Nyerere alijisaliti na kuwasaliti watanzania

Jamaa ameongea ukweli mchungu nampa big up sana mwalimu alikuwa dikteta kwan mrema mwaka 95 alishinda na nyerere ndio alishinikiza anyanganywe ushindi huo kitu ambacho mpka leo ccm wanaendelea nacho pia alikuwa tuu mbaguzi mfano angalia jeshini enz zke aliwajaza tuu wakurya wenzake alafu wanamuenz km vile mtakatifu ??!!! nyerere ni nyang'au na dikteta kama gadafi
 
Kama aliogopa nchi kuangukia mikononi mwa akina mrema,akidhani ccm tu ndio inaviongozi wazuri,alijidanganya jk je????si ni pumba zaidi??siku ya leo sio kukumbuka tu mazuri aliyofanya bali pia na mabaya aliyofanya kwa kumbukumbu ya vizazi vijavyo kwamba alitumia udikteta kutawala nchi,kutumia vibaya usalama wa taifa kutisha watu na kuwafanya waoga.kutumia rasilimali za taifa kumrudisha madarakani obote ambae wala hakudumu akaondolewa.Angeweza kutoa mafunzo kwa vijana wa nchi ambazo zilikuwa bado hazijajikomboa bila kupeleka wanajeshi wetu huko,wengi walikufa huko msumbiji,namibia ,na angola mafunzo hayo yangekuwa hata yakufikia vyeo vya maafisa then wapewa silaha wakajiongoze wenyewe.Ni Raisi aliyekuwa na huruma isiyo na tija kwa kuruhusu wafanyakazi waliohujumu mashirika ya umma kuhamishwa toka sehemu moja hadi nyingine na kuendeleza wizi.
 
Mengine yote nimewaachia wengine lakini hilo la Zanzibar, mwogope Mungu kwa sababu ushindi na kutoshindwa ulikuwepo mwaka 2000 Nyerere kifa fariki - Acheni uchuro!
 
kuna press conf moja niliiona juzi j3 itv. Kuna sehem alikuwa akiongelea siasa za tanzania. Alikuwa akiisema ccm vibaya sana. Akasema kuwa chama kimezeeka na bahati mbaya kaangalia kaona hakuna chama cha upunzani chenye nguvu na mizizi. Nccr ndo ilikuwa na miaka sijui mitatu. Mzee akaona hamna kitu hapo. Bora hao waliochokwa waendelee hivyohivyo hadi hapo upinzani wa kweli utakapopatikana. Bahati mbaya hajaishi kuona haya ya leo. Kwamba ndoto yake ya kuona upinzani wa kweli imeshatimia
 
Lakini hata mrema angepata urais naamini angetupeleka kama huyu jk kwa sababu ktk wapinzani ambao hawaoni chungu ya utawala wa huyu mkwele ni Lyatonga anausifia sana utawala huu lyatonga angetuweka pabaya sana ni mnafki sana yule mchaga na nina imani kwa term hii kama angeukosa ubunge basi angekula matapishi yake kwa kurudi ccm. Nyerere nae alikua anajiona kama yeye ni mmiliki pekee wa hii nchi nina mashaka na unyerere wa kupokwa ushindi 2015 MUNGU AKUWEKE PANAPOKUSTAHILI JULIUS nashindwa kumlazimisha mungu akuweke wanapolazimisha wengi.
 
Tutabaki kumlaumu Nyerere tu, lakini tunahitaji kujiuliza tutabaki tunamlaumu mpaka lini? Je kama tunamlaumu kuwa katufikisha hapa, je sisi tunafanya jitihada gani kuparekebisha hapa tulipo au na sisi tunaendelea kufanya madudu na sisi kizazi chetu kije kitulaumu kama sisi tunavyolaumu mda huu?
 
Nyerere alijijenga zaidi binafsi na kusahau nchi na wananchi, mpaka alipoona msala wa ubeberu akala kona ili jumba bovu limdondokee mtu mwingine. Ujamaa ulikuwa unazama duniani kote na alikuwa mwoga wa bad news.
 
Pamoja na mazuri aliyoyafanya Nyerere kwa nchi hii,lakini ni yeye pia alieweka msingi mbaya sana kwa watanzania kuhsu neno "amani" na mfumo wa vyama vingi.

Watanzania wamekaririshwa neno amani pasipo kuambiwa ukweli kuwa amani ni matokeo ya kuwepo kwa hali ya haki na usawa na kamwe si vinginevyo.

Watanzania wamekariri kuwa kukosekana kwa haki na usawa si tatizo bali kukosekana kwa amani ndio tatizo.Kwa maneno mengine,mtanzania ameridhika kunyimwa haki na usawa mradi tu amani iwepo.

Watanzania wengi,tofauti na watu wa mataifa mengine,wanashindwa kutambua kuwa wanapaswa kupigania haki na usawa na katika harakati hizo halali, amani inaweza kutoweka kwani watala watatumia hata mabavu kuzima madai yao na wa kulaumiwa si mwanaharakati(wapinzani n.k) bali ni mtawala.

Ni bahati mbaya sana watanzania wanaamini adui yao ni yule anaeongoza harakati za kudai haki na usawa na mtu mwema kwao siku zote ni yule anaimba amani majukwaani huku akitenda kinyume.

Hii ndio Tanzania aliotuachia Nyerere ikiwa ni matokeo ya kuishi katika mfumo wa chama kimoja kwa miaka mingi pasipo sauti za wapinzania(wanaharakati) wanaopigania haki na usawa.

Hali hii ndio leo inawafanya watanzania wengi waone anaeitisha maandamano ya kudai haki na usawa ni mtu wa fujo na anaezima maandamano kwa kutumia nguvu za dola, ndio mwenye kulinda amani!

Suluhisho la hali hii si elimu ya uraia wala nini(chunguza hata wasomii wa nchi hii),bali ni pale kizazi cha miaka ya 60,70 na 80 kitakapotoweka katika uso wa nchi hii kwasababu hata wakizeeka bado haisaidii kwani nao wana haki ya kupiga kura.

Nyerere hivi ndio ulivyotulea watanzania na mtoto umleavyo ndivyo akuwavyo.
 
Tanzania sio nchi inayowajibika,fikiria kila mjumbe alikuwa anapewa laki 3 lakini wananchi wake kibao maskini,wajinga maana hawana elimu na uwezo wao ni mdogo sana,hawana nyumba maana nyumba zao kama za kujificha,hawapati habari.....yaani tanzania ni shida sana,Acha mjini hapa.HALI NI MBAYA.
 
Kuna wakati huwa najuta kuwa mtanzania.
 
Nyerere hivi ndio ulivyotulea watanzania na mtoto umleavyo ndio akuwavyo.

Asante naww kwakuliona hili Watu wamekarirshwa kiasi kwamba hawajionei Huruma,,,,nawaambiga watu walioko kwenye MFUMO na mawakala wao wakifanya hivyo ni sawa lkn ss utakuta huku mtaani mtu hata KULA yake niyashida lkn analeta ushabiki wakijinga,,,!! Issue km ya KATIBA sio yakuletea ushabiki wa SIMBA na YANGA katiba inahusu vizazi vyetu vijavyo,,,lkn watu waala,,,Kesho na keshokutwa mambo aliyoyashabikia yanapomgeukia kummaliza analalamika Unajua kuna wakati huwa nahis cc watu weusi km ni laana flan Manake inafikia hatua wala hatujionei huruma hata mtu akitumbia ukweli wa Hatari iliyombele yetu ndo kwanzaa tunamuona mtu huyo ni Hatar ,,,Angalia kwa mfano tunapoelekea kwenye Uchaguz mwakani Jamaa tuliokuwa tunawatukana miaka.iliyopita kuwa wamefisidi hii leo watu walewale Wanaimba mapambio mtaani kuwa wanafaakutawala,,,,,!!
 
Kama kumbukumbu zangu ni nzuri,nadhani kuna wakati fulani,mahali fulani,akihutubia, Mwalimu kwa lugha ya kiingereza aliwahi kusema atawashangaa Watanzania iwapo watanyimwa haki zao halafu wakakaa kimya.Watakuwa wajinga.Mwenye ile speech yake anaweza kuiweka humu.
 
Wapo watakaobisha lakini ukweli ndio huo!Mchonga alidumaza fikra za watanzania kwa kiwango kikubwa na bahati mbaya watawala wa sasa ni zao la mzanaki.Ndugu zangu tusidanganyane mabadiliko bado sana!
 
Asante naww kwakuliona hili Watu wamekarirshwa kiasi kwamba hawajionei Huruma,,,,nawaambiga watu walioko kwenye MFUMO na mawakala wao wakifanya hivyo ni sawa lkn ss utakuta huku mtaani mtu hata KULA yake niyashida lkn analeta ushabiki wakijinga,,,!! Issue km ya KATIBA sio yakuletea ushabiki wa SIMBA na YANGA katiba inahusu vizazi vyetu vijavyo,,,lkn watu waala,,,Kesho na keshokutwa mambo aliyoyashabikia yanapomgeukia kummaliza analalamika Unajua kuna wakati huwa nahis cc watu weusi km ni laana flan Manake inafikia hatua wala hatujionei huruma hata mtu akitumbia ukweli wa Hatari iliyombele yetu ndo kwanzaa tunamuona mtu huyo ni Hatar ,,,Angalia kwa mfano tunapoelekea kwenye Uchaguz mwakani Jamaa tuliokuwa tunawatukana miaka.iliyopita kuwa wamefisidi hii leo watu walewale Wanaimba mapambio mtaani kuwa wanafaakutawala,,,,,!!

Ngozi nyeusi ni laana ndugu yangu.Hatujitambui kabisa.

Huko Hong kong wenzute wameshikama kupinga uzalimu wa China.Waanaandamana na hata polisi wa huko si wa hovyo kama hawa wetu ambao wengine wanaishi kwenye kambi za nyumba za mabati ila hawajitambui bali wanaona sifa kupiga waandamanaji.
 
Huo ndo ukweli, eti amani na utulivu huku watanzania wakinyimwa haki zao. Watanzania itawachukua muda mrefu kutoka usingizini.
 
Tanzania sio nchi inayowajibika,fikiria kila mjumbe alikuwa anapewa laki 3 lakini wananchi wake kibao maskini,wajinga maana hawana elimu na uwezo wao ni mdogo sana,hawana nyumba maana nyumba zao kama za kujificha,hawapati habari.....yaani tanzania ni shida sana,Acha mjini hapa.HALI NI MBAYA.

Pia twamshukuru kwa hilo la kuweka misingi ya amani ingawaje kwenye jengo dhiki na dhulma, Kwasemwa ati usiposhukuru kwa kidogo pia kikubwa huwezi shukuru aidha.
 
Back
Top Bottom