NSSF si shamba la bibi tena

Nimesoma maandiko mengi kuhusu uongozi wa NSSF uliopo sasa chini ya Bwana Erio ambaye wengine wanalibananga jina lake kwa kumgeuza mchaga na kumwita Urio. Usifikiri kuwa wanakosea, la hasha, wanafanya makusudi ili waonekane kuwa hawalijui jina lake. Wengine wao ni watu wake wa karibu ambao ukitajiwa majina yao hutoamini jinsi wanavyomzunguuka. UTOVU WA FADHILA

Kwa bahati nzuri mimi nimekuwepo katika shirika tangu enzi za mheshimiwa Mustafa Mkulo wakati huo NSSF ilikuwa NSSF kweli, iliyojengwa katika misingi ta utumishi wa umma, si kidini wala kikabila. Kwa kifupi huyo bwana alikuwa kama ndiye mwanzilishi wa shirika, na kwa hakika bila kupepesa macho, ndiye aliyefanya shirika lionekane.

Baada yake alifuata mheshimiwa Ramadhani Dau ambaye naye alijitahidi kuzuungusha gurudumu aliloachiwa. Lakini baadaye aliiingia katika ubaguzi wa kutaka kulifanya shirika hili la Umma kuwa taasisi ya kidini ambayo Corridor zake zote zilibadilika ghafla na kuwa sehemu za ibada. Mambo haya yalifanyika bila mheshimiwa Dau kuyakemea, kwa maana hiyo inaonekana alihusika kuanzisha hali hiyo. Kwa kifupi shirika lilikuwa kama Kuwait.

Kwa kipindi chake mambo mengi yalifanyika hadi kulipeleka shirika kwenye hali ya ukata. Tulishuhudia wakati Fulani shirika likikopa fedha benki kwa ajili ya kulipia mishahara ya watwana sie. Miradi ya ovyo ovyo iliyozingatia maslahi binafsi ndipo ilipoanzishwa, na kila aliyekuwa na fursa alipata mahali pa kuvuna kwa ajili yake na familia yake. Kuanzia Bosi mwenyewe, hadi mhudumu wa ofisi.

Hapo ndio ilipokuja Dege Eco Village, manunuzi ya viwanja na mashamba yasiyohitajika, Eka moja ya ardhi ilinunuliwa hadi kwa shilingi 800,000,000/-; kiwanja kimoja pale Dodoma ambacho kwa taarifa za kiuchunguzi kilikuwa na thamani kati ya shilingi 200,000,000/- na 400,000,000/- kilinunuliwa na shirika kwa shilingi bilioni 5.

Taarifa zote hizi zinafahamika na zipo kwenye ripoti ya CAG. Kuna bwana mmoja anayeitwa Musiba, mwanaharakati huru ameshasema mara nyingi juu ya ubadhirifu uliokuwepo, katika awamu hii. Akiuizwa leo atatiririka hadi utapatwa na hasira.

Baada ya hapo ilifuata awamu ya Profesa Mbobezi wa uchumi, G. Kahyarara ambaye hakudumu sana. Muulize atakueleza ubadhirifu alioukuta japokuwa naye aliangukia katika mkumbo ya upigaji uliojificha ndani ya uzalendo. Huyu alikuwa mwenye porojo nyingi zilizojaa nadharia za kiuchumi zisizotekelezeka.

Baada ya Profesa kulishindwa dude hili la NSSF, ndipo Mheshimiwa Rais Dokta John Pombe Joseph Magufuli akamteua bwana Erio ambaye hana historia ya wizi wala ubadhirifu ambaye kwa kweli amepigwa vita kubwa.

Alipoingia NSSF huyu bwana, Mbobezi wa taaluma ya Sheria alikuja kwa staili utekelezaji wa kile mheshimiwa Raisi alichokuwa akitaka, yaani kupambana na ubadhirifu, wizi na ufujaji wa mali ya umma. Alibana mianya yote ambayo wengine tulikuwa tumeizoea ya kupatia “riziki”.

Kwa kweli mwanzoni hata mimi nilimchukia kwa kuwa alisababisha moto ukawaka kwenye mifuko yangu. Lakini baadaye nikatafakari kitu uzima, nikakubali hali halisi kuwa maisha tuliyokuwa tukiishi hayakuwa sahihi. Moto kwenye mifuko haujaisha lakini naona ni bora niangalie njia nyingine za halali za kupatia kipato.

Kuna mtwana mmoja alishaniambia kuwa wanasheria wanafuata sheria kwenye kutawala, hili nimelishuhudia maana kila kitu kilichokuwa hakiruhusiwi kwenye sheria kilisitishwa, kwa wafanyakzi wengi hili halikuwa jambo jema walitamani yale mazoea yao yaachwe kama yalivyokuwa jambo ambalo kwa mwanasheria lingekuwa dhambi.

Kumbuka wale watu waliokuwa wakimpigia kelele mheshimiwa Rais kuwa aachie hela kwa kuwa maisha yalikuwa magumu, na yeye akawa akiwajibu kuwa watu wafanye kazi pesa watazipata.

Kwa tathmini yangu ya haraka huyu bwana Erio atapigwa vita kali hata afanyeje, bwana Erio, ile miradi mnayokamilisha kule Dungu, kijichi na Tuangoma inakuwinda kama mzimu. Kuna watu walitamani ushindwe hata kukamilisha hiyo sehemu ndogo. Walitamani uwatafute wale wakandarasi walioianza hiyo miradi ili waikamilishe na upigaji wake. Kama ulikuwa hujui, nakupa taarifa sasa.

Unaonekana kama umezuia ulaji wa watu kwenye hizo sehemu. Hujuma hizi hazijaishia kwa hao tu, hata wafanyakazi wengine wanakuhujumu, na wengine wanatumiwa na watu waliokuwepo kwenye tawala zilizopita. Waangalie sana hao. Kwa kuwa niko nao kazini kila siku, ukitaka hata majina nitakutajia.

Kwa mfano angalia yule kiongozi wa USA River, anatumiwa na watu wa nje kukuhujumu na ushahidi upo, na Mameneja wengine wa mikoa iliyopo Dar es salaam. Wengine nitaendelea kukutajia hadi uwajue wote. Wakitaka nisiwataje waache hujuma. Kulihujumu shirika ni kuihujumu serikali na kupinga juhudi za Raisi za kukuza uchumi wa nchi na kutatua kero za wanyonge.

Mradi wa Dege ni mzimu mwingine utakaokukosesha raha kwa kuwa matarajio ya walaji wengi umeyakatiza kwa kukataa kuendelea kutoa fedha za kumalizia mradi huo. Komaaa wala usirudi nyuma, hilo Dege ni Bomu la Atomiki, mradi hauna tija, ubadhirifu umejaa. Naamini hata Mheshimiwa Raisi hakubaliani na mradi huo.

Bwana mmoja akaandika katika makala yake eti kwa kuja Erio NSSF imedorora. Mimi nilikuwepo tangu enzi na enzi, ambaye nimeona awamu zote nasema NSSF haijadorora. Mdororo utakuwa umetokea kwenye mifuko ya huyo jamaa na mkewe. Maendeleo aliyoyafanya bwana Erio kwa muda mfupi yanaonekana dhahiri. Hata kule PPF alikotoka aliacha Mfuko ukiwa na hali nzuri sana na ushahidi upo. Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni.

Kwa ushahidi niliona baada ya uchunguzi wangu ni kuwa

1, Mwezi Julai 2018 wakati Mifuko ilipokuwa inaunganishwa ukaguzi wa wataalamu waliofunga mahesabu ya PPF walitanabahisha kuwa thamani ya Mfuko wa PPF ilikuwa ni Shilingi trilioni 3.1 wakati shirika la NSSF lilikuwa na thamani ya Shilingi trilioni 3.25.

Thamani ya Mfuko wa PPF ilitengenezwa na wafanyakazi 400 wakati ile ya NSSF ilitengenezwa na watumishi 1400. Je, kwa mwenye akili timamu ni Mfuko upi hapo ulikuwa ukifanya vizuri ? Hebu watu waache hekaya za Abunuwasi hapa.

2. Wakati huo return on investment ya PPF ilikuwa asilimia 22 wakati NSSF ilikuwa - 3%;

3. Fedha (liquid cash) zilizokuwepo PPF wakati huo zilikuwa jumla ya shilingi trilioni 1.5 trilioni pamoja na fixed deposits and government bonds.

Ikumbukwe wakati huo PPF ilikuwa ikilipa mafao na madeni yake bila matatizo yoyote. Ukija upande wa shirika letu, pamoja na mbwembwe zote tulizokuwa tukipiga shirika (NSSF) lilikuwa na Shilingi bilioni 350 wakati deni la mafao kwa zaidi ya miaka miwili (2) lilikuwa shilingi bilioni 109.

4. Kwenye TEHAMA, PPF ilikuwa ikifanya shughuli zake kwa kutumia mifumo ya kielektroniki tangu mwaka 2008 wakati NSSF ilikuwa ikiendesha mifumo yake manually kwa 80%. Kabla ya bwana Erio kuletwa, Shirika letu la NSSF lilishatumia shilingi bilioni 12 kuweka mifumo ya kielektroniki bila mafanikio. Aibu gani hii.

Kwa miaka 13 ambayo bwana Erio aliiongoza PPF hakujawahi kuwa na ubadhirifu wowote, na hata data zinazosemekana kupikwa na bwana Erio haikuwa kweli. CAG ambaye ndiye mtoa taarifa sahihi za Mfuko hakuwahi kuandika hoja yoyote ya aina hiyo iliyowahi kutolewa.

Shirika la NSSF wakati wa Profesa Kahyarara ndilo liliwahi kutoa taarida kuwa wanachma wa NSSF walikua milioni moja (1,000,000) wakati Mheshimiwa Rais alisema dhahiri katika kikao alichokiitisha Ikulu tarehe 28/12/2018 kuwa idadi kamili ilikuwa ya wanachama wa NSSF ilikuwa 448,000.

Pamoja na kwamba kiupinzani mimi ningeitetea NSSF, lakini msema kweli ni mpenzi wa Mungu. Data za NSSF ndizo zilikuwa za kuchemshwa.

Sasa ieleweke wazi kuwa kinachosumbua hapa kwetu kwa sasa ni njaa na ulafi. Bwana Erio anaelekea kukomesha kabisa ubadhirifu na wizi. Sasa inashangaza kumsikia mtu akisema eti nyie Menejimenti yenu (Mr. Erio na wenzako) eti mjifunze kutoka kwa waliotangulia. Mimi nawashauri muupuuze huo ushauri, hakuna cha kujifunza kwa waliopita. Mkikubali huo ushauri hata mimi nitawashangaa. Au mko tayari:-

5. Kujifunza kununua kiwanja cha milioni 400 kwa bilioni 5 kama walivyofanya wenzenu?

6. Kununua kiwanja baharini, Kunduchi Beach

7. Kuanzisha mradi kama Dege kwa kushirikiana na wahujumu uchumi?

8. Kufanya kazi ya siku mbili kwa Perdiem za mwezi mzima

9. Kuifanya taasisi kuwa ya kidini?

10. Kujifunza na mengine mengi ambayo nitayataja kama wendawazimu wengine wataibuka kuwatetea hao waliopita
Tena jambo lingine la utovu wa adabu ni lile la kuikosea taasisi ya Usalama wa Taifa kwa kudai imewekwa kwenye payroll na bwana Erio. Hii ni dharau kubwa sana kwa Taasisi hiyo.

Kuna wakati Baba wa Taifa aliwahi kumfukuza Askofu mmoja ambaye alidai kuwa ameiweka Serikali ya Tanzania Mfukoni. Hivi leo mtu asiye na woga anaweza kusema maneno yanayofanana na hayo ? Tena kwa Taasisi nyeti kama hiyo? Wahusika kazi kwenu.

Kwa Faida ya ninyi msiojua ukweli. Nimepenya mpaka kwenye taarifa sahihi za Shirika. Acha niwamegee hizi chache ambazo anayetaka anaweza kuthibitisha.

11. Pensheni ya wastaafu inalipwa tarehe 25 ya kila mwezi na inalipwa moja kwa moja kwenye akaunti za wastaafu. Hatua hii imesaidia kuokoa shilingi bilioni 1.3 kwa mwaka ambazo zilikuwa zikilipwa kama kamisheni kwa Post-Giro.

12. kwa mwaka wa fedha 2018/2019 michango ya wanachama imeongezeka kufikia shilingi bilioni 872 kutoka shilingi bilioni 690 mwaka wa fedha 2017/2018, ongezeko hili linatokana na matumizi ya mifumo ya kieletroniki ya fedha ikiwa ni pamoja na GePG na Internet Banking pamoja na uadilifu katika kufuatilia waajiri na Usimamizi madhubuti kwa watumishi, pia kuanzisha utaratibu wa billing, kuboresha ukaguzi kwa waajiri kwa kushirikiana na Taasisi zingine za Serikali kama TRA, WCF, OSHA, Idara ya Kazi, Wizara ya Mambo ya Ndani, na NIDA.

13. Nimethibitisha kuwa mapato yatokanayo na uwekezaji yameongezeka hadi kufikia shilingi bilioni 148 2018/2019 kutoka shilingi bilioni 131 mwaka 2017/2018.

Mapato ya daraja la Kigamboni yaliongezeka kutoka wastani wa shilingi bilioni 680 mwaka 2017/2018 mpaka wastani wa shilingi bilioni 950 mwaka 2018/2019.

14. Gharama za Uendeshaji kwa mwaka 2017/2018 zilikuwa asilimia 18% ambapo kwa sasa imeshuka mpaka 10% ambayo ndiyo matakwa ya miongozo ya kisekta.

15. Katika mwaka wa fedha 2017/2018 NSSF ilikuwa na malimbikizo ya mafao kwa wanachama 16,119 yenye thamani ya shilingi bilioni 109 wakati katika mwaka wa fedha 2018/2019 Shirika lililipa madai yenye thamani ya jumla ya shilingi bilioni 409 ikijumuisha malimbikizo ya 2017/18.

16. Thamani ya shirika imeongezeka hadi kufikia shilingi trilioni 3.72 kwa mwaka wa fedha 2018/2019 kutoka shilingi trilioni 3.25 trilioni kwa mwaka wa fedha 2017/2018. Hili ni ongezeko la shilingi bilioni 472 kwa kipindi cha mwaka mmoja.

17. Idadi ya wanachama imeongezeka kutoka 448,000 iliyokuwepo Disemba 2018 hadi kufikia 637,422 Desemba 2019.

Shirika pia limeokoa shilingi bilioni 1.5 kwenye ununuzi na matumizi ya server ambazo server zilizokuwa zinunuliwe kabla ya Erio kuingia NSSF zingegharimu shilingi bilioni 1.7 baada ya kuikata hiyo ruti server zikanunuliwa kwa shilingi milioni 160.

Kwa sasa uandikishaji wa wanachama unafanyika kwa kutumia kitambulisho cha Taifa ilikupata taarifa sahihi za wanachama kwa kutumia mfumo wa NIDA. Hapo shirika limeokoa shilingi milioni 200 Million kwa mwaka zilizokuwa zikilipwa kwa ajili ya mfumo uliokuwa ukitumika kuhakiki taarifa za wanachama kwa kutumia vidole. Mfumo huu pia umesaidia kupunguza matumizi kwa Kiasi cha shilingi bilioni 1.12.

Kwa mafanikio haya, bwana Erio hata ukihamisha wafanyakazi wote waliokuwa PPF ukawaleta huku hata mimi ningekuunga mkono. Hata hivyo, kwa hesabu zangu za kihenga NSSF ina Ofisi za Mikoa 29, kati ya hizo Ofisi za Mikoa 26 zinaongozwa na mameneja waliokuwa ndani ya NSSF. Ni mameneja wa Mikoa ya Arusha na Songwe pekee ndio wametoka PPF na yule wa Mkoa wa Morogoro amnbaye awali alikuwa wa LAPF.

Kwa leo nimetoa uzoefu wangu wa miaka kadhaa ya kuwepo kwangu kwenye shirika tangu enzi za Mr. Mkulo hadi haya ninayoyashuhudia leo. Acha tu niseme kuwa Mheshimiwa Rais John Pombe Joseph Magufuli unawakilishwa vema na bwana Erio.

Ule ubadhirifu uliokuwa unausikia ukifanyika NSSF unakaribia kuwa historia. Mteule wako akichanganywa na wateule wengine wa wizarani wanapigwa vita kwa sababu ya utekelezaji wa kuipeleka Tanzania katia hatua nyingine. Watoto wa mjini wanaita next level. Ukweli ni dhahiri kila mwenye macho anaona.

Pamoja na ukweli kwamba marekebisho ya shirika yameniletea mdororo mfukoni mwangu, na mto wa ugumu wa maisha unaniwakia sitaacha kusema ukweli kwa kuwa ucha Mungu wangu utakuwa na walakini kama nitasema uongo kwa sababu ya njaa.

Baadhi ya viongozi waliopita wa shirika, na baadhi ya wafanyakazi walilifanya shirika (NSSF) kuwa shamba la bibi lakini leo NSSF SIO SHAMBA LA BIBI TENA.

Wakandarasi na madalali wa upigaji fedha wote walikuwa wakichuma NSSF, hao ndio maadui wanaokuzunguuka.

Mungu atakupigania
Wakati mwingine mtu anafukuza mwizi si kwa sababu ni mwema sana bali anataka aibe yeye.
 
NSSF Kilimanjaro wamejenga jengo kubwa na zuri Cha ajabu like jengo nafkir linakaribia 10years na bado halijaa Cha ajabu NSSF Kilimanjaro wamepanga na wanalipa Kodi ya pango ilhali wanajengo zuri tuu nalakisasa na bado halijaa mpaka leo wanahangaika kutafuta wapangaji
 
Huwezi kufuta ukweli kwa kujitetea kwa hoja za kijinga, mjadala ulioanzishwa ulikuwa na ukweli 100%, na usidhani rais ni mjinga kwa kusoma utetezi wako wa kijinga, sema kama ufanisi umeongezeka kwanini ulikuta projection ya collection 18/19 ikiwa 1.+++trilion we ukashusha hadi 760b?
Tuonyeshe saving zako za kiuhalisia ukilinganisha na watangulizi, ni uongo majengo yanaribika bila matengenezo?
Ppf ilikuwa hata kulipa lumpsum walishindwa iweje uje na pumba huku, acha Rais afanye ajuavyo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hivi hizi kelele zote inazungumziwa NSSF IPI, ni hii ambayo HQ yake ni pale jirani na DIT?
Ni hii ambayo imekataa kuwalipa walioachishwa kazi mafao yao?
Ni hii ambayo kama umestaafu ukienda kufuatilia mafao wanaanza kukuambia kadi zimebadilishwa na kuipata kadi mpya kila Siku mashine mbovu toka April mwaka Jana hadi leo?
Tuwe serious kidogo kwenye mambo ya msingi. Kama ni kwa sababu ya uongozi mpya ni heli ule wa zamani uliokuwa na wapigaji na wanachama hatukunung"unika kiasi cha sasa.
Kama na wewe mtoa mada ni mfanyakazi wa NSSF kuna tusi nimekutukana kubwa sana linalohusiana na ulipotokea kuiona dunia.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwahiyo ndio mmejipanga formation ya kusafishana...poor mind.Lipeni mafao yetu kwa wakati acheni porojo nyingi!

Sent using iPhone Xr
 
Hongera Sana urio umefanya kazi iliyotukuka,ndani ya miaka mitatu tu umeifanya nssf kuwa shirika namba moja Tanzania kwa mapato na kuongoza Kim's Cha mshahara kufikia kiwango kinachoridhisha
 
Wengi wanaulizia fao la kujitoa na wanasema bila hilo fao kuwepo yaliyoandikwa yote ni upupu mtupu. Wakati wa Rama Dau mtu alikuwa akilipwa fasta tu...ndani ya wiki mbili...kwa sasa hali ikoje?
 
Nisawa kila mtu aongee anavyojisikia, ila wastaafu wanateseka sana kutokana na mafao yao.
Kabisa mkuu tena wanawazungusha sana...utakuta mtu ni ni mgonjwa uzeeni tena changamoto zake ila wanamzungusha ili afe wapige izo hela ndio michezo yao
 
Back
Top Bottom