Obama aguswa na Hasheem Thabeet

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,327
33,133
thabbet.jpg

Nyota wa Ligi Kuu ya Mpira wa Kikapu Marekani (NBA), Mtanzania Hasheem Thabeet

Jina la mcheza kikapu nyota wa Ligi Kuu ya Mpira wa Kikapu Marekani (NBA), Mtanzania Hasheem Thabeet lilijitokeza jana katika hotuba fupi aliyoitoa Rais wa Marekani, Barack Obama wakati akizungumza na waandishi wa habari, ikulu jijini Dar es Salaam.

Obama ambaye alikuwa amefuatana na mwenyeji wake, Rais wa Tanzania Jakaya Kikwete, alimtaja Thabeet kwa namna iliyoonyesha wazi kuwa anamfahamu vyema mchezaji huyo nyota wa timu ya Oklahoma City Thunder; huku akitania mwishoni mwa hotuba yake kwa kusema kuwa atamzungumzia siku nyingine.

Mtanzania Hasheem mwenye urefu wa mita 2.21, amejitwalia umaarufu mkubwa Marekani kutokana na uwezo wake uwanjani na pia kwa sababu hivi sasa ndiye mchezaji mrefu kuliko wote wanaocheza NBA.

Hasheeem alikwenda Marekani mwaka 2006 na kuanza kucheza NBA mwaka 2009 baada ya kusajiliwa na timu ya Memphis Grizzlies, hivyo kuandika rekodi ya kuwa Mtanzania wa kwanza kuwahi kucheza katika ligi hiyo yenye hadhi ya juu zaidi kwa mchezo wa mpira kikapu duniani.

Awali, kabla ya kuchomekea kwa utani jina la Hasheem katika hotuba yake, Obama alizungumzia namna Marekani inavyoshirikiana na Tanzania na mataifa mengine ya Afrika katika kukabiliana na changamoto mbalimbali kwa nia ya kusaidia harakati kuliendeleza bara hili.

ANENGUA 'LIVE' NGOMA YA MGANDA

Wakati akitua kwenye Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam akitokea Afrika Kusini, Obama alionekana kuvutiwa sana na ngoma mbalimbali za utamaduni alizochezewa wakati akipokelewa, zikiwamo za Mganda, Lizombe na Sindimba.

Kwa namna isiyotarajiwa, naye alijitosa na kuanza kunengua ngoma ya Mganda inayochezwa na wenyeji wa mkoa wa Ruvuma, huku akiungwa mkono na mwenyeji wake, Rais Kikwete na hivyo kuibua shangwe kubwa kutoka kwa wananchi waliokuwa wakishuhudia tukio hilo.

Kabla ya kuanza kucheza Mganda, Obama alianza kwa kumwaga tabasamu kuonyesha kuwa amevutiwa na ngoma hiyo, akawapigia makofi wachezaji na mwishowe akahitimisha hisia zake kwa kuanza kucheza.

Kabla ya Obama kutua, Rais Kikwete naye alionekana kuguswa na burudani ya ngoma zilizokuwapo uwanjani ambapo alikuwa akicheza kwa mtindo kama wa 'kiduku' muda mfupio kabla ya kuwasili kwa mgeni wake.

Katika hatua nyingine, mmoja wa watu waliofurahia salamu kwa kushikana mkono na kiongozi huyo alikuwa ni rais wa zamani wa klabu ya Yanga, Abbas Tarimba.

ZIARA YA OBAMA HAIMNUNUI RONALDO

Licha ya kuonekana kuwa ghali, gharama za jumla za ziara ya Rais Obama katika nchi tatu barani Afrika za Tanzania, Afrika Kusini na Senegal haikaribii hata kidogo fedha zilizotumiwa na klabu ya Real Madird ya Hispania kumnunua mshambuliaji wake Cristiano Ronaldo, imefahamika.

Kwa mujibu wa gazeti la Marekani la Washington Post, Obama na msafara wake watatumia dola za Marekani milioni 100 (Sh. bilioni 160) ili kujihakikishia usalama wakati wote wa ziara hiyo ambayo pia inawajumuisha mkewe Michele Obama na mabinti zake Malia na Sasha; kiasi ambacho ni kidogo kulinganisha na dau la paundi za England milioni 80 (Sh. bilioni 200) lililolipwa na Real Madrid kumtwaa Ronaldo kutoka Manchester United kabla ya kuanza kwa msimu wa 2009.

Hata hivyo, kiasi hicho cha fedha zinazotumiwa na Obama katika ziara yake Afrika (Sh. bilioni 160) kinalingana na bajeti za wizara tatu za serikali ya Tanzania kwa mujibu wa makadirio ya mapato na matumizi yaliyopitishwa bungeni mjini Dodoma hivi karibuni kwa mwaka wa fedha ulioanza jana wa 2013/2014.

Wizara ya Maliasili na Utalii imetengewa Sh. bilioni 75.6, Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais Sh. bilioni 55.6 na Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Sh. bilioni 30.3; hivyo jumla yao kuwa Sh. bilioni 161.5 ambazo ni sawa na gharama za ziara ya Obama barani.

Awali, baadhi ya Wamarekani walikuwa wakipinga ziara ya Obama barani Afrika kwa kudai kuwa ni ghali kwa taifa hilo, jambo ambalo limethibitika kuwa si sahihi na badala yake, ziara hiyo ina manufaa makubwa kiuchumi kwa Afrika na Marekani yenyewe kwani itasaidia pia kukuza fursa za kibiashara baina ya Afrika na taifa hilo.

CHANZO: NIPASHE

Mkuu Mh. waziri. Kwa kifupi, huyu jamaa Hasheem ni haibu kwa taifa kwani he's useless huko Marekani. Obama kama rais lazima ataongea vizuri juu yake kwa sababu ni kazi yake lakini uwongo haujitengi daima. Fuatilia habari za huyu kijana wetu mitandaoni, utakuta kuwa hana issue na amekuwa a dissapointment kwa kila timu aichezeae. Wenzake karibia ya wengi waliocheza na kutamba College wanakula hela za nguvu na wamekuwa masuper staa. Hasheem hana issue tofauti na tunavyodhania hapa Tanzania. Cha kusikitisha watu wengi huko Marekani pia hawamjuwi kwa sababu kucheza kwake ni nadra sana na mara nyingi anaingia dakika za majeruhi ili atoke jasho.
 
wivu wa kike
 
wivu wa kike

Wivu kama mtu unaongea uwongo, the dude is simply useless. Fuatilia makala za NBA huko Marekani utaona kama nakudanganya. Usiogope kusoma, kama huwezi kimombo wapo watu wa kukusaidia kutafsiri pamoja na mimi pia kama ukitaka.
 
wewe ni LIMBUKENI wa hizo lugha za magharibi,na siwezi shangaa kwani wa'KATA' wengi ndiyo mulivyo hasa uzao huu wa 2012!
Yaani kwa jinsi unavyoandika na 'psychology' yako inaonyesha wazi wewe ni wale wa vidole juu wasiopenda maendeleo ya wengine...dah!una safari ndefu ndugu yangu,
1.hebu taja mwanamichezo gani wa kibongo anayeingiza pesa nyingi?
2.Jivunie lugha yako,kujua swaenglish sio usomi....
3.Punguza au acha kabisa wivu usiokuletea wewe maendeleo kwani ipo siku utakufa kihoro....
4.Mpe hi mzee yusuph mwambie akusajili Jahazi na wewe naamini ukiwa na hadija yusuph au leyla rashidi mtafanya safi sana utampita Hasheem Thabeet kwa malipo na ukizingatia jamaa anakaa benchi ila analipwa vizuri
 
wabongo bhana, yaani kutajwa na obana wanadhani ndo anafanya vizuri, ni kwamba tu ndo mtanzanie pekee anaecheza mpira wa kikapu huko

ni kitu ambacho obama aliona akikisema kwenye audience itaonyesha anawependa watanzania, whether anapafomu au yuko benchi daily haimuhusu yeye kama rais, uwepo wake ndo muhimu basi
 
wewe ni LIMBUKENI wa hizo lugha za magharibi,na siwezi shangaa kwani wa'KATA' wengi ndiyo mulivyo hasa uzao huu wa 2012!
Yaani kwa jinsi unavyoandika na 'psychology' yako inaonyesha wazi wewe ni wale wa vidole juu wasiopenda maendeleo ya wengine...dah!una safari ndefu ndugu yangu,
1.hebu taja mwanamichezo gani wa kibongo anayeingiza pesa nyingi?
2.Jivunie lugha yako,kujua swaenglish sio usomi....
3.Punguza au acha kabisa wivu usiokuletea wewe maendeleo kwani ipo siku utakufa kihoro....
4.Mpe hi mzee yusuph mwambie akusajili Jahazi na wewe naamini ukiwa na hadija yusuph au leyla rashidi mtafanya safi sana utampita Hasheem Thabeet kwa malipo na ukizingatia jamaa anakaa benchi ila analipwa vizuri

Usiwe mjinga kijana. The truth never lies...huyu unayempigia debe is useless katika fani yake kila mtu Marekani anajuwa hilo isipokuwa wewe tu, mbona evidences are there to prove to you. Soma unaongopa nini, au hutaki kujuwa ukweli zaidi? Sasa kwa taarifa yako, unaambiwa wengi walio na kipaji kama yeye wanachota tu pesa kinoma tena mara 20 ya huyu yanki. Suala la yeye kuingiza pesa nyingi hapa Tanzania is not even a brainer...yule analipwa in dollars hata kama ni hela ya utumbo kwa hapa Tanzania lazima atakuwa ndiyo anaingiza zaidi shinda mwana michezo yeyote. Mbona wewe mjinga kihivyo, umesomea nini maishani mwako? Hawa vijana wa fleva bwana, yaani mtu unabisha kitu hata hujuwi unabishia nini, yaani ili mradi tu. Soma wasifu wa Hasheem katika makala za NBA utaona kama nakudanganya, usiwe mwoga wa kuogopa ukweli. Utamwonea wivu mtu asiye nyota katika fani yake wala mwelekeo, inakuja kichwani kweli hii?
 
Mkuu Mh. waziri. Kwa kifupi, huyu jamaa Hasheem ni haibu kwa taifa kwani he's useless huko Marekani. Obama kama rais lazima ataongea vizuri juu yake kwa sababu ni kazi yake lakini uwongo haujitengi daima. Fuatilia habari za huyu kijana wetu mitandaoni, utakuta kuwa hana issue na amekuwa a dissapointment kwa kila timu aichezeae. Wenzake karibia ya wengi waliocheza na kutamba College wanakula hela za nguvu na wamekuwa masuper staa. Hasheem hana issue tofauti na tunavyodhania hapa Tanzania. Cha kusikitisha watu wengi huko Marekani pia hawamjuwi kwa sababu kucheza kwake ni nadra sana na mara nyingi anaingia dakika za majeruhi ili atoke jasho.

Kuwepo tu NBA hata kama ni benchi basi ni hatua kubwa sana, ni ndoto ya vijana wengi duniani.

Kumbuka Hasheem anakipiga karibu kila mechi na takwimu zake zinaonesha kupanda.

Sijui umetokea dunia gani. Aliyekwambia una wivu wa kike kakosea, mimi naona una wivu wa kingese.
 
Back
Top Bottom