Nyoka aua mtu na kukaa juu ya kaburi lake

kilimasera

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
3,068
268
Kioja cha mwaka kimetoke nchi jirani, Kenya, ambapo Gazeti la Daily nation limenukuliwa likiripoti kuwa, Nyoka aliyekuwa anafugwa na mwanakijiji mmoja huko kaskazini mwa Kenya, alifanya tukio la ajabu.

Nyoka huyo alifanya tukio hilo pale alipomgonga anayemfuga na kumuua kisha nyoka huyo akajificha. Baada ya maziko nyoka huyo alionekana akikaa juu la kaburi la mfuga nyoka huyo. Mchungaji wa eneo hilo, alishangazwa pale alipoona waombolezaji wakikimbilia kaburini baada ya kumuona huyo nyoka akiwa juu ya kaburi na wakamuua papo hapo.

Wanakijiji wakasema, nyoka huyu ndiye Yule Yule aliyekuwa akimfuga. Watu wa kiji hicho wana utamaduni wa kufuga nyoka na kuwatumia kwa njia za kishirikina. Ama kweli kunguru hafugiki.
 
Mara nyingi uchawi ukizidi sana Mungu anakulaani na unakurudia wewe mwenyewe!!
 
Kwekwekwe jk naye anafuga manyoka,tena yenye sumu kali juzi yalitaka yaongezewe unga mfugaji akagoma sasa yanataka kummeza!!na wana kijiji wana mpango wa kumwamisha kijijini, kuku zao zimekwisha kutokana na majoka ya jk anawapoza wanakijiji jana tu kawapelekea mayai huko longido ili kuwatuliza Tuungane kumuondoa mfuga nyoka huyu kijijini kwetu
 
majoka ya jk yanatafuna hela kama hayana akili nzuri
 
Kwekwekwe jk naye anafuga manyoka,tena yenye sumu kali juzi yalitaka yaongezewe unga mfugaji akagoma sasa yanataka kummeza!!na wana kijiji wana mpango wa kumwamisha kijijini, kuku zao zimekwisha kutokana na majoka ya jk anawapoza wanakijiji jana tu kawapelekea mayai huko longido ili kuwatuliza Tuungane kumuondoa mfuga nyoka huyu kijijini kwetu

Hahahahahahahahahaha niliyaona magari ya msafara wake eneo la arusha air port jana jioni wakati anaondoka nikaanza kuyahesabu nikapata magar 53 pikipik 3
 
Back
Top Bottom