Nyoka wa ajabu

Habari za mda huu wana JF

Siku ya leo mapema tuu mchana kwenye saa saba wakati napitia posts mbali mbali hapa jamvini nilijikuta nimepitiwa na usingizi wa ghafla.

Na kujikuta nipo mazingira ambayo sijawahi kuyaona, na nilikuwa katika umbo la nyoka kimwili na mawazo pia, hilo halikunishangaza sana kwa sababu nilijiona kuwa mimi ni nyoka na niliona hayo ndio maisha yangu ya siku zote kama nyoka wengine,

Lakini ghafla kulitokea na njiwa wawili waliotua mbele yangu juu ya mti ulio mfano wa miti ile ya Crismass, nami nikaanza kuupanda ule mti kwa taratibu na busara kwa lengo la kuwakamata wale njiwa ili niwale...

Cha ajabu nilipofika juu na kuwakaribia nikagundua kuwa wale sio njiwa ila ni kunguru, na mimi kama nyoka nilikuwa sina tabia ya kula kunguru hivyo niliamua kushuka chini bila kuwabugudhi niendelee na mambo mengine lakini nilipofika chini na kutazama tena juu ya ule mti niliwaona kuwa ni njiwa na wala si kunguru kama nilivyofikiri hapo mwanzo, kwa mara ya pili niliamua kurudi tena juu ya mti ili niwakamate, ila nilipofika juu niliwaona ni kunguru na wala sio njiwa, hichi kitu kilinishangaza sana, maana nikiwa chini nawaona kama njiwa lakini nikiwa juu nawaona kama kunguru...

Wakati nipo katika dimbi la mawazo nisijue nini cha kufanya mara ghafla chini ya ule mti alipita sungura...

Hapo sasa nikaachana na habari ya wale njiwa/kunguru na kuanza kumfukuza yule sungura,

Ghafla nikashituka maana nilikuwa naamshwa ili nile chakula cha mchana na nilipongalia saa ilikuwa ni saa saba na dakika ishirini na tano mchana

Shida yangu hapa sio tu kutaka kujua hii ndoto inamaanisha nini Ila nikukutaka kujua mimi ni nani?

Je mimi ni binadamu ambaye nawaza/kuota kuwa nyoka au ni nyoka ambaye anawaza/kuota kuwa binadamu???

Na je maisha yangu na ufahamu wangu kwa sasa upo wapi?
Ni kwa nyoka au binadamu?
Na ni yapi ni maisha yangu ya kweli ninayoishi sasa kati ya nyoka au binadamu?

Cc Appolo Annael Bennie 369 Mkuu wa chuo aretasludovick pamoja na wengine wote ambao mna ufahamu kuhusu haya maswala naomba ufafanuzi wenu maana naona muda unapita bila mimi kupata ufumbuzi kwenye hili
Shukuru Mungu hukuona choo........
 
Ndoto imebeba ujumbe!
Na ndo kinachokusumbua!.
Ww ni mtu,shida ni nafsi ipo wapi!?

A u christian?
Nikusaidie mafundisho fulani hv, kuhusu ndoto frm bible!
 
Ndoto imebeba ujumbe!
Na ndo kinachokusumbua!.
Ww ni mtu,shida ni nafsi ipo wapi!?

A u christian?
Nikusaidie mafundisho fulani hv, kuhusu ndoto frm bible!
No iam not..... Lakini unaweza kutoa hayo mafundisho kwa niaba ya wengine
 
Kivipi??

Pia mi bado sijafa mkuu

usiulize maswali Mengi sana...Wewe elewa kuwa umefanikiwa kujua maisha yako after death

Ila tambua kuwa Hapo ulikuwa unapitishwa katika ufahamu wa maisha yako yajayo....huna muda mrefu sana katika hali yako ya ubinadamu.......

Nikuulize swali lingine...Ulikuwa nyoka wa aina gani?
 
Sio fair kuniambia nisiulize maswali mengi wakati nimeuliza moja tu hujalijibu zaidi ya kuongeza swali jingine.
Nilikuwa napitishwa na nani kwenye hayo maisha yajayo?
 
Sio fair kuniambia nisiulize maswali mengi wakati nimeuliza moja tu hujalijibu zaidi ya kuongeza swali jingine.
Nilikuwa napitishwa na nani kwenye hayo maisha yajayo?

Sasa naona wewe hutaki kuelewa

Aliyekuumba ndiye aliyekuwa anakupitisha
 
Hahahahaaaaa! Mkuu umenifurahisha sana, swali lako ni moja, naona majibu zaidi ya 100 lakini huoneshi kuyakubali majibu ya wadau. Kuna kitu unafahamu ww hapa unatuangaisha tu!
Mim naweza kukujibu hivi; we ni jinsi unavyofikiria, binadamu tunafikiri kila dakika aidha kwa kujua au kutojua! Ndio maana wakati mwingine MTU anaweza akawa sehemu fulani kimwili huku mawazo yakiwa mbali sana. Nadhani nimeeleweka....
 
Sijakubaliana na ambao wamesema vitu ambavyo sivifahamu kabisa
 
Huwa sifatishi ndoto kabisa, na huwa naota vitu vingi tu lakini napuuzia, hiyo ilinishangaza kwavile ilikuwa mchana halafu tofauti na ndoto zingine hiyo nimeota kama ninmebadilika na kuwa nyoka, na pia niliweka bayana kuwa lengo la huu uzi sio tu kuambiwa ndoto hiyo ina maana gani tu, bali pia nilipenda kwenda deep zaidi ili nipate kufahamu kama mimi ni binadamu mwenye mawazo ya nyoka au Nyoka mwenye mawazo ya kuwa binadamu au ni vipi?
Jimema nilikuwa naendelea kusoma post ili nije nikujibu lakini nimeona hii post yako nikaona niseme kitu hapa.Ni muhimu kutunza kumbukumbu kwa kuandika or any means za ndoto unazoota,ndoto ni njia mojawapo ambapo Mungu huweza kuongea na watu kuhusu mambo yanayokuja.Usipofanya kitu mambo hayo hutokea na yakiwa mabaya inauma sana.
Vitu vyote vinaanzia katika ulimwengu wa roho kama ambavyo kila kitu kinaanza na idea then unapofanyia kazi idea yako kinakuwa kitu halisi.Unapokuwa umelala the unconscious mind inadominate na inaweza kukufahamisha mambo mengi,kuna mtu mmjo siku nyingi aliniambia kwamba huwa tunaota ndoto nyingi ila kukumbuka utakumbuka si zaidi ya tatu per night.
NB:Usidharau ndoto unazoota sometimes unapewa taarifa za mambo yajayo ukipuuza yatakupata.Trust me I know two parents walipoteza watoto wao,lakini kabla ya watoto kufa waliota ndoto na huwa haichukui muda sana unakuta around miezi mitatu mambo yanatokea.
Naendelea kusoma post nitakujibu kuhusu wewe kuota kuwa nyoka,binafsi sishangai kwani najua unachoamini na umeacha milango wazi sasa wageni wanapoingia am not surprised my sister.
 
Hao wazazi wangefanyaje ili kuzuia vifo vya hao watoto??

Mi hii niliyoieleza hapa ndio ndoto pekee niliyowahi kuifikiria na ndio nikadiriki kuandika huu uzi. Ila pia nimeshaachana nayo, sasa kama itatokea siku nikageuka nyoka ndo nitajua kuwa ndoto huwa ni kweli
 
Niwe muwazi kwako na wengine,mmoja wa hao waliopoteza mtoto ni mimi,sitaenda into details.
Kama nilivyosema vitu vyote vinaanzia katika ulimwengu wa roho na baadaye vinadhihirika katika physical world.Hata wachawi(najua hauamini lakini wapo kwani hata Mungu anatambua uwepo wao) hunuiza maneno wanapotaka kufanya jambo fulani kwa imani na ikibidi hutoa sadaka ili kufanikisha jambo hilo.
Ndoto ni njia mojawapo ambayo Mungu anaweza kuitumia kuongea na wanadamu,ambacho wanadamu tunakosea tukiota ndoto hatuendi mbele za Yehova(ambaye wewe haumwamini) kumwuliza ndoto hii ina maana gani.Sasa unapo ota ndoto,mara nyingi kuna muda wa wewe kufanya jambo kuhusu hilo uliloliota,sasa ukiwa hujui unjikuta haujari then yakitokea unasema lakini nakumbuka nilishawahi kuota ndoto kuhusu jambo hili.
Mwanadamu alivyoumbwa naturally lazima atakuwa anaabudu kitu,that is why usipoabudu Mungu wa kweli utaabudu miungu mingine au hata vitu.Unafanya hivyo kwa sababu ndani yako kuna kiu cha kuabudu.
Mwanadamu anakosea zaidi akienda kutafuta msaada kwa mtu asiyemtegemea Mungu,kama watabiri wa nyota,waganga wa kienyeji etc.Mungu wetu ni Mungu mwenye wivu unapofanya hivyo anachukia,alitegemea uende kwake kuomba msaada yeye akusaidie.Hapa JF kuna watu wanatumiwa na shetani aidha wanajijua au hawajijui,wana nguvu fula ya ushawishi ndani yao na wanaposema kitu wasiojua huamini kirahisi.Hata wewe uwe makini kuhusu ndoto yako badala ya kupata msaada utaongezewa matatizo.Huta jua mwanzoni kwani utendaji wa shetani una umakini wa hali ya juu,wewe utaonma umesaidiwa na kuna mambo utayaona kweli yanatokea lakini in reality utapotezwa.
Kwa wale wanaoamini unapo ota ndoto hauifahamu,unakimbilia kwa Mungu kama ni ndoto mbaya unamwomba akuepushe nayo,kama ni jambo fulani unamwomba akusaidie kuelewa maana ya ndoto,kwa mfano kilichokukuta wewe unatakiwa ufahamu maana yake au kama ulivyosem je wewe ni nyoka.
NBiwe muwazi kwako sikujui lakini mtu husema kilichoujaza moyo wake,post zako hap zinaonyesha hauamini katika Mungu,na hapo tayari unakuwa umefungua milango ya adui kukushambulia.Falme ni mbili tu,kuna ufalme wa Mungu na ufalme wa shetani,ni lazima kila mtu atakuwa katika ufalme mmoja wapo.

Kuna watu walikuambia mambo ya uchawi,naomba nichangie kidogo si lazima wewe ushiriki inawezekana wazazi wako labda ulipokuwa mdogo walukukabidhi kwa miungu au hata wazazi wa wazazi wako walikabidhi ukoo kwa miungu.Katika ulimwengu wa roho kuna mikataba na maagano,hata kama hukushiriki unakuwa involved kwa sababu aliyeshiriki mwanzo alikabidhi vizazi vyote huko.
Kuna mtu hapa analalamika kwanini kosa alifanya adamu tunahukumiwa hata sisi?Kama wewe ni mwanadamu na hukutokana na adamu na Hawa sawa lakini kama ulitokana na Adam na Hawa,kwa wanawake utazaa kwa uchungu ,mwanaume utakula kwa jasho lako.
Ndoto yako unahitaji msaada ,ulinishauri nifanye stral projection ,je wewe ulishafanya hii kitu?OBE(out of body experience) haishauriwi kwa christians labda kama iwe imeanzisha na Mungu mwenyewe na si wewe.Katika ulimwengo huo kuna demons na kila aina za roho chafu sasa ukitoka nje ya mwili kule unakua haupajua je ni nani mwenyeji wako?Watu wanafanya matokeo yake wanakuwa vulnerable to bad spirit alafu huku mnajisifu kwamba kuna vitu mmegundua ni kweli lakini mwisho wake si mzuri.
Biblia inamwita shetani kama baba wa uongo.
Ushauri wangu kwako leo na muda huu,mbingu na ardhi ni mashahidi kwani vitu hivi vimekuwepo tangu mwanzo.Kuna Mungu alikuumba,naye anahitaji uishi katika njia zake,nyenyekea chini ya mkono wake naye atakuponya.In a nut shell,surrender your life to Jesus and you will be surprised.Mpaka wewe umeota ni nyoka maana yake huna ulinzi,you cab be used ,wachawi pia huweza kutumia sura za watu kufanya uchawi wao.Anaweza akaja kwako kama aqua,ukifanyiwa maombi yanatamka jina la mtu,ukiwa mwilini unajenga na vita na huyo mtu,ukiwa rohoni unaenda mbele za Mungu kumwuliza kama ni kweli.
Kuna mambo mengi yamefichwa kwa wanaojiita wasomi na yamefunuliwa kwa watu dhaifu wengine hata darasa la saba hawajasoma.
Niulize kama kuna kitu unahitaji kujua zaidi.
 
Hao wazazi wangefanyaje ili kuzuia vifo vya hao watoto??

Mi hii niliyoieleza hapa ndio ndoto pekee niliyowahi kuifikiria na ndio nikadiriki kuandika huu uzi. Ila pia nimeshaachana nayo, sasa kama itatokea siku nikageuka nyoka ndo nitajua kuwa ndoto huwa ni kweli
Jimema amka,ukiwa nyoka utajuaje kama ndoto huwa ni kweli si tayari umekuwa nyoka?
Mzazi hawezi kuzui kifo isipokuwa Mungu,wazazi wanachofanya nikuingia katika maombi na kukataa yale mabaya yote au kuzui mambo hayo yasitokee.Kwa sababu Mungu alikuonyesha ndotoni maana yake anajua unaweza kuzuia ukimtegemea yeye.
Si kila ndoto ina maana ila zingine zina maana kwako wewe hauko salama sikutishi kwani huu ndiyo ukweli.Unachokiamini unajua mwenyewe.Mrudie Mungu wako leo ,biblia inasema msimpe ibilisi nafasi,ukimpa nafasi huwa aleti mapozi anakumaliza kwelikweli.Wewe najua hata ukitaka ujaribu kutakuwa na ugumu kwani kuna vitu amepanda katika ufahamu wako,as I said before in order for the glass to be filled with new water you need to empty it first.
Tafuta video za Joyce Meyer online(youtube etc) zitakusaidia hasa ukipata anazoongelea how satan attack our mind.
Ukiwa na shida usisite kunishirikisha kama utahitaji msaada,kukuombea hata usiponiambia nitafanya.kama ambavyo huwa namwombea Kiranga na wengine of that type.
 
Hizo hadithi mi nimeshazisikia sana na wala hazina ukweli wowote ule
 
Hizo hadithi mi nimeshazisikia sana na wala hazina ukweli wowote ule
Ok,kama ni hadithi na hauko tayari kupokea bado unazidi kuacha milango wazi,nakupa ushauri mzuri lakini kutokana na vitu vilivyo ndani yako unaona ni hadithi,watakuja hao wa upande wa pili nao utawasikiliza.kama ni kweli umeota ulivyosema kuna vitu vinafanyika katika ulimwengu wa roho muda ukifika vitadhihilika.Kama hutaki kuamini watumishi waliopo sasa hata akifufuka unayemfahamu akaja hutaamini.Nimefanya kazi yangu juu ya nafsi yako,Bwana mwenyewe atajua cha kufanya juu yako yeye anazo njia nyingi lakini uwe makini kwani ukishupaza shingo inawezavunjika.
Tatizo ulilonalo wewe hata kuna baadhi ya watumishi huwapata,Mungu anaweza akaongea na wewe kupitia mtu na usielewe kama ni Mungu amemtumia huyo mtu kuongea na wewe.
Kasome Yoshua24:15
"Kama hamtaki kumtumikia Mwenyezi-Mungu, basi chagueni leo hii ni nani mtakayemtumikia: Kwamba ni miungu ile ambayo wazee wenu waliitumikia ngambo ya mto Eufrate, au miungu ya Waamori ambao sasa mnaishi nchini mwao. Lakini mimi na nyumba yangu, tutamtumikia Mwenyezi-Mungu.”
Basi Kwa kuwa hautaki ushauri wa kimumngu subilia waje watakaokushauri kwa hekima na elimu za kidunia au za ule ufalme wa giza.
 
Hizo hadithi mi nimeshazisikia sana na wala hazina ukweli wowote ule
kwe kwe kwe....
umenichekesha kwa jibu ulilompa katoa maelezo meeeengi....!!
kama kuota hata mimi nishaota sana mpk mda mwengine nikawa na hofu lkn there is no anything matter..
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom