Nyangwine bomu

notmar

Member
Jun 4, 2011
81
1
wana tarime wamekosea sana kumchagua nyangwine kuwa mbunge wao.nimemsikiliza akichangia hotuba jioni hii....ni mtu ambaye hawezi kujenga hoja mtu wa kuchekacheka hata ktk mambo ambayo ni serious km mauaji ya nyamongo............amejikanyaga kwa kutaja mambo ya ajabu kama kukata watu mapanga mpaka lukuvi (ambaye wanatoka chama kimoja)ameomba afute kauli...........this is nyangwine.
 
Wakuu nimesikiliza mchango wa mbunge wa Tarime Nyangwine nyambari nikagundua ana mapungufu yafuatayo:-
1.Hajiamini anaongea kwa kuchekacheka.
2.Anaongea kama yupo kwenye vijiwe vya kampeni Nyamono.
3.Anapoongea hatulii kwenye kiti anakuwa kama anawashwa.

My take:
Kwa mnaomfahamu naomba mnipe mnachokifahamu kuhusu huyu mheshimiwa.
 
unaona sasa....na wewe huna tofauti na huyo nyangwine:......

ameongea nini
juu ya nini
wapi
lini
na kwa nini............
 
Wakuu nimesikiliza mchango wa mbunge wa Tarime Nyangwine nyambari nikagundua ana mapungufu yafuatayo:- 1.Hajiamini anaongea kwa kuchekacheka.2.Anaongea kama yupo kwenye vijiwe vya kampeni Nyamono. 3.Anapoongea hatulii kwenye kiti anakuwa kama anawashwa.My take:Kwa mnaomfahamu naomba mnipe mnachokifahamu kuhusu huyu mheshimiwa.
we ndo sio mzima. Uko peponi sio?
 
Hata mimi nimemsikia. Ni tofauti na wabunge wa tarime waliopita. Nafasi hakuitumia kabisa kuwatetea wanatarime vizuri mbele ya serikali. Labda ssb yupo chama cha magamba.
 
Hiyo ni dhahiri kabisa huyo bwana hana uwezo wa kuteta nadhani kiswahili kinampiga chenga japo nimeona ameandika vitabu vingi vya lugha ya taifa,tarime mnapotoshwa,inamlazimu abadilike sana labda bunge lijalo atakua na kuacha utoto.
 
Ni mbunge wangu kwa maana ya ndio kwetu,ingawa sasa sipo huku.Kilichomfanya Nyambari awe mbunge sio kujiamini,ufundi wa kuongea au chaguo la wanatarime!Bali ni wapinzani kutosimamisha mgombea mmoja?Chadema -Mwita,Cuf-Mwera,Nccr-Mdogo wake Chacha Wangwe?Unategemea nani angeshida?Ukijumlisha kura za hao wapinzani waliishida Ccm.Kwa mtindo huo tutaendelea kupata wabunge dizaini ya Nyambari!
 
si tu hawezi bali hastahili kwa nafasi hiyo.
Kama kiswahili ni tatizo aongee kiingereza.
 
sijui walitumia vigezo gani katika kumchagua huyu mtu, hana hata uwezo wa kujenga hoja, utadhan ni mtoto mdogo, kwa kweli CCM mlikosea sana kumpa nafasi huyu mtu anaitwa nyangwine, hana uwezo kabisa wa kupambanua mambo. ni kuchekacheka tu. kwa ujumla watu wa tarime mmechagua bomu na si mbunge
 
Nimemsikiliza. Kwa kweli huyu jamaa nikimsikia tena anapewa nafasi ya kuzungumza, nabadili chaneli, haongei chochote bungeni zaidi ya kutamba kwamba yeye ndo mbunge wa nyamongo na cdm wanamuingilia kwenye jimbo lake. Anaongea kama yuko mtaani, hana maandalizi, kwa kifupi anaboa kumsikiliza. Ni wazi anajua hakushinda kwenye uchaguzi ndo maana hajiamini.
 
nadhani watu tunatofautiana sana katika kutafsiri mambo. kaongea kipi kibaya? kwani si kweli kuwa wana tarime wamechoshwa? kwani si kweli kuwa sasa wako tayari kwa lolote? kwa taarifa yenu. hamjui tu kumsoma mtu mwenye furaha, huzuni, hasira n.k. muda ule jamaa alikuwa na machungu sana na wala msione alikuwa anacheka. mimi si wa Tarime wala mwana ccm bali namuunga mkono. si mmeona hata Ndugai kampotezea Lukuvi?

kwa taarifa yenu, ujumbe not only sent, but delivered. na wasitekeleze aliyosema Nyangwine waone. kama mnataka kujua kuwa alikuwa sahihi nendeni Tarime mkawaulize wahanga juu ya alichoongea leo kama hamjakaa kimya.
 
Hivi we mzima kweli?? Mbunge anapoongea kuchangia hoja unadhani anakuwa vichochoroni?? Hoja hapa ni style ya kuongea na sio points alizoongea

Hawa jamaa ambao wanakushangaa siwaelewi kwani hawakuwa wanaangalia Tv. Huyu Mbunge wa Tarime hata mimi ananishangaza kwani anajichekesha ovyo kana kwamba kuna mtu pembeni anamtekenywa au anamchekesha. Sijaona kama yuko serious na anachoongea kwani lazima uso uonyeshe expression tofauti tofauti unaposisitiza mambo ya msingi jambo ambalo Nyangwine hakuonyesha bali ku smile kuanzia mwanzo hadi mwisho.
 
Nyambari Nyangwine ni Nyambari Nyangwine kweli kweli na wala siyo mbunge wa Tarime. Watu wa Tarime siyo kama Nyambari Nyangwine!
Narudia tena, Nyambari Nyangwine ni Nyambari Nyangwine na wala siyo mbunge wa Tarime ni kituko tupu!
 
Chadema wenyewe walichemka kupeleka mtu asiekubalika...yule mbunge aliekuepo anafaa sana na ndie alikua mshindi,,wa kulaumiwa ni chadema sio watu wa Tarime..huyu ni kimeo sio mbng
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom