Okwi asaini Yanga

watani zangu masharubu acheni kupiga mayowe Asprin, kichenchele, stroke, Kakalende, Safari_ni_Safari, Abdulhalim na Kigogo ngoja wayaone wenyewe. Kombe la kuku jana mlitoka ngapi ngapi na lamba lamba Azam

Ngoja niwajibie, Jana tulitoa sare ya goli moja moja, na wewe naomba utusaidie kutafuta ukweli wa hili, inaeleweka kabisa Yanga hawana timu B, hawa mliowapeleka Zanzibar wakacheza mechi moja wakapigwa tatu na kesho kufukuzwa na uongozi wa ZFA mliwaokoteza wapi?
 
Na Jina la Timu Litabadilika Kabisa
Simba baada yatwaa ubingwa1-5.jpg

Mimi kama mdau wa yanga nakwambia sio kweli, ila huyu Okwi anataka sana kuja yanga kwa sababu yanga baada ya uchaguzi itakuwa kama TP Mazembe. Hata sisi tulikuwa tunamhitaji isipokuwa ana mkataba na Simba ambao unaisha december mwaka huu. kumsajili sasa hivi italeta matatizo.
 
Masuke ndio tumepeleka kikosi chetu B kupasha kombe la kuku kikosi A kipo katika mazoezi makali ya kutetea ndoo ya kagame
 
Last edited by a moderator:
Masuke ndio tumepeleka kikosi chetu B kupasha kombe la kuku kikosi A kipo katika mazoezi makali ya kutetea ndoo ya kagame

Mkuu nimeuliza mliwaokoteza wapi? maana inafahamika timu yenu haina kikosi B, na hili la Okwi hebu tueleze hii sio janja ya kutaka kuondoa maswali mengi kwa wanachama wenu na mashabiki wanayojiuliza ilikuwaje mkapeleka timu ya kuokoteza kwa jina la Yanga wakati kila siku wanasikia kwenye radio mmesajili wachezaji mahiri?

Lakini pia kuna mashindano ya vijana yanaanza tarehe 09 nchini Burundi na Yanga kama ina timu ya vijana wanatakiwa kwenda kushiriki sasa timu hiyo hiyo mkaipeleka Zanzibar kama ndo yenyewe kweli mashindano ambayo yanaisha tarehe 12 kama sijakosea na pengine timu ingefika fainali sasa hapo mngewezaje kushiriki mashindano mawili kwa wakati mmoja?
 
Okwi amewafanya vibaya kandambili.Khamsa, tano,five,fem zinawaotesha kandambili.Keep dreaming malapa.
Okwi punguza dozi next time malaria imewapanda kichwani.
 
ndo tatizo la soka la bongo,simba anafikir akimfunga yanga ndo maisha yamekwisha na yanga vivyo hvyo.nadhan ni vzur kufikir kuhusu maendeleo ya mbele kwan yanga kuchukua wachezaj wa simba lengo ni kulipiza kisasi lakin kimataifa maendeleo yatakua ni ndoto na hzi timu ztaendelea kuishia round za mwanzoni tu.
 
Jana nilimsikiliza kwa makini Bwana Nyange "Kaburi" alivyokuwa anaweweseka kuhusiana na Okwi mbele ya Press katika kipindi cha michezo cha Times Fm,eti na yeye ametoa siku 7 kwa gazeti lililoandika habari hiyo( ya Okwi ku'sign Yanga) kuhakikisha wanatoa habari ya kukanusha kwenye page ya mbele na kwamba wamewasiliana na Mwanasheria wao ili aweze kukishtaki chombo hicho cha habari endapo kitashindwa kufanya hivyo....poor Nyange "Kaburi" inaonekana anasahau kabisa kuwa kwenye suala la michezo hususani nyakati za usajili tetesi ni jambo la kawaida na chombo chochote cha habari kinaweza kuandika tetesi za aina hiyo pasipo kulazimika kukanusha endapo hata walichoandika hakitakuja kutokea,napenda kumshauri Bwana Nyange "Kaburi" kuwa aache kufikiria ki'Masaburi na kama anafikiria kile chombo cha habari kina haja ya kutoa habari ya kukanusha habari za Okwi ku'sign Yanga basi na Mwenyekiti wake pia aitishe Press akanushe habari alizoutangazia uma kuwa walishamsajili Nizar na wangemtambulisha siku ya Simba day au na yeye ashtakiwe.
 
Mkuu nimeuliza mliwaokoteza wapi? maana inafahamika timu yenu haina kikosi B, na hili la Okwi hebu tueleze hii sio janja ya kutaka kuondoa maswali mengi kwa wanachama wenu na mashabiki wanayojiuliza ilikuwaje mkapeleka timu ya kuokoteza kwa jina la Yanga wakati kila siku wanasikia kwenye radio mmesajili wachezaji mahiri?

Lakini pia kuna mashindano ya vijana yanaanza tarehe 09 nchini Burundi na Yanga kama ina timu ya vijana wanatakiwa kwenda kushiriki sasa timu hiyo hiyo mkaipeleka Zanzibar kama ndo yenyewe kweli mashindano ambayo yanaisha tarehe 12 kama sijakosea na pengine timu ingefika fainali sasa hapo mngewezaje kushiriki mashindano mawili kwa wakati mmoja?

Yanga ina team B kiongozi,althogh it is not as strong as ile ya kwenu, ila hii team ipo na hufundishwa na Keneth Mkapa na kipindi kingine na Salvatory Edward
 
Yanga ina team B kiongozi,althogh it is not as strong as ile ya kwenu, ila hii team ipo na hufundishwa na Keneth Mkapa na kipindi kingine na Salvatory Edward

Asante mkuu kwa kujibu maana naona niyemuuliza kala kona ya ajabu, ila viongozi wenu hawajafanya vizuri kutopeleka timu ya wakubwa kama walivyokubaliana kama walikubaliana kweli.
 
Yanga wamelazimika kuimba jina lake Airport wakimpokea kocha wao.Chezea Okwi wewe.:baby::baby::baby::baby::baby:OKWI OKWI OKWI ,OKWI OKWI.Mara 5,khamsa,punch,fem,five,mkono. Utaacha kuimba lazima uimbe.
 
Napenda kuchukua nafasi hii kuwatangazia rasmi,kwa forward line ya Yanga ya sasa hivi Said Bahanuzi "Spider Man",Hamis Kiiza "Diego" na Didier Kavumbagu...striker wa type ya Emanuel Okwi hana nafasi tena
 
Back
Top Bottom