Nyoka Mwenye Mkono Mmoja Awashangaza Wanasayansi China

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,322
33,126
3106010.jpg

Thursday, September 17, 2009 2:58 AM
Nyoka aliyezaliwa akiwa na mkono mmoja nchini China amewashangaza wanasayansi nchini China. Nyoka huyo aligundulika baada ya kuingia kwenye nyumba ya bibi mmoja nchini humo nyakati za usiku.

Bibi Xiu Qiong Duan, 68, aliliambia shirika la habari la Beijing, SINA kwamba usingizi wake ulikatika usiku wakati aliposikia kitu kikwaruza kwaruza kwenye kuta za chumba chake.

"Niliamka usiku baada ya kusikia sauti ya kitu kikwaruza kwaruza kwenye ukuta wa chumba changu.. awali nilifikiri watakuwa ni wezi" alisema.

"Nilipowasha taa nilishtushwa kuona kiumbe hiki cha ajabu kikitambaa kwenye ukuta kwa kutumia mkono wake".

Nyoka huyo alikuwa na mkono mmoja uliochomoza kwenye mwili wake ukiwa na vidole vyenye kucha.

Duan, mkazi wa mji wa Suining uliopo magharibi mwa China alisema kuwa alichukua kiatu na kuanza kumpiga nacho nyoka huyo mpaka alipofariki.

Asubuhi ya siku iliyofuatia aliuchukua mwili wa nyoka huyo na kuwakabidhi wanasayansi wa kitengo cha sayansi cha China katika mji wa Nanchang.

Mtaalamu wa nyoka katika kitengo hicho cha sayansi, Long Shuai alisema kuwa walishtushwa kumuona nyoka huyo wa ajabu ambaye alikuwa na urefu wa sentimeta 40 na unene sawa na unene wa kidole kidogo cha mkono.

"Hatuwezi kusema chochote sasa hivi mpaka tutakapomaliza kumfanyia uchunguzi", alisema mtaalamu huyo wa nyoka.

Wanasayansi katika kitengo hicho walisema kuwa walishawahi kuona nyoka waliozaliwa wakiwa na vichwa viwili lakini hawajawahi kuona nyoka aliyezaliwa akiwa na mkono mmoja. GONGA HAPA KUMUONA KWA UKARIBU NYOKA HUYO
http://www.nifahamishe.com/NewsDetails.aspx?NewsID=3106010&&Cat=2
 
Back
Top Bottom