Nyumba za wadaiwa sugu Tanesco kupigwa mnada

LE GAGNANT

JF-Expert Member
Jan 20, 2011
1,241
251
SHIRIKA la Umeme Tanzania (Tanesco), limesema kuwa linaandaa utaratibu wa kupiga mnada nyumba za watu na kampuni kubwa binafsi ambazo wamiliki wake ni wadaiwa sugu wa shirika hilo.

Shirika hilo sasa limetoa wiki mbili kwa wadaiwa hao kulipa malimbikizo ya madeni yao kabla hatua ya kufidia madeni hayo kwa kuuzwa nyumba, haijaanza kutekelezwa.
Meneja Uhusiano wa Tanesco, Badra Masoud alisema jana jijini Dar es Salaam kuwa, utaratibu huo mpya wa kufidia madeni ya Tanesco utaanza baada ya kipindi hicho cha wiki mbili kumalizika.

Nyumba za wadaiwa sugu Tanesco kupigwa mnada

SASA HAWA TANESCO WANA-CONCENTRATE KUJIANDAA KUPIGA MNADA NYUMBA ZA WATU NA KAMPUNI KUBWA BINAFSI. WANA MPANGO GANI NA WADAIWA SUGU SERIKALINI?
 
Waanzie majengo ya mawizara kwanza.

Hivi hayo madeni sugu wanayozungumzia yako kwenye mfumo wa secured loans? Yana collateral au namna gani? Manake sielewi vipengele vya sheria vimekaaje hapo.
 
0,,16085187_401,00.jpg

[h=4]Matukio ya Afrika[/h] [h=2]Tanzania: Tanesco kupiga mnada nyumba za wanaodaiwa deni la umeme[/h]

Meneja wa uhusiano wa shirika la Umeme nchini Tanzania, Badra Masoud, amewaonya wezi wa umeme nchini kwamba shirika lake liko mbioni kuwakamata wezi wote na kuhakikisha wanalipa madeni wanayodaiwa na shirika hilo.
Meneja wa uhusiano wa shirika la Umeme nchini Tanzania, Tanesco, Badra Masoud, amewaonya wezi wa umeme nchini humo kwamba shirika lake liko mbioni kuwakamata wezi wote na kuhakikisha wanalipa madeni wanayodaiwa na shirika hilo.
Badra amesema baada ya wiki mbili shirika lake litaanza kupiga mnada nyumba za watu pamoja na za kampuni kubwa kubwa nchini humo ambazo zinazodaiwa na TANESCO. Hata hivyo, Badra Masoud amesema shirika hilo pia litaanza mikakati ya kupambana na wafanyakazi walaji rushwa ambao wanashindwa kutekeleza majukumu yao.
Awali Amina Abubakar alizungumza na Badra Masoud na mwanzo alitaka kujua zaidi juu ya mikakati hiyo ya Tanesco katika kuwakamata wezi wa umeme....
Insert
Mwandishi Amina Abubakar
Mhariri Othman Miraji



SOURCE: Tanzania: Tanesco kupiga mnada nyumba za wanaodaiwa deni la umeme | Matukio ya Afrika | DW.DE | 20.08.2012
 
I am just passing.
The other wonder is how were those debts accumulated ? In music they say you need two to tangle. I assume power is supplied to customers according terms and conditions and a contract must be in place.
If those buildings are not part of the contract then I can see the power utility entering into litigation which might end up to be very costly. Anyway the played the game together with negligence some of those debts are now bad debts.
The utility must be smart and counter the challenges kulalamika and kulia is not going to collect the monies. Let wait and see!
 
Kwani waliingia mkataba na wateja wao na nyumba zikawekwa dhamana?eeh hebu nijitahidi kutumia akili yangu mluga luga mimi...
 
Ukiona watawala wanaanza kutunga sheria za hovyo hovyo na kuwa fikra kama watoto wa primary ,ujue ndio mwisho wao wa kufikiria na wamejawa na ufisadi kichwani,na nywele tu hakuna la ziada...nyumba anakaa mpangaji unaweza ukainadi bila docs halali toka kwa mwenye nyumba?hakuna njia nyingine za kuwadai na walipe?mbona ile ya luku ingekuwa nzuri zaidi?fungia luku woote unakata 10% ya deni kwa kila nunuzi la luku....itasaidia na atamaliza deni lake muda mfupi tu!!
 
Waanze na serikali maana serikali ndio mdaiwa namba moja na mdaiwa mkuu wa tanesco!!
 
Kwani waliingia mkataba na wateja wao na nyumba zikawekwa dhamana?eeh hebu nijitahidi kutumia akili yangu mluga luga mimi...

Huyo Badri Meneja Uhusiano shule imempiga chenga,kwa kweli tamko kuwa watapiga mnada nyumba ya mteja ni kichekesho.
Sikubaliani na wizi wa umeme lakini sioni jinsi watskavyoweza kuuza nyumba za wadaiwa.
Kwa msingi huo huyu Badri anauhadaa umma kwa maana mlolongo wa deni la umeme mpaka kuattach mali ya mdaiwa unsongelea miaka hapo.
 
Serikali ya mapinduzi zanzibar imemaliza deni wanalodaiwa?
 
Wafanyakazi wa tanesco wanashirikiana na wadaiwa kuficha madeni. Anzeni kujisafisha wenyewe tanesco.
 
Back
Top Bottom