Ofisi ya Bunge yakanusha ongezeko la Posho

hata 70,000 wanayolipa haistahili. Ukiwa mbunge maana yake uhudhurie vikao vya bunge. Ndo kazi yako. Sasa kwa nini ulipwe?
Mkuu,

Mbunge anapoomba kura anasema kazi ninayoomba ni pamoja na kuwawakilisha bungeni, sasa hiyo kazi aliyoiomba atalipwaje mbona Daktari, Mwalimu hawalipwi posho? ili hali wote wanafanya kazi walizoomba
 
Oooo Ghosh!!!!!!!!!!!!!!!!! nilipanga kikao cha january niongeze nyumba ndogo nyingine, but mr. Kashililah can you came again on this important issue imetustua sana sisi wabunge, presha inapanda presha inashuka.
UNALETA MASIARA?? wenzako tunashindia uji kila kukicha heri ya jana we unapanga kuongeza mke kwa pesa zetu? Japo najua umetania lkn c utani mzuri!
 
Hii ofisi ya Bunge ni Wasanii wakubwa. Habari hii iko katika vyombo vya habari tangu wiki ya mwisho ya November hawakutia neno kwa zaidi ya wiki na January Makamba au Zitto Kabwe hawawezi kusema uongo kuhusu ongezeko hilo la posho, labda machale yamewacheza baada ya kuona Watanzania kuwajia juu kuhusu kuongeza posho hiyo huku Serikali ikiwa na madeni chungu nzima ambayo ni ya miaka mingi sasa

~*~*~*~**~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~**~*~**~

Makamba ashtushwa
Mbunge wa Bumbuli, January Makamba, alieleza kushangazwa na ongezeko hilo la ghafla akisema kamwe wabunge wasifikiri kuwa wanaweza kumaliza matatizo yao au ya wapigakura wao kwa fedha ya posho.
Alisema kitendo cha wabunge kuongezewa posho za vikao kwa asilimia 185.7, kinaleta jazba kwa wananchi ambao wanahangaika kila kukicha kwa ugumu wa maisha.

“Kwenye jamii lazima kuwe na usawa, kama watu tupo kwenye hali mbaya (ugumu wa maisha) lazima wote tuenende sawa. Wabunge kuongezewa posho kwa asilimia 185 siyo sawa kabisa, tunajiweka mbali na wananchi na wanatuona tunafaidika sana wakati wao wanateseka kwa ugumu wa maisha,” alisema Makamba.

Alisema kuwa, kutokana na msimamo wake huo, Juni mwaka huu alikataa posho iliyotolewa na Wizara ya Nishati na Madini baada ya kuhudhuria semina iliyoandaliwa na wizara hiyo.

“Tulikaa kwenye semina kwa saa mbili, tunamaliza naletewa karatasi nisaini posho ya Sh280,000. Nilikataa. Nilikataa kwa sababu nilitambua kuwa ile ni kazi yangu kama mbunge, sasa unanilipa hela ya kazi gani?” alihoji Makamba.

Habari hii imeandaliwa na Fredy Azzah, Frederick Katulanda, Mwanza, Patricia Kimelemeta, Fidelis Butahe na Ellen Manyangu

Posho za wabunge zazua mjadala
 
Asante CS! Sasa tunaomba vyombo vya habari vitwambie vilipata wapi hizi habari! Kuna watu wengi wametoa maoni!wengine wameng'aka na kufoka kumbe habari zenyewe uhongo!ngoja tuone vyombo vya habari watatwambia nini!
mkuu walikuwa wanabeep ili waone kama watanzania tutanyamaza kimya sasa wameona mambo yamefika shingoni wanaamua kutoa taarifa za upupu kama hizo.
 
Nimeamini kuna media ambazo zinatumiwa na chadema kuipaka matope serikali.

Yani embu jiulizeni yafuatayo:
1. Wabunge wote waliotoa maoni yao under the impression kuwa posho imepanda walikuwa misinformed na walikuwa ni wadaku?
2.january makamba na zito kabwe walivoandika waraka wao kila mmoja kupinga hawakujua kama hazijapanda au walikuwa wanaota?
3. Kuna baadhi ya wabunge(nadhani Mrema naye yumo) walisema hawana taarifa rasmi ya maandishi kuhusu kupanda kwa posho lakini kutokana na latest figures ni kweli posho zilikuwa zimepanda tofauti na kawaida yani alfu 70.
NB: Mrema yeye aliunga mkono kupanda kwa posho akidai wabunge wana majukumu mengi.
4. Bunge lilikuwa wapi kukanusha hayo muda wote? Walipata muda wa kukanusha ‘uongo‘ wa madai ya katiba ya chadema na lissu lakini huu hawakuwa na muda kuukanusha?

Kutokana na hayo mi nadhani ni kweli posho ilipanda.Hii kauli ya bunge ni a second thought baada ya kuona reaction ya umma.
 
Huyu katibu wa bunge ni kati ya watu wasioaminika kwasasa.....ni kati ya watu waliochakachua mswada wa katiba na sasa anaendelea kuchakachua ukweli.....
 
Ukiisoma vizuri habari hii kuna kitu kinazungukwa na ukweli kwamba vyombo vya habari vimeandika ukweli wa kilichojilia bungeni wakati bungeni wawakilishi wa wananchi waliridhia posho za vikao hivyo ziongezwe.

Bunge limekubali kwamba katika kikao cha bunge kilichopita waliomba serikali kuangalia upya posho za wabunge kwa maana ya kufanya uboreshaji kwa kuongeza kiwango chake. Nakumbuka Speaker Makinda alisema atachukua hatua stahiki baada ya wabunge kujadili jambo hilo. Wengi hatukuelekeza akili na masikio Dodoma wakati huo kutokana na kuelekea Arusha kwenye maandamano ya Chadema yaliyoleta purukushani pale uwanja wenye historia ya mageuzi ya kisiasa nchini.

Cha msingi serikali bado kuridhia, isipokuwa ukweli ungali pale pale kwamba wabunge wameomba kuongezewa posho za vikao kwa maana kwamba hawaridhishwi na posho za vikao wanazopata za sasa.
Bunge lina ajenda hapo kama hamjajua, linataka kuvunja maandamano ya walimu yanategemewa kuanza January maana kigezo kikubwa cha walimu ni kwa nini walimu wasilipwe madai yao wakati wabunhe wamepandishwa posho toka 70,000.00 hadi 200,000.00 ongezeko ambalo lingetosha kulipa madai yote ya walimu pasipo na shida yoyote?
 
Bunge lina ajenda hapo kama hamjajua, linataka kuvunja maandamano ya walimu yanategemewa kuanza January maana kigezo kikubwa cha walimu ni kwa nini walimu wasilipwe madai yao wakati wabunhe wamepandishwa posho toka 70,000.00 hadi 200,000.00 ongezeko ambalo lingetosha kulipa madai yote ya walimu pasipo na shida yoyote?
Exactly! Nchi hii inaendeshwa kwa matukio kwa sasa na sio sheria, kanuni, na taratibu. Aibu tupu.
 
Posho inayotolewa kwa sasa ni ile iliyoainishwa kwenye waraka wa Rais wa October 25, 2010 ambayo iliridhia posho ya vikao kuwa 70,000/=
Kwa hiyo taarifa iliyotolewa siyo sahihi.


Mimi hapo ndipo penye matatizo kwani allowance hii ilikuwa inatumika kabla ya October 2010 iweje Raisi atoe waraka huo mwezi wa October mwaka jana?
 
Wana jf walipoandika POSHO ILIYOTOLEWA KWA SASA ina maana gani?angeandika posho iliyotolewa tarehe,kikao,kiasi ndipo ingekua na ukweli!hapo kuna utapeli
 
Wasichomoe mchezo!

Nchi maskini hivi na wabunge (wengi wao wanaishi maisha ya anasa), wanapitisha mswada wa kuijongezea maposho!
Hata hawajiulizi kama kweli wafanyacho ni kama kuihujumu nchi!
Shauri yao, wanaona yanayotokea nchi za Uarabuni, Tanzania sio exception, anything can happen kama viongozi watajisahau na kujilimbikizia utajiri na kusahau waliowachagua!
 
kaka soma hii habari vizuri huku ukiitafakari vizuri hiyo habari, hiko so fishing. wanahabari kazi yao ni kuripoti tu kinachozungumzwa
na pia kuchokoza pia ni moja ya kazi zao. imewachukua muda mrefu sana kukanusha habari hii pia huyu kashilaha alishaulizwa before kuhusiana na issue hii akasema yeye sio msemaji wa bunge kwahiyo kesi hii bado haijafungwa.

Mkuu, nazani unakumbuka wakati wa utoto watu tunavyokua na ndoto za ajabu ajabu....mara nataka kuwa rubani, mara nataka kuwa rais, mara nataka kuwa mfanyakazi wa benki! myself, nilitamani sana kuwa mwandishi wa habari...why, sijui!! May be because nilikuwa napenda sana riwaya za Willy Gamba during my childhood! c unamjua Willy Gamba, Veronica Hamadu na Shareef?! c unakumbuka jinsi walivyoji-act waandishi wa habari hadi kufanikiwa kufichua njama za makaburu za kupora silaha za wapigania uhuru wa SA pale banadari ya Dar es salaam! dah, it was a very interesting novel, kama hujasoma then look for NJAMA! as for tht, nilipenda sana uandishi wa habari!! Lakini leo, dah! am very disappointed na hii fani!!! u knw wht i mean?! leo hii ukitaka kuanza kukanusha kila habari za kwenye magazeti then u need to establish idara maalumu kwa ajili hiyo tu!! Sio siri, hata zile habari zenye ukweli utakuta bado sina mapugunfu kibao!!
 
mkuu walikuwa wanabeep ili waone kama watanzania tutanyamaza kimya sasa wameona mambo yamefika shingoni wanaamua kutoa taarifa za upupu kama hizo.

Dah! ni kweli serikali ye2 inasemekana very stupid ..... lakini sizani kama imefikia u stupid wa kupandisha posho toka 70,000/= hadi 200,000/= ktk mazingira tulinayo sasa...at least to 100,000/= it can make sense!
 
Nalipongeza sana gazeti la Mwananchi kwa kuibua uozo huu. Wiki 1 iliyopita Habari hii ilipoibuliwa kwamba posho za vikao kwa wabunge zimepanda kimya kimya Kashilila mwenyewe alisema sio msemaji wa wabunge, ila kuna baadhi ya wabunge walikiri! Tunataka hao wabunge warudishe chenji ya hela ambayo walishapokea.
Pia nampongeza Rais kwa kuwa msikivu, kasikia kelele zetu, na chonde chonde tunamsihi asi sign hizo posho mpya. Huu sio muda muafaka.
 
Ongezeko lililokuwepo kwenye posho za mkutano uliopita lilikuwa kwa ajili ya kupitisha muswada wa mchakato wa katiba mpya!
Tunasubiri waraka wa serikali posho zipande rasmi, hapo kabla walituambia tunaweza kupandisha lakini leo wamebadilika wakasema tusubiri waraka.
Hata hivyo serikali imeahidi kupandisha posho kwa asilimia 500 pindi katiba mpya itakapojadiliwa na kupitishwa haraka ili tufikie lengo lililowekwa na serikali kulingana na muda.

IDARA YA MASLAHI KWA WAHESHIMIWA TANZANIA
 
Back
Top Bottom