Mommadou Keita
JF-Expert Member
- Oct 8, 2013
- 230
- 237
Wakati alipokuwa akiumwa, Mtangazaji mahiri hapa nchini, Julius Nyaisangah hakuna hata mwanahabari mmoja aliyekuwa akijali afya yake, wanahabari wa Dar es Salaam hawakuona umuhimu wa kuchangishana na kumhudumia mwenzao lakini alipofariki dunia waliamua kuuteka msiba na kuuleta Dar es es Salaam. Wakatoa ahadi ya kuupeleka kwa ndege mwili wake hadi kijiji kwake alikozaliwa huko Mara.
Hata hivyo, hawakutimiza ahadi hiyo ya kumpeleka kwa ndege baada ya kutafuta umaarufu pale Leaders Club na kisha mwili ukasafirishwa kwa gari hadi huko kwao. Kwa nini basi, waliamua kuuleta mwili Dar? Je, kulikuwa na shinikizo la nani?
Pili, kwa nini waliidharau kamati ya mazishi ya Morogoro kwa kubadilisha jeneza la kumbebea mwili wake na kumweka katika jeneza lingine? Kama kweli walikuwa na uchungu na Julius kwanini hawakujikusanya na kwenda Morogoro kuungana na kamati ya mazishi ya kule na kuangalia upungufu uliopo na kuukamilisha.
Naamini kabisa kwamba Abood alikuwa amejiandaa vyema kuusafirisha mwili wa Nyaisangah hadi kijijini kwake na kila kitu kilikuwa kimekamilika, je kamati iliyoundwa Dar ilikuwa ya kisiasa au kutaka umaarufu.
Ikumbukwe kuwa Nyaisangah alikuwa amefanya kazi Redio Tanzania na Redio One na kikatokea cha kutokea na kuacha kazi, alikuwa na marafiki wengi ambao hawakuweza kumsadia na kumfanya kuwa mmoja wa watangazaji ambao wengeweza kwenda kutangaza katika vyombo vya kimataifa ( vye nje) lakini marafiki hao hawakuwa na msaada wowote kwake, baada ya kufariki ndiyo kila mtu anajidai kuwa ndugu, rafiki na wa kumuonea huruma.
Watz, tuache uzandiki huu wa kuithamani maiti na kutomjali mtu wakati akiwa anaumwa. Binafsi nisingependa kuona hiki kitu kikijirudia kwa mtu mwingine.