Nyimbo ya mtanzania yapigwa MTV BASE

Zombie S2KIZZY

JF-Expert Member
Mar 15, 2021
823
1,613
Ni ngumu sana kuona kwenye channel za wenzetu wakipiga ngoma zetu za kibongo yaan labda ya msanii mkubwa Sana Africa na sehem zingine duniani.

Sisi channel zetu zinaweka sana utimu mbele na kupiga ngoma za wanaigeria,wamarekani na kudidimiza sanaa ya bongo na ndy maana wasanii wanawaiga wanaigeria ,wasouth na wamarekani kufanya miziki kama Yao sababu ndy inayochezwa Sana kwenye radio na TV za kibongo.

Aah By the way shukrani kwa baadhi ya mashabiki wa kibongo na mashabiki wengi wa nje ya bongo ambao ndy wanatukubali Sana.

Maana huku nyumbani tunachukiwa ,tunatukanwa na kukejeliwa sababu tu ya mafanikio yetu wasanii 🙌

Shukrani pia kwa MTV BASE kuicheza hii ngoma pekee ya kitanzania au niseme ya kiswahili kwenye channel yenu na kuiweka kwenye top 10 ya ngoma Kali afrika nzima, nayo imeshika nafasi ya 7 👏👏👏.

Haters endeleeni kuchukia namwisho wa siku mziki wa bongo upotee kabisa kwenye ramani ya Africa na Dunia kwa ujumla ,maana ukimtoa Big hakuna msanii yeyote anaetambulika kimataifa Hapa Tanzania ,
Watanzania tupende vya kwetu,
Asante Mungu
Asante Diamond Platnumz
Asante mashabiki
Asante haters
Asante Tanzania, East Afrika,Dunia nzima
Asante MTV BASE
Asante JamiiForums.

InShot_20231107_184307873.jpg
 
Usichokijua ni kwamba MTV Base imeletwa africa kupitia nigeria kwa ajili ya kupromote mziki wa nigeria 80% ! Kisha south. Hapo mwanzo walishoboka na ngoma za east africa ili wapate-mileage tu. Hata BET wameileta africa na imefikia nigeria na 80% zinapigwa ngoma za naija na south tu! Something is wrong kwa PARAMOUNT labda hawajajua ukubwa wa hizo taasisi jinsi Africa tunavyozichukulia kana kwamba hata TRACE kaja kuwa-overtake.

Kinachofanyika hata sisi akitokea mfanya biashara mkubwa anaweza kuwashawishi FOX ENTERTAINMENT ije Tanzania kwa kusudi la kupromote contents za africa ila TANZANIA tukapewa 70% ya airtime all day!.
 
Mliopata DStv baada ya punguzo la bei mnakera, MTV Base wamepiga hadi nyimbo za AY na Juma nature…
Vanessa Mdee alikua Presenter miaka ya 2000’ nyeusi ( I bet ulikua hujui lol)
 
Nyimbo ikipigwa sisi inatussidia nini labda ,nyimbo kupigwa huko itamsaidia mwenyewe huko

Ova
 
Mtv base ya wapi homeboy? Mbona kitambo wanacheza ngoma za wabongo au mimi ndio sielewi unachozungumzia

Mara kibao kabla ya Vanessa kupiga chini mziki ngoma zake zilikuwa zinachezwa au yeye hakuwa mtanzania?
Achana na kipindi kile cha Vanessa
Mi nazungumzia kipindi Cha katikati hapo zilikua hazipigwi kabisa yaan unaweza tizama video asubuhi mpk jion huwez ona nyimbo ya mtanzania
Ila now heshima ya mbongo imeanza Rudi hivyo
 
Mliopata DStv baada ya punguzo la bei mnakera, MTV Base wamepiga hadi nyimbo za AY na Juma nature…
Vanessa Mdee alikua Presenter miaka ya 2000’ nyeusi ( I bet ulikua hujui lol)
Sasa nashindwa kujuaje na wakati vanessa ni mshkaji wangu tokea kitambo ,
Kitu ambacho hujaelewa mi nimezungumzia ngoma za kibongo kupigwa miaka ya hivi karibuni let's say 2019 mpk now
 
Ni ngumu sana kuona kwenye channel za wenzetu wakipiga ngoma zetu za kibongo yaan labda ya msanii mkubwa Sana Africa na sehem zingine duniani.

Sisi channel zetu zinaweka sana utimu mbele na kupiga ngoma za wanaigeria,wamarekani na kudidimiza sanaa ya bongo na ndy maana wasanii wanawaiga wanaigeria ,wasouth na wamarekani kufanya miziki kama Yao sababu ndy inayochezwa Sana kwenye radio na TV za kibongo.

Aah By the way shukrani kwa baadhi ya mashabiki wa kibongo na mashabiki wengi wa nje ya bongo ambao ndy wanatukubali Sana.

Maana huku nyumbani tunachukiwa ,tunatukanwa na kukejeliwa sababu tu ya mafanikio yetu wasanii 🙌

Shukrani pia kwa MTV BASE kuicheza hii ngoma pekee ya kitanzania au niseme ya kiswahili kwenye channel yenu na kuiweka kwenye top 10 ya ngoma Kali afrika nzima, nayo imeshika nafasi ya 7 👏👏👏.

Haters endeleeni kuchukia namwisho wa siku mziki wa bongo upotee kabisa kwenye ramani ya Africa na Dunia kwa ujumla ,maana ukimtoa Big hakuna msanii yeyote anaetambulika kimataifa Hapa Tanzania ,
Watanzania tupende vya kwetu,
Asante Mungu
Asante Diamond Platnumz
Asante mashabiki
Asante haters
Asante Tanzania, East Afrika,Dunia nzima
Asante MTV BASE
Asante JamiiForums.

View attachment 2807113
Wakati mwingine unatakiwa kuandika hivi; Wimbo wa Mtanzania wapigwa MTV BASE. Na siyo Nyimbo ya Mtanzania yapigwa MTV BASE.

Nyimbo ~ nyingi/zaidi ya mmoja
Wimbo ~ mmoja
 
Back
Top Bottom