Hasheem Thabeet arudi Tanzania, kuichezea timu ya Pazi ligi ya kikapu Bongo

TheCrocodile

JF-Expert Member
May 31, 2021
1,077
2,814
Mtanzania Hasheem Thabeet amerejea nchini leo kwa ajili ya kujiunga na timu ya Basketball ya Pazi ambayo inajiandaa kwa ajili ya michezo ya hatua awali ya mchujo ya michuano ya BAL.

Hasheem amerejea Tanzania na kusema kuwa yupo mbioni kumaliza kucheza mpira wa Kikapu ila Watanzania wao kama timu ya Pazi watarajie mambo makubwa.

“Sio ni Mimi nimekuja kucheza ni timu ya Pazi kwa ujumla, wategemee mabadiliko katika basketball, imekuwa miaka mingi tunafanya tu ila naona kama hatufiki ila muda wangu ukikaribia kabisa mimi kumaliza basketball unakaribia, lengo langu kubwa ni mimi kurudi nyumbani kuja kufanya basketball katika level ambayo Tanzania inatakiwa icheze”

Link:
View: https://twitter.com/millardayo/status/1705395333768069619

Source:MillardAyo
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom