Obama aliapishwa mara ya pili bila biblia

Exaud J. Makyao

JF-Expert Member
Nov 30, 2008
1,518
22
NIMEPATA UTATA WA UHALALI NA MAANA YA RAIS WA MAREKANI BARAK OBAMA KUAPISHWA MARA YA PILI BILA KUTUMIA BIBLIA KAMA ALIVYO FANYA MARA YA KWANZA.
NAPATWA NA WASI WASI KAMA JAMBO HILI NI SAWA.
Exaud J.Makyao
 
Kwani Biblia inatajwa kwenye Katiba kama kitu cha lazima kwenye kiapo Marekani? Sidhani. Kutumia Biblia ni chaguo la anayeapa (kama ilivyo Tanzania)

Iwapo kiapo cha kwanza kilikuwa valid, basi mara ya pili Obama "alirudia" kiapo. Kurudia kiapo ni kuapa mara mbili? Kwa mfano, wengi tunapenda kurudia ahadi za ndoa tunaposherekea Jubilee ya Ndoa (25 years). Kwa kurudia huko, utasema tumeoa mara mbili?

Kama kiapo cha kwanza cha Obama hakikuwa valid, basi aliapa alipofanya hivyo mara ya pili. In either case aliapa, validly, mara moja tu.
 
Je waungwana ni kweli Chief Justice aliamua kumuangusha makusudi Obama???????

Is it really a cospiracy theory kwa kuwa Obama ni Black Amerikan?
 
Je waungwana ni kweli Chief Justice aliamua kumuangusha makusudi Obama???????

Is it really a cospiracy theory kwa kuwa Obama ni Black Amerikan?

Kumuangusha kwani alizuia Obama asiwe Rais?. Hivyo ni vitu vya kawaida hutokea mara moja moja hasa kwenye situation kama hiyo ambayo Chief Justice anajua kuwa naye anaingia katika Historia lazima achachawe kidogo. Na hasa kama alijifanya ameweka kichwani maneno yote.

Hakuna kitu kama hicho kumuangusha. Na kitendo cha kurudia mara ya pili ni kuzima midomo michafu ya kina Rush na conservative wengine wasipate talking show kwa miaka 4.
 
Kwa mujibu wa katiba Obama alishakuwa raisi saa sita kamili mchana Januari 20 hata kabla ya kiapo, hivyo hicho kiapo cha pili it was, but just irrelevant.
 
Kumuangusha kwani alizuia Obama asiwe Rais?. Hivyo ni vitu vya kawaida hutokea mara moja moja hasa kwenye situation kama hiyo ambayo Chief Justice anajua kuwa naye anaingia katika Historia lazima achachawe kidogo. Na hasa kama alijifanya ameweka kichwani maneno yote.

Hakuna kitu kama hicho kumuangusha. Na kitendo cha kurudia mara ya pili ni kuzima midomo michafu ya kina Rush na conservative wengine wasipate talking show kwa miaka 4.

Unajua Obama akiwa senata alipiga kura kutomkubali huyu Chief Juctice..je yawezekama aliamua kummgeuzia kibao kwa makusudi?
 
Back
Top Bottom