Nyaisangah hakutendewa haki hata kidogo

Jifunze jambo moja!!!!

Ukiwa hai imarisha sana familia yako na kuijengea misingi imara ya kusimamia mambo yao bila kushirikisha watu wa mbali na vikundi shirikishi!!!!

Rafiki zako ni rafiki zako wewe once haupo hawana dhamana ya kusimamia uliyoyaacha kama mlikutana.bar ili mnywe na wewe ushakufa na huwezi kunywa you are good for nothing!!!!!Mke au mume ndio mpango mzima ukitoka hapo ni wadogo au wakubwa zako na spouse kwa umoja,hao marafiki ni kama wataamua kushiriki hawafungwi popote!!!!!

Hivi umefiwa wewe wanakuja marafiki wa marehemu ndugu yako na kukuambia tunaomba sijui tupeleke mwili sabasaba sijui heshima.imefanyaje na unakubali????!!!!!! THIS SIGNIFIES NOTHING BUT A WEAK FAMILY!!!!!!!

TUKIWA HAI TUJENGE FAMILIA ZETU JAMANI

Hakika umeongea kila kitu.
 
Nimefurahi kukubali kwamba Uncle J alikuwa na uwezo mkubwa wa kuweza kwenda nje, je, umejiuliza kwa nini hakupata nafasi hiyo hadi kwenda kufia Morogoro badala ya Uingereza ua Ujerumani? Kuna wengi hawakuwa na uwezo wa kufanya kazi kama Uncle J lakini walibebwa na kupewa fursa hizo. Naamini kuwa Uncle J alikuwa na marafiki wengi na wengine wanafanya kazi nje ya nchi,jiulize nani aliyekwenda hata kumpa ushauri wa mawazo kwamba asiende Morogoro na kumshauri kwenda nje?
Na wewe acha uzandiki, haya ulitakiwa uyaseme kabla hajafa. Wewe alivokuwa hai ulimpa msaada gani?
 
Familia nayo mpaka iwe na uwezo wa kuelewa mambo, unajua uncle J was blessed, inawezekana waliomzunguka uwezo na blessings hizo hawakuwa nazo. sio kosa lake kazi kapiga sasa amepumzika.
 
HIVI WANA JF KUWEKA MWILI WA MAREHEMU LEADERS CLUB IMEKUA FASHION?HALAFU INAKUAJE MTU KAFARIKI MOROGORO BADALA YA KUUPELEKA KWAO MBEYA AU BUKOBA UNALETWA DAR KWANZA huo ni ujinga na sifa zisizo na tija
 
Ndugu yangu jenga maisha yako kwa mkono wako. Usiwekematumaini yako kwa misaada ya ndugu na marafiki. Ni dhambi kubwa kuwalaumu ndugu na marafiki kwa umasikini ulonao ilhali nguvu ulikuwa nazo na kazi unafanya. "mtegemea cha ndugu hufa hali masikini"
 
Wabongo wengine acheni kutegemea jamii kila kitu, ujamaa umetubweteza.Kila kitu kutegemea kuchangiwa noma.

Kuna haja ya kupanga mambo vizuri, kuandika wosia,na kupanga jinsi ya kuzikwa mapema.

Halafu sio lazima kuzikwa kijijini kwenu hata kama uwezo wa kusafirisha mwili watu hawana.
 
Nimefurahi kukubali kwamba Uncle J alikuwa na uwezo mkubwa wa kuweza kwenda nje, je, umejiuliza kwa nini hakupata nafasi hiyo hadi kwenda kufia Morogoro badala ya Uingereza ua Ujerumani? Kuna wengi hawakuwa na uwezo wa kufanya kazi kama Uncle J lakini walibebwa na kupewa fursa hizo. Naamini kuwa Uncle J alikuwa na marafiki wengi na wengine wanafanya kazi nje ya nchi,jiulize nani aliyekwenda hata kumpa ushauri wa mawazo kwamba asiende Morogoro na kumshauri kwenda nje?
Kazi ya utangazaji, zaidi ya kuwa na kipaji na sauti nzuri, kuna areas of competence!, competence ya Uncle J. ni kwenye vipindi vya burudani, hakuwa mtu wa hard news na wala sio repoter, mahitaji ya redio za nje ni mtu anayeweza ku play multi competence. mara baada ya kuondoka Radio One, aliripotia Sauti ya Ujerumani, briefly, kwa vile yeye hakuwa radio reporter bali presenter, nadhani kazi ilimuwia ngumu!.

RTD pia imelemaza vibaya, kuna watangazaji wengi ni presenters tuu na sio producers, hicho wanachosoma, wameandikiwa!, waambie waambie waandike wenyewe utashangaa!. Redio za kule wanataka ufanye reseach mwenyewe, uandike mwenyewe, ndipo u present mwenyewe!, sio watangazaji wengi wenye uwezo huo ndio maana tunashuhudia ni wachache tuu ndio wamefanikiwa!.
Pasco.
 
Jifunze jambo moja!!!!

Ukiwa hai imarisha sana familia yako na kuijengea misingi imara ya kusimamia mambo yao bila kushirikisha watu wa mbali na vikundi shirikishi!!!!

Rafiki zako ni rafiki zako wewe once haupo hawana dhamana ya kusimamia uliyoyaacha kama mlikutana.bar ili mnywe na wewe ushakufa na huwezi kunywa you are good for nothing!!!!!Mke au mume ndio mpango mzima ukitoka hapo ni wadogo au wakubwa zako na spouse kwa umoja,hao marafiki ni kama wataamua kushiriki hawafungwi popote!!!!!

Hivi umefiwa wewe wanakuja marafiki wa marehemu ndugu yako na kukuambia tunaomba sijui tupeleke mwili sabasaba sijui heshima.imefanyaje na unakubali????!!!!!! THIS SIGNIFIES NOTHING BUT A WEAK FAMILY!!!!!!!

TUKIWA HAI TUJENGE FAMILIA ZETU JAMANI

asanteeee,,asante sana OLESAIDIMU
 
Last edited by a moderator:
Wabongo wengine acheni kutegemea jamii kila kitu, ujamaa umetubweteza.Kila kitu kutegemea kuchangiwa noma.

Kuna haja ya kupanga mambo vizuri, kuandika wosia,na kupanga jinsi ya kuzikwa mapema.

Halafu sio lazima kuzikwa kijijini kwenu hata kama uwezo wa kusafirisha mwili watu hawana.

ukweli mchungu
 
Kibaya zaidi wakawadanganya wafiwa waliokuwa wamebaki Morogoro ambao ilikuwa wasafiri na msiba kwenda Musoma, kuwa walishawaandalia usafiri wa kutangulia Musoma wakati mwili ukija kuagwa dar. Matokeo yake waombolezaji wale wakatelekezwa pasipo kujua wafanyeje, ikabidi wausubiri mwili utoke dar ndipo waanze safari ya pamoja kuelekea Musoma. Hili pia halikupendeza!
Nadhani kulitokea miss communication mahali!. Abood alitoa gari la kuubeba mwili na basi la waombolezaji.
Waandishi walikuwa waupeleke Mwili Mwanza kwa ndege, then ikakutikana hakuna logistical support from Mwanza to Musoma, Mwanza Press Club walikuwa kimya!.

Ikaja hoja from Kijijini kwake kuwa Mwili usubirishwe for one extra day for familiy reasons. Then mawasiliano yakafanya usiku ule ule mwili ulipoingia Dar kuwa ile gari iliyotolewa na Abood itangulie kijijini kwake kwenda kuandaa logistics za huko, mwili ukafanyiwa proper embalming na kusafirishwa kwa gari, ili ufike the day after!. Hili la waombolezaji wa Morogoro kutelekezwa its news for me!. Gari alizotoa Abood zilienda wapi?.

Jaman 2kimjadili marehem haisaidii,betr 2jtazme 2liobaki kwan hakuna mkamilifu
 
Mkuu mi kimya sana Muhimu ni kumuomba Mwenyezi Mungu Raha ya Milele ampe Uncle J na mwanga wa Milele amuangazie apumzike kwa Amani Amen.
 
Wakati alipokuwa akiumwa, Mtangazaji mahiri hapa nchini, Julius Nyaisangah hakuna hata mwanahabari mmoja aliyekuwa akijali afya yake, wanahabari wa Dar es Salaam hawakuona umuhimu wa kuchangishana na kumhudumia mwenzao lakini alipofariki dunia waliamua kuuteka msiba na kuuleta Dar es es Salaam. Wakatoa ahadi ya kuupeleka kwa ndege mwili wake hadi kijiji kwake alikozaliwa huko Mara.

Hata hivyo, hawakutimiza ahadi hiyo ya kumpeleka kwa ndege baada ya kutafuta umaarufu pale Leaders Club na kisha mwili ukasafirishwa kwa gari hadi huko kwao. Kwa nini basi, waliamua kuuleta mwili Dar? Je, kulikuwa na shinikizo la nani?

Pili, kwa nini waliidharau kamati ya mazishi ya Morogoro kwa kubadilisha jeneza la kumbebea mwili wake na kumweka katika jeneza lingine? Kama kweli walikuwa na uchungu na Julius kwanini hawakujikusanya na kwenda Morogoro kuungana na kamati ya mazishi ya kule na kuangalia upungufu uliopo na kuukamilisha.

Naamini kabisa kwamba Abood alikuwa amejiandaa vyema kuusafirisha mwili wa Nyaisangah hadi kijijini kwake na kila kitu kilikuwa kimekamilika, je kamati iliyoundwa Dar ilikuwa ya kisiasa au kutaka umaarufu.

Ikumbukwe kuwa Nyaisangah alikuwa amefanya kazi Redio Tanzania na Redio One na kikatokea cha kutokea na kuacha kazi, alikuwa na marafiki wengi ambao hawakuweza kumsadia na kumfanya kuwa mmoja wa watangazaji ambao wengeweza kwenda kutangaza katika vyombo vya kimataifa ( vye nje) lakini marafiki hao hawakuwa na msaada wowote kwake, baada ya kufariki ndiyo kila mtu anajidai kuwa ndugu, rafiki na wa kumuonea huruma.

Watz, tuache uzandiki huu wa kuithamani maiti na kutomjali mtu wakati akiwa anaumwa. Binafsi nisingependa kuona hiki kitu kikijirudia kwa mtu mwingine.
eti aboubakar liongo anajifanya msemaji wa familia...mnafiki mkubwa toka amefukuzwa DW radio hajawahi hata kukanyaga Morogoro...
 
Mkuu umenena vizuri sanaaa ufike mahali watz tuache unafki
 
wanafiki ni wengi mno na hilo umejionea kwa kuwa huyo mtu maarufu lakini kwa sisi wagema ulimbo ndio tunafanyiwa sana hivi na hawa watu wanajifanya wana fedha.Wakati wa matatizo wala huwa hawajitokezi wakisikia fulani kafa ndio hujitokeza na kusema gharama zote za msiba ni juu yake na hataki mchango wa mtu yoyote kwa kuwa marehemu ni mtu wake wa karibu.
Nalog off
 
Back
Top Bottom