Habari zenu Wakuu,
Mimi sio mfuatiliaji wa Muziki wa nyumbani (Bongo Fleva) ila nimekuwa nikisikia nyimbo za wasanii wetu ambazo maudhui yake ni tabia mbovu za mtu (Character).
Kipindi cha miaka ya nyuma kuna wimbo uliimbwa na Sir Nature wimbo wenyewe unaitwa (Mtoto Idd) kama sijakosea, ukiusikiliza ule wimbo ni dhahiri kuwa wenye majina ya Idd walikuwa wanapitia kipindi kigumu kutokana na watu kuwatania
Wimbo wa Mtoto Idd ni wimbo unaozungumzia Tabia mbaya za mtu binafsi, lakini jambo la kusikitisha ni kwamba msanii alitumia jina hilo na kuzua taharuki kwa wenye majina hayo nchini.
Hivi karibuni kuna wimbo mwengine nimeusikia unaitwa "Sele", ambao kaimba msanii wa BongoFleva pia. Ukiangalia maudhui yake ni kumuongelea mtu vibaya lakini jina la mtu ndio limetumika kama Character ya wimbo.
Swali langu kwa Mamlaka za kusimamia wasanii ni hili,
Ni lini mtakemea wasanii kutumia majina ya watu kama kiwakilishi cha Tabia mbovu kwenye nyimbo zao, au ndio mnasubiri mpaka jina la kiongozi aliepo madarakani liimbwe ndo mchukue hatua?
Mjanja M1