Nyoka wa ajabu

Jimena

JF-Expert Member
Jun 10, 2015
25,843
95,770
Habari za mda huu wana JF

Siku ya leo mapema tuu mchana kwenye saa saba wakati napitia posts mbali mbali hapa jamvini nilijikuta nimepitiwa na usingizi wa ghafla.

Na kujikuta nipo mazingira ambayo sijawahi kuyaona, na nilikuwa katika umbo la nyoka kimwili na mawazo pia, hilo halikunishangaza sana kwa sababu nilijiona kuwa mimi ni nyoka na niliona hayo ndio maisha yangu ya siku zote kama nyoka wengine,

Lakini ghafla kulitokea na njiwa wawili waliotua mbele yangu juu ya mti ulio mfano wa miti ile ya Crismass, nami nikaanza kuupanda ule mti kwa taratibu na busara kwa lengo la kuwakamata wale njiwa ili niwale...

Cha ajabu nilipofika juu na kuwakaribia nikagundua kuwa wale sio njiwa ila ni kunguru, na mimi kama nyoka nilikuwa sina tabia ya kula kunguru hivyo niliamua kushuka chini bila kuwabugudhi niendelee na mambo mengine lakini nilipofika chini na kutazama tena juu ya ule mti niliwaona kuwa ni njiwa na wala si kunguru kama nilivyofikiri hapo mwanzo, kwa mara ya pili niliamua kurudi tena juu ya mti ili niwakamate, ila nilipofika juu niliwaona ni kunguru na wala sio njiwa, hichi kitu kilinishangaza sana, maana nikiwa chini nawaona kama njiwa lakini nikiwa juu nawaona kama kunguru...

Wakati nipo katika dimbi la mawazo nisijue nini cha kufanya mara ghafla chini ya ule mti alipita sungura...

Hapo sasa nikaachana na habari ya wale njiwa/kunguru na kuanza kumfukuza yule sungura,

Ghafla nikashituka maana nilikuwa naamshwa ili nile chakula cha mchana na nilipongalia saa ilikuwa ni saa saba na dakika ishirini na tano mchana

Shida yangu hapa sio tu kutaka kujua hii ndoto inamaanisha nini Ila nikukutaka kujua mimi ni nani?

Je mimi ni binadamu ambaye nawaza/kuota kuwa nyoka au ni nyoka ambaye anawaza/kuota kuwa binadamu???

Na je maisha yangu na ufahamu wangu kwa sasa upo wapi?
Ni kwa nyoka au binadamu?
Na ni yapi ni maisha yangu ya kweli ninayoishi sasa kati ya nyoka au binadamu?

Cc Appolo Annael Bennie 369 Mkuu wa chuo aretasludovick pamoja na wengine wote ambao mna ufahamu kuhusu haya maswala naomba ufafanuzi wenu maana naona muda unapita bila mimi kupata ufumbuzi kwenye hili
 
cc: mshana jr

Yaweza kuwa ulisinzia kuelekea kaskazini ya chumba ulichokuwepo.... wataalam wanasema ikiwa hivyo utaota ndoto za mang'am ng'am.

Wewe ni mtu wa wapi? Kwenu mna mizimu?
Kuna mkoba (uchawi) kwenye familia na haujakabidhiwa mtu?

Jina unalotumia ni la kurithi kutoka kwa bibi au shangazi au .....? Huyo mwenye jina asili alikuwa na mambo ya matambiko? Kama huna basi kuna roho inakutafuta. .....

La itakuwa malaria inakaribia kupanda kichwani wapi hospital.

La ilikuwa ni njaa usiku huu ukilala hutoota tena hivyo.

Pole.
 
Nimejikuta nacheka peke yangu. Mkuu angalia isije ikawa unataka kupata malaria kweli, unajua ungeuliza ndoto ina maana gani ningekuelewa, ila unapouliza wewe ni nani ndio hapo umeniacha hoi. Wewe si binadamu au? ungekuwa nyoka ungeweza kweli hata kuja humu JF?
 
Ndoto ya mchana ...wanaota wasichana
1469390463022.jpg

cc: mshana jr

Yaweza kuwa ulisinzia kuelekea kaskazini ya chumba ulichokuwepo.... wataalam wanasema ikiwa hivyo utaota ndoto za mang'am ng'am.

Wewe ni mtu wa wapi? Kwenu mna mizimu?
Kuna mkoba (uchawi) kwenye familia na haujakabidhiwa mtu?

Jina unalotumia ni la kurithi kutoka kwa bibi au shangazi au .....? Huyo mwenye jina asili alikuwa na mambo ya matambiko? Kama huna basi kuna roho inakutafuta. .....

La itakuwa malaria inakaribia kupanda kichwani wapi hospital.

La ilikuwa ni njaa usiku huu ukilala hutoota tena hivyo.

Pole.
Maswali yako ni magumu sana ila ntayajibu kwa kadri ninavyoelewa
Kuhusu uchawi hata sijui kama kuna ambae ana mikoba na hajaikabidhi
Sijarithi jina la mtu yoyote
Pia familia yangu sio watu wa maswala ya kufatilia mizimu kabisa
Kuhusu upande niliolalia sina hakika acha nichunguze maana sipo kwangu niko ugenini mpaka usiku ndio nategemea kuondoka
Asante sana
 
Nimejikuta nacheka peke yangu. Mkuu angalia isije ikawa unataka kupata malaria kweli, unajua ungeuliza ndoto ina maana gani ningekuelewa, ila unapouliza wewe ni nani ndio hapo umeniacha hoi. Wewe si binadamu au? ungekuwa nyoka ungeweza kweli hata kuja humu JF?
Itabidi kufanya kipimo hicho mkuu
 
Hapa ninachokiona huyu muota ndoto,ndoto na biashara zake zinashabiana kama alipita njia ya waganga wa kienyeji, kwa hiyo basi, kwa kuwa Kuna ushindani wa kibiashara na wafanyabiashara wenzie, Kuna kuwa na nguvu ya mvutano ndio anaota ndoto kama hizo
 
Na kama ni mfanya biashara kweli ila biashara haikuhusisha kabisa hayo maswala ya waganga au mambo kama hayo inaweza kuwa ni tatizo gani na nini kifanyike?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom