Ofisi ya Bunge yakanusha ongezeko la Posho

"Dk Thomas Kashililah alipoulizwa kuhusu taarifa hizo alisema hawezi kuzungumzia jambo hilo kwa sababu siyo msemaji wa wabunge, bali Ofisi ya Bunge" Kama dk. kashilila alisema yeye si msemaji wa bunge kwa nini leo hii ajifanye ni msemaji wa bunge? Kwa mtazamo wangu Dr. Kashilila kasomeshwa na Nape kubadilisha ukweli kuwa uwongo na uwongo kuwa ukweli. kwa vyovyote vile posho ya wabunge imepandishwa, chukua maneno yangu!
 
"Dk Thomas Kashililah alipoulizwa kuhusu taarifa hizo alisema hawezi kuzungumzia jambo hilo kwa sababu siyo msemaji wa wabunge, bali Ofisi ya Bunge" Kama dk. kashilila alisema yeye si msemaji wa bunge kwa nini leo hii ajifanye ni msemaji wa bunge? Kwa mtazamo wangu Dr. Kashilila kasomeshwa na Nape kubadilisha ukweli kuwa uwongo na uwongo kuwa ukweli. kwa vyovyote vile posho ya wabunge imepandishwa, chukua maneno yangu!
BEI JUU-MKOLONI
 
Mkuu, nazani unakumbuka wakati wa utoto watu tunavyokua na ndoto za ajabu ajabu....mara nataka kuwa rubani, mara nataka kuwa rais, mara nataka kuwa mfanyakazi wa benki! myself, nilitamani sana kuwa mwandishi wa habari...why, sijui!! May be because nilikuwa napenda sana riwaya za Willy Gamba during my childhood! c unamjua Willy Gamba, Veronica Hamadu na Shareef?! c unakumbuka jinsi walivyoji-act waandishi wa habari hadi kufanikiwa kufichua njama za makaburu za kupora silaha za wapigania uhuru wa SA pale banadari ya Dar es salaam! dah, it was a very interesting novel, kama hujasoma then look for NJAMA! as for tht, nilipenda sana uandishi wa habari!! Lakini leo, dah! am very disappointed na hii fani!!! u knw wht i mean?! leo hii ukitaka kuanza kukanusha kila habari za kwenye magazeti then u need to establish idara maalumu kwa ajili hiyo tu!! Sio siri, hata zile habari zenye ukweli utakuta bado sina mapugunfu kibao!!

Hahaha, dah! wee Nas umenitoa ktk mada na kunikumbusha mbali sana. Hebu nambie kama Zabibu naye kafa naye wily gamba(E.m.u.s...b.a) au? Na je yule sikazwe wa makaburu ana uhusiano gani na kina hawa skazwe wa hapa bongo wa leo? Haha! Unajua ukisoma vile vitabu na ku-sense uzalendo ulio mle,then ukiangalia usalama wa taifa wa leo na usaliti wao, utaishia kulia au kuhama nchi km mimi, loh
 



Suala la mabadiliko la bosho za vikao vya bunge lilijadiliwa katika mkutano wa wabunge November 08, 2011
walipoiomba serikali iangalie upya suala hili ili kuboresha. Hadi tunapotoa taarifa hii serikali haijatoa taarifa kama posho hizo zimeongezeka kutoka kiwango cha awali na kufikia laki mbili.


Je katika huo mchakatato wa kuwaongezea posho imeombwa iwe kiasi gani na hao wabunge marafiki wa wanannchi wao maskini?
 
bungeletu.jpg


Bunge latoa tamko nyongeza ya posho
BAADA ya kuvuja kwa taarifa za kupanda kwa posho za vikao vya wabunge, Ofisi ya Bunge jana iliibuka na kutoa ufafanuzi kuwa, ingawa mjadala huo upo, posho hizo hazijaanza kulipwa. Juma lililopita gazeti hili liliripoti taarifa za ndani kwamba posho za wabunge zimepanda kutoka Sh70,000 hadi 200,000 hivyo kufanya bajeti ya posho hizo kwa mwaka kufikia Sh28 bilioni.

Kutokana na ongezeko hilo, taarifa hizo zilisema kila mbunge atakuwa akilipwa Sh80,000 kama posho ya kujikimu (perdiem) anapokuwa nje ya jimbo lake, posho ya vikao (sitting allowance) Sh200,000 na mafuta ya gari Sh50,000 kila siku, sawa na Sh330,000 kwa siku.
Wakati taarifa hiyo inaripotiwa, Katibu wa Bunge Dk. Thomas Kashililah alisema hawezi kuzungumzia jambo hilo kwa sababu yeye si msemaji wa Bunge na akashauri atafutwe Spika wa bunge.

Lakini, baada ya mjadala wa takriban juma moja wa wanaharakati, wabunge na wasomi kupinga nyongeza hiyo ya posho, jana Dk. Kashililah aliibuka na kukiri kuwa wabunge wanataka waongezewe posho za vikao, lakini mapendekezo hayo, hayajaanza kutekelezwa. Dk. Kashililah alitoa kauli hiyo katika taarifa yake aliyoisambaza kwa vyombo vya habari jana.

Kwa mujibu wa Katibu huyo bunge, mapendekezo ya kutaka posho za wabunge zipande, yaliibuka katika mkutano wa wabunge mjini Dodoma Novemba 8 mwaka huu, lakini hadi sasa hayajaanza kutekelezwa. "Suala la mabadiliko ya posho za vikao vya Bunge lilijitokeza katika Mkutano wa Wabunge, tarehe 8 Novemba, 2011 walipoiomba Serikali iangalie upya suala hilo kwa lengo la kuboresha,” alisema Dk Kashililah katika taarifa hiyo na kuongeza: ”Hadi tunapotoa tangazo hili (jana), Serikali haijatoa taarifa iwapo posho hiyo imeongezeka kutoka Sh70,000 hadi Sh200,000."

Dk Kashililah aliendelea kueleza "Kwa mujibu wa Waraka wa Rais kuhusu Masharti ya Mbunge uliotolewa tarehe 25 Oktoba,2010, wenye Kumbukumbu namba CAB111/338/01/83 na kusainiwa na Katibu Mkuu Kiongozi, pamoja na stahili zingine, Mbunge anastahili kulipwa posho ya kikao ambayo ni sawa na Sh70,000 kwa kila kikao na masharti hayo hayajafanyiwa marekebisho wala kufutwa."

"Kwa hiyo, taarifa hiyo iliyotolewa siyo sahihi, lakini endapo itatokea, mwenye mamlaka ya kupitisha kiwango kipya cha posho za vikao vya Bunge, itakuwa ni uamuzi kama uamuzi mwingine anaoutoa wa kuwaongezea watumishi wa umma mishahara, posho, marupurupu na mafao mengine."

Baada ya taarifa hiyo kuripotiwa Novemba 28 mwaka huu, wasomi, wanaharakati, wanasiasa na wabunge walitofautiana kwa kupinga na kukubali. Baadhi ya wabunge waliopinga nyongeza hiyo ni Januari Makamba wa jimbo la Bumbuli,mbunge wa Kigoma Kaskazini Zitto Kabwe na Mbunge wa Hai Freeman Mbowe.

Mbowe alisema walivyokuwa wakipinga posho hizo wakati zilivyokuwa Sh70,000 waandishi wa habari walichukua suala hilo kama ajenda ya Chadema, hivyo kupandishwa kwa posho hizo ni matokeo ya watu kuwapuuza walivyokuwa wakizipinga.

“Msimamo wetu sisi tulishautoa tangu wakati posho zikiwa Sh70,000 wakati sisi tukipinga hizi posho waandishi wa habari na Watanzania mlichukulia suala hili kama ajenda ya Chadema, sisi wenyewe tupo wachache bungeni, tulichotaka ni kuonyesha jinsi fedha za Watanzania zinavyotumika vibaya,” alisema na kuongeza:

“Achilia mbali hizo 200,000 za wabunge kuna watu huko serikalini wanalipwa mpaka Sh400,000 au Sh1 milioni kwa siku nyie ulizeni.”


Makamba ashutushwa Mbunge wa Bumbuli, January Makamba, alieleza kushangazwa na ongezeko hilo la ghafla akisema kamwe wabunge wasifikiri kuwa wanaweza kumaliza matatizo yao au ya wapigakura wao kwa fedha ya posho.

“Kwenye jamii lazima kuwe na usawa, kama watu tupo kwenye hali mbaya (ugumu wa maisha) lazima wote tuenende sawa. Wabunge kuongezewa posho kwa asilimia 185 siyo sawa kabisa, tunajiweka mbali na wananchi na wanatuona tunafaidika sana wakati wao wanateseka kwa ugumu wa maisha,” alisema Makamba. Alisema kuwa, kutokana na msimamo wake huo, Juni mwaka huu alikataa posho iliyotolewa na Wizara ya Nishati na Madini baada ya kuhudhuria semina iliyoandaliwa na wizara hiyo. “Tulikaa kwenye semina kwa saa mbili, tunamaliza naletewa karatasi nisaini posho ya Sh280,000 nilikataa.

Nilikataa kwa sababu nilitambua kuwa ile ni kazi yangu kama mbunge, sasa unanilipa hela ya kazi gani?” alihoji Makamba. Zitto adai ni usaliti Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe, alisema kuwa amestushwa na taarifa za kupandishwa kwa posho za vikao kwa wabunge huku wananchi wakiugulia ugumu wa maisha na kusema kuwa ipo siku Watanzania watawapiga mawe kwa usaliti huo.

“Nimeshtushwa zaidi kwamba posho hizi zimeanza kulipwa katika mkutano wa Bunge uliopita kabla hata Rais hajaamua, maana maslahi yote ya wabunge huamuliwa na Rais baada ya kupokea mapendekezo ya Bunge kupitia Tume ya Bunge,” alisema Zitto.

Aliwata wabunge wote kutambua kwamba, kuamua kujipandishia posho bila kuzingatia hali ya maisha ya mwananchi wa kawaida ni usaliti usio na mfano. “Mbunge yeyote ambaye anabariki jambo hili labda anaishi hewani, haoni taabu za wananchi au ni mwizi tu na anaona ubunge ni kama nafasi ya kujitajirisha binafsi,” alisema Zitto.

Wakati wabunge hao wakipinga John Shibuda wa Maswa Magharibi na mbunge wa Ludewa Deo Filikunjombe walizikubali wakisema ni sahihi. Filikunjombe alisema kuongezeka kwa posho hizo kunatokana na wabunge kuwa wanalipwa mishahara midogo kulingana na kazi wanayofanya.

“Ninachosema mimi, siyo wabunge peke yao, lakini watumishi wote wa umma wanalipwa mishahara midogo sana mimi binafsi sitegemei posho za Bunge, kabla ya kuingia bungeni nilikuwa nimefanya kazi kwa miaka 14 na nilikuwa napata mshahara mzuri tu,” alisema Filikunjombe. Shibuda adai posho muhimu Mbunge wa Maswa Mashariki (Chadema), John Shibuda alisema suala la wabunge kuongezewa posho halina ubaya wowote kwa kuwa litawafanya wasiwe ombaomba.

“Umefikia wakati Waafrika tulinde fedheha kwa viongozi wetu ili wasiwe ombaomba. Viongozi wakilipwa vizuri wataweza kuitumikia nchi na jamii inayowazunguka, ipasavyo. Kutokulipwa vizuri ndio mwanzo wa viongozi kusaini mikataba mibovu,” alisema Shibuda.

Tucta wawaka
Kwa upande wake Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi (Tucta), kitendo cha wabunge hao kujiongezea posho ni ishara ya kushindwa kutetea maslahi ya wananchi wao waliowapeleka bungeni. “Tucta inalaani kitendo cha wabunge kujiongezea posho kubwa kama hizo huku wakijua kuwa wananchi waliowachagua wanawategemea wao, hasa katika kipindi hiki kigumu cha maisha.

Jambo hilo linaonyesha wazi kuwa hawako kwa ajili ya kutetea maslahi ya wananchi, bali kujinufaisha wenyewe,”alisema Nicolaus Mgaya. Mwisho
 
Ndiyo uzuri wa kuandamana kwa kauli moja. Wananchi waliamua kuandamana kwa maoni na kuacha itikadi zao nyuma na bunge limepata ujumbe. Walikuwa wanatesti zali na wameona reaksheni kutoka kwa wananchi.
 
Naanza kupata wasiwasi na Gazeti la Mwananchi, limekua sehemu ya udaku
hivi kweli hakuna mbunge hata mmoja mpenda nchi ambae anaweza kujitokeza na kututhibitishia iwapo wamelipwa ama laa??\
chadema mpo wapi?
tuambieni ukweli.
 
Suala la mabadiliko la bosho za vikao vya bunge lilijadiliwa katika mkutano wa wabunge November 08, 2011 walipoiomba serikali iangalie upya suala hili ili kuboresha. Hadi tunapotoa taarifa hii serikali haijatoa taarifa kama posho hizo zimeongezeka kutoka kiwango cha awali na kufikia laki mbili.
Sasa kama Bunge linasubiri taarifa ya serikali ina maana ombi la ongezeko lipo au halipo?... Kama lipo kwa nini bunge liseme hii ni taariufa ya Uongo wakati wenyewe wamepitisha ongezeko hilo ktk vikao vyao..JK plse usipitishe kabisa matumizi mabovu kama haya..
 
41774_100001490228404_276_n.jpg


TAARIFA KWA UMMA

Hivi karibuni kumekuwa na taarifa iliyotolewa na baadhi ya vyombo vya habari na baadhi ya wabunge kuwa posho ya vikao vya bunge imeongezeka kutoka Sh 70,000/= hadi kufikia 200,000/=.

Suala la mabadiliko la bosho za vikao vya bunge lilijadiliwa katika mkutano wa wabunge November 08, 2011 walipoiomba serikali iangalie upya suala hili ili kuboresha. Hadi tunapotoa taarifa hii serikali haijatoa taarifa kama posho hizo zimeongezeka kutoka kiwango cha awali na kufikia laki mbili.

Tunasikitika na kushangaa sana kwa kauli hii kwani inajenga chuki baina ya wabunge na wananchi waliowapigia kura.

Posho inayotolewa kwa sasa ni ile iliyoainishwa kwenye waraka wa Rais wa October 25, 2010 ambayo iliridhia posho ya vikao kuwa 70,000/=

Kwa hiyo taarifa iliyotolewa siyo sahihi.

Imetolewa na
Dr. Thomas D. Kahililah
Katibu wa Bunge


Bofya link ya kijani hapo chini habari hii ilivyoripotiwa na Gazeti la Mwananchi kupata mengi zaidi.

Bunge latoa tamko nyongeza ya posho

Mama wa YUTONG kanusha tangazo hili
 
Hii kweli ni Serikali taahira!!! Nani tumwamini sasa kuhusu posho mpya? Tumuamini Kashilila au Makinda!?

~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~**~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*

Spika atetea posho mpya
Imeandikwa na Namsembaeli Mduma; Tarehe: 6th December 2011
Habarileo


SPIKA wa Bunge, Anne Makinda amekiri nyongeza ya posho za vikao vya wabunge kutoka Sh 70,000 hadi Sh 200,000 kwa siku na kusema imesababishwa na kupanda kwa gharama za maisha mjini Dodoma.

Ametetea uamuzi wa nyongeza hizo kuwa una nia njema ya kuwawezesha wabunge wamudu gharama za kuwawakilisha wananchi vizuri, kwa kuwa mishahara wanayolipwa ni midogo ikilinganishwa na gharama wanazoingia wakiwa bungeni.

Makinda alisema hayo Dar es Salaam jana baada ya kuzindua Ripoti ya Maendeleo ya
Wanawake Duniani kuhusu Haki kwa mwaka 2011.

Ripoti hiyo imeandaliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Jinsia na Uwezeshaji kwa Wanawake (UN Women) na Shirika la UN la Idadi ya Watu Duniani (UNFPA).

Makinda alitaja siku ambazo wabunge walilipwa posho hizo mpya kuwa ni Novemba 08, 09
na 11, mwaka huu pamoja na wiki ya pili ya Bunge la Mkutano wa Tano na kueleza kuwa
pasipo kuwa na vikao vya Bunge, wanacholipwa ni mshahara pekee.

“Ni vyema jamii ifahamu kuwa wabunge hawalipwi fedha nyingi kama inavyozungumzwa
na baadhi ya watu na kwamba, wanachobaki nacho baada ya makato ya mkopo wa gari na kodi, hakiwatoshi kumudu gharama zote wawapo Dodoma kuhudhuria vikao vya Bunge, kama vile malazi na nyinginezo,” alisema Makinda.

Akichanganua kipato cha mbunge kwa mwezi, Makinda alisema mbunge analipwa Sh
milioni 2.3 tu k
ama mshahara na katika malipo hayo, hukatwa Sh 700,000 za kodi na Sh
800,000 za mkopo wa gari. Kwa hesabu hizo, mbunge kwa mwezi anabakiwa na Sh 800,000 tu.

“Hebu fanyeni hesabu muone katika mshahara huo mbunge anabaki na shilingi ngapi? (Dah!!!)

Na mkumbuke pia kuwa fedha hiyo ndiyo anayoitumia kwa gharama za kutengeneza gari lake endapo litapata matatizo, mafuta na kwa ajili ya matumizi mengine kama atataka kwenda jimboni na kwingineko kwa sababu za kikazi,” alisema Makinda ambaye ni Mbunge wa Njombe Kusini (CCM).

Alisema posho ya Sh 70,000 isingemsaidia kumudu gharama hata za chumba kwa sababu
zimekuwa juu mno kutokana na mji wa Dodoma kuwa kituo cha elimu ya vyuo vikuu kwa sasa.

“Kila kitu kimepanda bei na kwa bahati mbaya nyumba zile za CDA (Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu) zilizokuwa nafuu zilichukuliwa na wabunge wa Bunge la Tisa kwa
mikataba binafsi na wengi hawajazirudisha hadi sasa ili kuwezesha wapya kuzipangisha,”
alisema Spika.


Kitendo hicho cha wabunge wa Bunge la Tisa kung’ang’ania nyumba za CDA kwa mujibu wa Makinda, kimesababisha wabunge wapya wapange hoteli ambako hutozwa fedha nyingi tofauti na kipato wanachokipata.

“Pia sio kweli kwamba posho hizo zinatolewa kinyemela kwa sababu zilipitishwa katika vikao halali na kukubaliwa kuwa atakayezipata ni yule mbunge atakayehudhuria vikao vya Bunge asubuhi mpaka vitakapoahirishwa tu.

“Atakayesaini asubuhi na jioni ndiye atakayekuwa na uhalali wa kulipwa. Hata Kabwe Zitto anayezizungumzia, hajapewa hata senti moja kwa kuwa hakuwepo vikaoni, alikuwa mbali,” alisisitiza Makinda na kuongeza kuwa mshahara huo ni wa tangu mwaka 2003 na haujawahi kufanyiwa marekebisho yoyote hadi sasa.

“Sioni kama kuna malipo ya kustaajabisha umma kwa sababu hali halisi inajionyesha wazi, mazingira ya gharama za maisha nazo zinaonekana kiasi cha kushawishi kuwepo kwa nyongeza hiyo katika posho,” alisema.

Hivi karibuni, Katibu wa Bunge, Dk. Thomas Kashililah alitoa taarifa kwa vyombo vya habari akikanusha kuwepo kwa nyongeza hiyo.

Dk. Kashililah katika taarifa hiyo alikiri kuwa wabunge wanataka waongezewe posho za vikao, lakini mapendekezo hayo, hayajaanza kutekelezwa.

Alisema mapendekezo ya nyongeza hiyo yaliibuka katika mkutano wa wabunge mjini Dodoma Novemba 8 mwaka huu, lakini hadi sasa hayajaanza kutekelezwa.

“Suala la mabadiliko ya posho za vikao vya Bunge lilijitokeza katika Mkutano wa Wabunge, tarehe 8 Novemba, 2011 walipoiomba Serikali iangalie upya suala hilo kwa lengo la kuboresha,” alisema Dk. Kashililah katika taarifa hiyo.

“Hadi tunapotoa tangazo hili (Jumapili), Serikali haijatoa taarifa iwapo posho hiyo imeongezeka kutoka Sh 70,000 hadi Sh 200,000," taarifa hiyo ilieleza.

 
BAK,we waonaje? Badala ya kuhangaika na Mt Kilimanjaro..,kwenye New Top 7 Wonders Of the World.... Iende nchi kama nchi..na si vivutio vilivyomo. Vinatuchukua muda kuvitangaza!
 
Back
Top Bottom