kama tunavyoona sasa.

Waliokufa Arusha ni binadamu haijalishi ni wafuasi wa CDM au sio. Sasa Mwigulu kutaka kutumia marehemu kujinufaisha kisiasa kama anavyo fanya kwa kijana Musa Tesha alieathirika kisaikolojia baada ya kumwagiwa Tindikali ni jambo linalosikitisha na la Kumchukiza hata MUNGU.
Mwigulu kumbuka kwamba cheo ni dhamana.na kujidai wewe unajuwa kila kitu kwa kweki siku moja utajutia inachokifanya siku moja. Kumbuka hukujiumba bali kuna aliekuumba na kwamba siku yafika kwa huyo aliekuumba kusema sasa basi.

Mwisho wa UBAYA siku zote ni AIBU!!
 
[h=2]Hanipha Musri

icon1.png
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Gairo amwagiwa Tindikali[/h]
Mwenyekiti wa CCM Wilaya mpya ya Gairo Bwana Omary Awadhi, amemwagiwa tindikali usiku wa kuamkia leo nyumbani kwake Gairo. Kwa mujibu wa mwenyekiti huyo tukio hilo lilitokea usiku wa manane baada ya watu wasiojulikana kumgongea na kumwamsha.

Hata hivyo anasema aligoma kufungua mlango bali alifungua kioo cha dirisha la chumbani kwake. Watu hao walimuonya kutohudhuria kikao ambacho yeye ni mhusika alipokataa, ndipo ghafla akahisi kumwagiwa kitu usoni kilichomletea maumivu makali sana.

Aliwahi kunawa maji lakini hali bado ni tete.Muda huu yupo safarini anakimbizwa Dar kwa matibabu zaidi baada ya uso wake kuharibika.

GAIRO​

Hili litakuwa Capitalized kuliko hata bomu la Arusha. Just wait?
 
Anatakiwa kujua jinsi anavyoianadi ibaya CHADEMA ndivyo anavyoijenga.Sielewi kama wanaCCM wenzake wanalielewa hilo.Walianza na CUF ya waislamu,mara wameleta majambia ili kuanzisha vita,mara hawa ni waroho wa madaraka.Mwisho wa siku CUF ikafa leo yale yale yanajirudia,tatizo ni kuwa huwezi kudanganya watu wote wakati wote ,CCM inatakiwairudi nyuma ijiangalie kwa nini tupo hapa tulipo.
 
Cdm pressure inapanda pressure inashuka

Sent from my BlackBerry 9360 using JamiiForums
 
Back
Top Bottom