Jimena
JF-Expert Member
- Jun 10, 2015
- 25,920
- 95,936
- Thread starter
- #261
Sasa mkuu kuogopa kwako kutoka nje ya mwili haimaanishi kuwa hilo haliwezekaniNiwe muwazi kwako na wengine,mmoja wa hao waliopoteza mtoto ni mimi,sitaenda into details.
Kama nilivyosema vitu vyote vinaanzia katika ulimwengu wa roho na baadaye vinadhihirika katika physical world.Hata wachawi(najua hauamini lakini wapo kwani hata Mungu anatambua uwepo wao) hunuiza maneno wanapotaka kufanya jambo fulani kwa imani na ikibidi hutoa sadaka ili kufanikisha jambo hilo.
Ndoto ni njia mojawapo ambayo Mungu anaweza kuitumia kuongea na wanadamu,ambacho wanadamu tunakosea tukiota ndoto hatuendi mbele za Yehova(ambaye wewe haumwamini) kumwuliza ndoto hii ina maana gani.Sasa unapo ota ndoto,mara nyingi kuna muda wa wewe kufanya jambo kuhusu hilo uliloliota,sasa ukiwa hujui unjikuta haujari then yakitokea unasema lakini nakumbuka nilishawahi kuota ndoto kuhusu jambo hili.
Mwanadamu alivyoumbwa naturally lazima atakuwa anaabudu kitu,that is why usipoabudu Mungu wa kweli utaabudu miungu mingine au hata vitu.Unafanya hivyo kwa sababu ndani yako kuna kiu cha kuabudu.
Mwanadamu anakosea zaidi akienda kutafuta msaada kwa mtu asiyemtegemea Mungu,kama watabiri wa nyota,waganga wa kienyeji etc.Mungu wetu ni Mungu mwenye wivu unapofanya hivyo anachukia,alitegemea uende kwake kuomba msaada yeye akusaidie.Hapa JF kuna watu wanatumiwa na shetani aidha wanajijua au hawajijui,wana nguvu fula ya ushawishi ndani yao na wanaposema kitu wasiojua huamini kirahisi.Hata wewe uwe makini kuhusu ndoto yako badala ya kupata msaada utaongezewa matatizo.Huta jua mwanzoni kwani utendaji wa shetani una umakini wa hali ya juu,wewe utaonma umesaidiwa na kuna mambo utayaona kweli yanatokea lakini in reality utapotezwa.
Kwa wale wanaoamini unapo ota ndoto hauifahamu,unakimbilia kwa Mungu kama ni ndoto mbaya unamwomba akuepushe nayo,kama ni jambo fulani unamwomba akusaidie kuelewa maana ya ndoto,kwa mfano kilichokukuta wewe unatakiwa ufahamu maana yake au kama ulivyosem je wewe ni nyoka.
NBiwe muwazi kwako sikujui lakini mtu husema kilichoujaza moyo wake,post zako hap zinaonyesha hauamini katika Mungu,na hapo tayari unakuwa umefungua milango ya adui kukushambulia.Falme ni mbili tu,kuna ufalme wa Mungu na ufalme wa shetani,ni lazima kila mtu atakuwa katika ufalme mmoja wapo.
Kuna watu walikuambia mambo ya uchawi,naomba nichangie kidogo si lazima wewe ushiriki inawezekana wazazi wako labda ulipokuwa mdogo walukukabidhi kwa miungu au hata wazazi wa wazazi wako walikabidhi ukoo kwa miungu.Katika ulimwengu wa roho kuna mikataba na maagano,hata kama hukushiriki unakuwa involved kwa sababu aliyeshiriki mwanzo alikabidhi vizazi vyote huko.
Kuna mtu hapa analalamika kwanini kosa alifanya adamu tunahukumiwa hata sisi?Kama wewe ni mwanadamu na hukutokana na adamu na Hawa sawa lakini kama ulitokana na Adam na Hawa,kwa wanawake utazaa kwa uchungu ,mwanaume utakula kwa jasho lako.
Ndoto yako unahitaji msaada ,ulinishauri nifanye stral projection ,je wewe ulishafanya hii kitu?OBE(out of body experience) haishauriwi kwa christians labda kama iwe imeanzisha na Mungu mwenyewe na si wewe.Katika ulimwengo huo kuna demons na kila aina za roho chafu sasa ukitoka nje ya mwili kule unakua haupajua je ni nani mwenyeji wako?Watu wanafanya matokeo yake wanakuwa vulnerable to bad spirit alafu huku mnajisifu kwamba kuna vitu mmegundua ni kweli lakini mwisho wake si mzuri.
Biblia inamwita shetani kama baba wa uongo.
Ushauri wangu kwako leo na muda huu,mbingu na ardhi ni mashahidi kwani vitu hivi vimekuwepo tangu mwanzo.Kuna Mungu alikuumba,naye anahitaji uishi katika njia zake,nyenyekea chini ya mkono wake naye atakuponya.In a nut shell,surrender your life to Jesus and you will be surprised.Mpaka wewe umeota ni nyoka maana yake huna ulinzi,you cab be used ,wachawi pia huweza kutumia sura za watu kufanya uchawi wao.Anaweza akaja kwako kama aqua,ukifanyiwa maombi yanatamka jina la mtu,ukiwa mwilini unajenga na vita na huyo mtu,ukiwa rohoni unaenda mbele za Mungu kumwuliza kama ni kweli.
Kuna mambo mengi yamefichwa kwa wanaojiita wasomi na yamefunuliwa kwa watu dhaifu wengine hata darasa la saba hawajasoma.
Niulize kama kuna kitu unahitaji kujua zaidi.
Hiyo ni moja, pili hizo hadithi nyingine nimeshazisikia sana ila hazina ukweli wowote ule,
Asante sana Aqua kwa maelezo marefu yaliyojaa Imani