Nyumba ya Meya wa Manispaa ya Moshi yashambuliwa

Magesi

JF-Expert Member
Jul 10, 2012
2,587
573
Hali katika kata ya Pasua usiku kucha kuanzia jana ilikua imechafuka baada ya wananchi kuchukizwa na maamuzi ya kikundi cha ulinzi shirikishi katika mtaa wa Bomambuzi kuwapiga mpaka kuwasababishia vifo watu wawili ndugu kuwatuhumu kuwa ni wez.

Chanzo ni wizi uliotokea katika duka la bidhaa na mwenye duka hilo kumhisi mfanyabiashara mwenzake kuwa amehusika nawizi huo na kuwakodisha kikundi hicho maarufu KUNGURU ambacho kinafadhiliwa na Meya wa manispaa ya moshi Mh. JAFFAR MICHAEL kumhoji mfanyabiashara huyo dukan kwake na kumkuta na vocha zikiwemo zilizoibiwa ndipo walipoanza kuwapiga mpaka kupoteza maisha na wananchi wakaanzisha vurugu kupinga mauaji hayo kwa kuwa waliouawa walikua sio wezi bali aliuziwa baadhi ya vocha.

Vurugu ilikua ni kubwa kwan nyumba katika mtaa wa bomambuzi zimechomwa moto na nyingine kupasuliwa vioo ikiwemo ya Meya. Polisi walishindwa kudhibiti machafuko hayo kutokana na maelfu ya watu wakiwa na silaha za jadi kuwashinda nguvu vurugu zimeendelea mpaka alfajiri.

Mpaka sasa ulinz ni mkali Polisi wamemwagwa kila mahali.Vijana wa KUNGURU wengi wameshatiwa mbaroni mpaka sasa kwa kweli uharibifu ni mkubwa kwan nyumba nyingi zimeharibiwa
 
haya ndo matokeo ya watu kukosa imani na vyombo vyetu vya kutulinda
 
Uamuzi ni sahihi kabisa hata mm sitakubalu ndugu yangu auawe kwa kuhisiwa, Dola piga marufuku kikundi cha KUNGURU na meya ashtakiwe ikishindikana piga kura ya kutokuwa na imani naye msiangalie Chama ni MUUAJI huyo kama story ni ya kweli
 
Siku hizi mameya na viongozi wengine 'wanafadhili' vikundi, na vinaweza kufanya mahojiano? Huko tunakoelekea siko kabisaa!
 
Ukinunua kitu cha wezi na wewe ni mwizi tu. Vocha zinauzwa kwa maajenti kibao, kwanini ununue za wizi?
 
Hali katika kata ya Pasua usiku kucha kuanzia jana ilikua imechafuka baada ya wananchi kuchukizwa na maamuzi ya kikundi cha ulinzi shirikishi katika mtaa wa Bomambuzi kuwapiga mpaka kuwasababishia vifo watu wawili ndugu kuwatuhumu kuwa ni wez.Chanzo ni wizi uliotokea katika duka la bidhaa na mwenye duka hilo kumhisi mfanyabiashara mwenzake kuwa amehusika nawizi huo na kuwakodisha kikundi hicho maarufu KUNGURU ambacho kinafadhiliwa na Meya wa manispaa ya moshi Mh.JAFFAR MICHAEL kumhoji mfanyabiashara huyo dukan kwake na kumkuta na vocha zikiwemo zilizoibiwa ndipo walipoanza kuwapiga mpaka kupoteza maisha na wananchi wakaanzisha vurugu kupinga mauaji hayo kwa kuwa waliouawa walikua sio wezi bali aliuziwa baadhi ya vocha.Vurugu ilikua ni kubwa kwan nyumba katika mtaa wa bomambuzi zimechomwa moto na nyingine kupasuliwa vioo ikiwemo ya Meya.Polisi walishindwa kudhibiti machafuko hayo kutokana na maelfu ya watu wakiwa na silaha za jadi kuwashinda nguvu vurugu zimeendelea mpaka alfajiri. Mpaka sasa ulinz ni mkali Polisi wamemwagwa kila mahali.Vijana wa KUNGURU wengi wameshatiwa mbaroni mpaka sasa kwa kweli uharibifu ni mkubwa kwan nyumba nyingi zimeharibiwa

Huyo meya ni wa CCM au CDM?
 
Ni kweli tunahitaji taarifa lakini taarifa ziwe na ukweli na kama ni tetesi ni vyema ionyeshwe ni tetesi. Taarifa ya kushambuliwa kwa nyumba ya Meya wa Manispaa ya Moshi, Jaffar Michael (Chadema) si sahihi.

Ni kweli kuna nyumba kama 10 zilishambuliwa kwa mawe na wananchi wenye hasira waliokuwa wakitaka kulipiza kisasi kwa kikundi kinachojulikana kama JAMAA Group maarufu kama KUNGURU HAFUGIKI ambacho kiliwakamata watu wawili na kuwatesa kisha mmoja kufariki dunia jana.

Wananchi zaidi ya 500 walifika nyumbani kwa Meya huyo jana saa 5:00 usiku kwa lengo la kushambuliwa nyumba yake lakini alipotoka na kuzungumza nao na kuwaeleza hana uhusiano na kikundi hicho, wananchi hao waliondoka bila hata kurusha jiwe moja.

Hivyo si sahihi kusema nyumba yake imeshambuliwa. Ni kweli wananchi walichoma matairi na kuharibu vioo, madirisha na milango ya baadhi ya nyumba lakini hakuna iliyochomwa, polisi walidhibiti hali hiyo ambayo ilidumu hadi usiku wa manane.
 
Ni kweli tunahitaji taarifa lakini taarifa ziwe na ukweli na kama ni tetesi ni vyema ionyeshwe ni tetesi. Taarifa ya kushambuliwa kwa nyumba ya Meya wa Manispaa ya Moshi, Jaffar Michael (Chadema) si sahihi. Ni kweli kuna nyumba kama 10 zilishambuliwa kwa mawe na wananchi wenye hasira waliokuwa wakitaka kulipiza kisasi kwa kikundi kinachojulikana kama JAMAA Group maarufu kama KUNGURU HAFUGIKI ambacho kiliwakamata watu wawili na kuwatesa kisha mmoja kufariki dunia jana.......
Hapa unapotosha kuhusu Meya kuongea na wananch, kwan Meya mwenyewe baada ya kuona kundi la wa2 linakuja alitoka na gari kwa hyo hakupata nafasi ya kuongea nao. Nyumba yake ilirushiwa mawe baada ya kuondoka.Hata waandishi wa habari wa TBC Wamechukua picha na wamemhoji mstahikh Meya mapema asubuh
 
umeambiwa meya!
Elewa kuwa ni meya!
Hakutangazwi sera hapo,
ni meya full stop

jogi vipi mbona watumia miguvu kiasi hiki????? watu wanataka ufafanuzi kujua ni wa chama gani na pengine chama chake kina maoni gani juu ya tuhuma za meya wake!!! kulikoni.......???
 
jogi vipi mbona watumia miguvu kiasi hiki????? watu wanataka ufafanuzi kujua ni wa chama gani na pengine chama chake kina maoni gani juu ya tuhuma za meya wake!!! kulikoni.......???

sawa mkuu, sikuwa na uelewa ulio nao, ushaambiwa ni wa chadema, tuambie ulichokusudia kusema.
 
Huyo Meya atakuwa na uhusiano wa karibu na Mwita Mwikwabe, maana wote wauaji mashuhuri kutoka CHADAMu.
 
Hata musoma pia kuna vikundi vya kihalifu kama MDOMO WA FURU,MBIO ZA VIJITI,WEST LAWAMA na JAMAICA MOKERS.ni vikundi hatari sana kwa usalama wa raia na mali zao.
 
Hali katika kata ya Pasua usiku kucha kuanzia jana ilikua imechafuka baada ya wananchi kuchukizwa na maamuzi ya kikundi cha ulinzi shirikishi katika mtaa wa Bomambuzi kuwapiga mpaka kuwasababishia vifo watu wawili ndugu kuwatuhumu kuwa ni wez......

Dah, Jaffary si ndo walokua wanamwangalia kwa jicho la tatu kama Mrithi wa Ndesa? Uckute ndo kampeni chafu zishaanza?
 
moshi wote ni wajanja wajanja tu
wanaibiana wenyewe kwa wenyewe,
mbaya ni kuua tu.
 
Back
Top Bottom