NSSF si shamba la bibi tena

Baraka Selemani

New Member
Jan 8, 2020
2
30
Nimesoma maandiko mengi kuhusu uongozi wa NSSF uliopo sasa chini ya Bwana Erio ambaye wengine wanalibananga jina lake kwa kumgeuza mchaga na kumwita Urio. Usifikiri kuwa wanakosea, la hasha, wanafanya makusudi ili waonekane kuwa hawalijui jina lake. Wengine wao ni watu wake wa karibu ambao ukitajiwa majina yao hutoamini jinsi wanavyomzunguuka. UTOVU WA FADHILA

Kwa bahati nzuri mimi nimekuwepo katika shirika tangu enzi za mheshimiwa Mustafa Mkulo wakati huo NSSF ilikuwa NSSF kweli, iliyojengwa katika misingi ta utumishi wa umma, si kidini wala kikabila. Kwa kifupi huyo bwana alikuwa kama ndiye mwanzilishi wa shirika, na kwa hakika bila kupepesa macho, ndiye aliyefanya shirika lionekane.

Baada yake alifuata mheshimiwa Ramadhani Dau ambaye naye alijitahidi kuzuungusha gurudumu aliloachiwa. Lakini baadaye aliiingia katika ubaguzi wa kutaka kulifanya shirika hili la Umma kuwa taasisi ya kidini ambayo Corridor zake zote zilibadilika ghafla na kuwa sehemu za ibada. Mambo haya yalifanyika bila mheshimiwa Dau kuyakemea, kwa maana hiyo inaonekana alihusika kuanzisha hali hiyo. Kwa kifupi shirika lilikuwa kama Kuwait.

Kwa kipindi chake mambo mengi yalifanyika hadi kulipeleka shirika kwenye hali ya ukata. Tulishuhudia wakati Fulani shirika likikopa fedha benki kwa ajili ya kulipia mishahara ya watwana sie. Miradi ya ovyo ovyo iliyozingatia maslahi binafsi ndipo ilipoanzishwa, na kila aliyekuwa na fursa alipata mahali pa kuvuna kwa ajili yake na familia yake. Kuanzia Bosi mwenyewe, hadi mhudumu wa ofisi.

Hapo ndio ilipokuja Dege Eco Village, manunuzi ya viwanja na mashamba yasiyohitajika, Eka moja ya ardhi ilinunuliwa hadi kwa shilingi 800,000,000/-; kiwanja kimoja pale Dodoma ambacho kwa taarifa za kiuchunguzi kilikuwa na thamani kati ya shilingi 200,000,000/- na 400,000,000/- kilinunuliwa na shirika kwa shilingi bilioni 5.

Taarifa zote hizi zinafahamika na zipo kwenye ripoti ya CAG. Kuna bwana mmoja anayeitwa Musiba, mwanaharakati huru ameshasema mara nyingi juu ya ubadhirifu uliokuwepo, katika awamu hii. Akiuizwa leo atatiririka hadi utapatwa na hasira.

Baada ya hapo ilifuata awamu ya Profesa Mbobezi wa uchumi, G. Kahyarara ambaye hakudumu sana. Muulize atakueleza ubadhirifu alioukuta japokuwa naye aliangukia katika mkumbo ya upigaji uliojificha ndani ya uzalendo. Huyu alikuwa mwenye porojo nyingi zilizojaa nadharia za kiuchumi zisizotekelezeka.

Baada ya Profesa kulishindwa dude hili la NSSF, ndipo Mheshimiwa Rais Dokta John Pombe Joseph Magufuli akamteua bwana Erio ambaye hana historia ya wizi wala ubadhirifu ambaye kwa kweli amepigwa vita kubwa.

Alipoingia NSSF huyu bwana, Mbobezi wa taaluma ya Sheria alikuja kwa staili utekelezaji wa kile mheshimiwa Raisi alichokuwa akitaka, yaani kupambana na ubadhirifu, wizi na ufujaji wa mali ya umma. Alibana mianya yote ambayo wengine tulikuwa tumeizoea ya kupatia “riziki”.

Kwa kweli mwanzoni hata mimi nilimchukia kwa kuwa alisababisha moto ukawaka kwenye mifuko yangu. Lakini baadaye nikatafakari kitu uzima, nikakubali hali halisi kuwa maisha tuliyokuwa tukiishi hayakuwa sahihi. Moto kwenye mifuko haujaisha lakini naona ni bora niangalie njia nyingine za halali za kupatia kipato.

Kuna mtwana mmoja alishaniambia kuwa wanasheria wanafuata sheria kwenye kutawala, hili nimelishuhudia maana kila kitu kilichokuwa hakiruhusiwi kwenye sheria kilisitishwa, kwa wafanyakzi wengi hili halikuwa jambo jema walitamani yale mazoea yao yaachwe kama yalivyokuwa jambo ambalo kwa mwanasheria lingekuwa dhambi.

Kumbuka wale watu waliokuwa wakimpigia kelele mheshimiwa Rais kuwa aachie hela kwa kuwa maisha yalikuwa magumu, na yeye akawa akiwajibu kuwa watu wafanye kazi pesa watazipata.

Kwa tathmini yangu ya haraka huyu bwana Erio atapigwa vita kali hata afanyeje, bwana Erio, ile miradi mnayokamilisha kule Dungu, kijichi na Tuangoma inakuwinda kama mzimu. Kuna watu walitamani ushindwe hata kukamilisha hiyo sehemu ndogo. Walitamani uwatafute wale wakandarasi walioianza hiyo miradi ili waikamilishe na upigaji wake. Kama ulikuwa hujui, nakupa taarifa sasa.

Unaonekana kama umezuia ulaji wa watu kwenye hizo sehemu. Hujuma hizi hazijaishia kwa hao tu, hata wafanyakazi wengine wanakuhujumu, na wengine wanatumiwa na watu waliokuwepo kwenye tawala zilizopita. Waangalie sana hao. Kwa kuwa niko nao kazini kila siku, ukitaka hata majina nitakutajia.

Kwa mfano angalia yule kiongozi wa USA River, anatumiwa na watu wa nje kukuhujumu na ushahidi upo, na Mameneja wengine wa mikoa iliyopo Dar es salaam. Wengine nitaendelea kukutajia hadi uwajue wote. Wakitaka nisiwataje waache hujuma. Kulihujumu shirika ni kuihujumu serikali na kupinga juhudi za Raisi za kukuza uchumi wa nchi na kutatua kero za wanyonge.

Mradi wa Dege ni mzimu mwingine utakaokukosesha raha kwa kuwa matarajio ya walaji wengi umeyakatiza kwa kukataa kuendelea kutoa fedha za kumalizia mradi huo. Komaaa wala usirudi nyuma, hilo Dege ni Bomu la Atomiki, mradi hauna tija, ubadhirifu umejaa. Naamini hata Mheshimiwa Raisi hakubaliani na mradi huo.

Bwana mmoja akaandika katika makala yake eti kwa kuja Erio NSSF imedorora. Mimi nilikuwepo tangu enzi na enzi, ambaye nimeona awamu zote nasema NSSF haijadorora. Mdororo utakuwa umetokea kwenye mifuko ya huyo jamaa na mkewe. Maendeleo aliyoyafanya bwana Erio kwa muda mfupi yanaonekana dhahiri. Hata kule PPF alikotoka aliacha Mfuko ukiwa na hali nzuri sana na ushahidi upo. Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni.

Kwa ushahidi niliona baada ya uchunguzi wangu ni kuwa

1, Mwezi Julai 2018 wakati Mifuko ilipokuwa inaunganishwa ukaguzi wa wataalamu waliofunga mahesabu ya PPF walitanabahisha kuwa thamani ya Mfuko wa PPF ilikuwa ni Shilingi trilioni 3.1 wakati shirika la NSSF lilikuwa na thamani ya Shilingi trilioni 3.25.

Thamani ya Mfuko wa PPF ilitengenezwa na wafanyakazi 400 wakati ile ya NSSF ilitengenezwa na watumishi 1400. Je, kwa mwenye akili timamu ni Mfuko upi hapo ulikuwa ukifanya vizuri ? Hebu watu waache hekaya za Abunuwasi hapa.

2. Wakati huo return on investment ya PPF ilikuwa asilimia 22 wakati NSSF ilikuwa - 3%;

3. Fedha (liquid cash) zilizokuwepo PPF wakati huo zilikuwa jumla ya shilingi trilioni 1.5 trilioni pamoja na fixed deposits and government bonds.

Ikumbukwe wakati huo PPF ilikuwa ikilipa mafao na madeni yake bila matatizo yoyote. Ukija upande wa shirika letu, pamoja na mbwembwe zote tulizokuwa tukipiga shirika (NSSF) lilikuwa na Shilingi bilioni 350 wakati deni la mafao kwa zaidi ya miaka miwili (2) lilikuwa shilingi bilioni 109.

4. Kwenye TEHAMA, PPF ilikuwa ikifanya shughuli zake kwa kutumia mifumo ya kielektroniki tangu mwaka 2008 wakati NSSF ilikuwa ikiendesha mifumo yake manually kwa 80%. Kabla ya bwana Erio kuletwa, Shirika letu la NSSF lilishatumia shilingi bilioni 12 kuweka mifumo ya kielektroniki bila mafanikio. Aibu gani hii.

Kwa miaka 13 ambayo bwana Erio aliiongoza PPF hakujawahi kuwa na ubadhirifu wowote, na hata data zinazosemekana kupikwa na bwana Erio haikuwa kweli. CAG ambaye ndiye mtoa taarifa sahihi za Mfuko hakuwahi kuandika hoja yoyote ya aina hiyo iliyowahi kutolewa.

Shirika la NSSF wakati wa Profesa Kahyarara ndilo liliwahi kutoa taarida kuwa wanachma wa NSSF walikua milioni moja (1,000,000) wakati Mheshimiwa Rais alisema dhahiri katika kikao alichokiitisha Ikulu tarehe 28/12/2018 kuwa idadi kamili ilikuwa ya wanachama wa NSSF ilikuwa 448,000.

Pamoja na kwamba kiupinzani mimi ningeitetea NSSF, lakini msema kweli ni mpenzi wa Mungu. Data za NSSF ndizo zilikuwa za kuchemshwa.

Sasa ieleweke wazi kuwa kinachosumbua hapa kwetu kwa sasa ni njaa na ulafi. Bwana Erio anaelekea kukomesha kabisa ubadhirifu na wizi. Sasa inashangaza kumsikia mtu akisema eti nyie Menejimenti yenu (Mr. Erio na wenzako) eti mjifunze kutoka kwa waliotangulia. Mimi nawashauri muupuuze huo ushauri, hakuna cha kujifunza kwa waliopita. Mkikubali huo ushauri hata mimi nitawashangaa. Au mko tayari:-

5. Kujifunza kununua kiwanja cha milioni 400 kwa bilioni 5 kama walivyofanya wenzenu?

6. Kununua kiwanja baharini, Kunduchi Beach

7. Kuanzisha mradi kama Dege kwa kushirikiana na wahujumu uchumi?

8. Kufanya kazi ya siku mbili kwa Perdiem za mwezi mzima

9. Kuifanya taasisi kuwa ya kidini?

10. Kujifunza na mengine mengi ambayo nitayataja kama wendawazimu wengine wataibuka kuwatetea hao waliopita
Tena jambo lingine la utovu wa adabu ni lile la kuikosea taasisi ya Usalama wa Taifa kwa kudai imewekwa kwenye payroll na bwana Erio. Hii ni dharau kubwa sana kwa Taasisi hiyo.

Kuna wakati Baba wa Taifa aliwahi kumfukuza Askofu mmoja ambaye alidai kuwa ameiweka Serikali ya Tanzania Mfukoni. Hivi leo mtu asiye na woga anaweza kusema maneno yanayofanana na hayo ? Tena kwa Taasisi nyeti kama hiyo? Wahusika kazi kwenu.

Kwa Faida ya ninyi msiojua ukweli. Nimepenya mpaka kwenye taarifa sahihi za Shirika. Acha niwamegee hizi chache ambazo anayetaka anaweza kuthibitisha.

11. Pensheni ya wastaafu inalipwa tarehe 25 ya kila mwezi na inalipwa moja kwa moja kwenye akaunti za wastaafu. Hatua hii imesaidia kuokoa shilingi bilioni 1.3 kwa mwaka ambazo zilikuwa zikilipwa kama kamisheni kwa Post-Giro.

12. kwa mwaka wa fedha 2018/2019 michango ya wanachama imeongezeka kufikia shilingi bilioni 872 kutoka shilingi bilioni 690 mwaka wa fedha 2017/2018, ongezeko hili linatokana na matumizi ya mifumo ya kieletroniki ya fedha ikiwa ni pamoja na GePG na Internet Banking pamoja na uadilifu katika kufuatilia waajiri na Usimamizi madhubuti kwa watumishi, pia kuanzisha utaratibu wa billing, kuboresha ukaguzi kwa waajiri kwa kushirikiana na Taasisi zingine za Serikali kama TRA, WCF, OSHA, Idara ya Kazi, Wizara ya Mambo ya Ndani, na NIDA.

13. Nimethibitisha kuwa mapato yatokanayo na uwekezaji yameongezeka hadi kufikia shilingi bilioni 148 2018/2019 kutoka shilingi bilioni 131 mwaka 2017/2018.

Mapato ya daraja la Kigamboni yaliongezeka kutoka wastani wa shilingi bilioni 680 mwaka 2017/2018 mpaka wastani wa shilingi bilioni 950 mwaka 2018/2019.

14. Gharama za Uendeshaji kwa mwaka 2017/2018 zilikuwa asilimia 18% ambapo kwa sasa imeshuka mpaka 10% ambayo ndiyo matakwa ya miongozo ya kisekta.

15. Katika mwaka wa fedha 2017/2018 NSSF ilikuwa na malimbikizo ya mafao kwa wanachama 16,119 yenye thamani ya shilingi bilioni 109 wakati katika mwaka wa fedha 2018/2019 Shirika lililipa madai yenye thamani ya jumla ya shilingi bilioni 409 ikijumuisha malimbikizo ya 2017/18.

16. Thamani ya shirika imeongezeka hadi kufikia shilingi trilioni 3.72 kwa mwaka wa fedha 2018/2019 kutoka shilingi trilioni 3.25 trilioni kwa mwaka wa fedha 2017/2018. Hili ni ongezeko la shilingi bilioni 472 kwa kipindi cha mwaka mmoja.

17. Idadi ya wanachama imeongezeka kutoka 448,000 iliyokuwepo Disemba 2018 hadi kufikia 637,422 Desemba 2019.

Shirika pia limeokoa shilingi bilioni 1.5 kwenye ununuzi na matumizi ya server ambazo server zilizokuwa zinunuliwe kabla ya Erio kuingia NSSF zingegharimu shilingi bilioni 1.7 baada ya kuikata hiyo ruti server zikanunuliwa kwa shilingi milioni 160.

Kwa sasa uandikishaji wa wanachama unafanyika kwa kutumia kitambulisho cha Taifa ilikupata taarifa sahihi za wanachama kwa kutumia mfumo wa NIDA. Hapo shirika limeokoa shilingi milioni 200 Million kwa mwaka zilizokuwa zikilipwa kwa ajili ya mfumo uliokuwa ukitumika kuhakiki taarifa za wanachama kwa kutumia vidole. Mfumo huu pia umesaidia kupunguza matumizi kwa Kiasi cha shilingi bilioni 1.12.

Kwa mafanikio haya, bwana Erio hata ukihamisha wafanyakazi wote waliokuwa PPF ukawaleta huku hata mimi ningekuunga mkono. Hata hivyo, kwa hesabu zangu za kihenga NSSF ina Ofisi za Mikoa 29, kati ya hizo Ofisi za Mikoa 26 zinaongozwa na mameneja waliokuwa ndani ya NSSF. Ni mameneja wa Mikoa ya Arusha na Songwe pekee ndio wametoka PPF na yule wa Mkoa wa Morogoro amnbaye awali alikuwa wa LAPF.

Kwa leo nimetoa uzoefu wangu wa miaka kadhaa ya kuwepo kwangu kwenye shirika tangu enzi za Mr. Mkulo hadi haya ninayoyashuhudia leo. Acha tu niseme kuwa Mheshimiwa Rais John Pombe Joseph Magufuli unawakilishwa vema na bwana Erio.

Ule ubadhirifu uliokuwa unausikia ukifanyika NSSF unakaribia kuwa historia. Mteule wako akichanganywa na wateule wengine wa wizarani wanapigwa vita kwa sababu ya utekelezaji wa kuipeleka Tanzania katia hatua nyingine. Watoto wa mjini wanaita next level. Ukweli ni dhahiri kila mwenye macho anaona.

Pamoja na ukweli kwamba marekebisho ya shirika yameniletea mdororo mfukoni mwangu, na mto wa ugumu wa maisha unaniwakia sitaacha kusema ukweli kwa kuwa ucha Mungu wangu utakuwa na walakini kama nitasema uongo kwa sababu ya njaa.

Baadhi ya viongozi waliopita wa shirika, na baadhi ya wafanyakazi walilifanya shirika (NSSF) kuwa shamba la bibi lakini leo NSSF SIO SHAMBA LA BIBI TENA.

Wakandarasi na madalali wa upigaji fedha wote walikuwa wakichuma NSSF, hao ndio maadui wanaokuzunguuka.

Mungu atakupigania
 
William Eriyo, umeandika yote ila umesahau kusema kuwa wewe ni mtoto wa dada ya Benjamin William Mkapa. Mkapa ni mjomba wako, na hicho pekee ndiyo sifa yako ya kutumikia PPF na sasa NSSF.

Nani anaweza kuwa na data hizo kama siyo William Erio mwenyewe.
 
Daaah Erio bhna, Benja atakuita kukuonya akiona hii habari yako hapa umeandika hivi.

Umesema korido za NSSF zilibadilika zikawa kama msikitini, ungekuwa unajua kuwa waislamu wanaswali sehemu safi wala usingeandika ule upuuzi kuhalalisha udini.

Umesema sasa NSSF inafuata maagizo ya Rais, je huko NSSF hakuna utaratibu wake? hakuna mpango kazi na malengo ya taasisi mpaka inafikia hatua kufuata maagizo ya mtu?

Kwako wewe, kuwa wafanyakazi wengi ndio ufanisi sio?

Unajua kama kutokufuata sheria ni uhujumu uchumi pia? NSSF ya sasa hivi inachelewesha stahiki za watu na ni ya hovyo kabisa halafu unakuja kusifia uozo?

Hizo aya za mwisho umejisifia sana mpaka hata huyo aliyekuteua akiona atashangaa, ila kwa kuwa na yeye anapenda hivyo basi sio mbaya.
 
Lakini huo ushauri wa kutomalizia mradi wa Dege Eco village naona si sahihi, kama makosa yalishafanyika mwanzo ila kwa sasa hakuna budi kumalizia ule mradi.

Sehemu ni kubwa sana na majengo mengi tayari structure imekamilika utaachaje pale ilipo? Ndo maana watu saev wanaiba material pale

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Eti " Bwana Erio hata ukihamisha wafanyakazi wote waliokua PPF nitakuunga mkono". You are not smart kwenye usanii Bwana Erio. Hiki ndio kitu umekifnya kuanzia siku ya kwanza ulipoteuliwa kua DG

Unahamisha ile timu yako ya PPF kuiipelelka NSSF. Umeondoa mameneja wote waliokuwepo na wanakua replaced na watu kutoka huko ulipokua. Kwanza wakati wa uhai wa PPF mfuko ulikua na hali gani financially mpaka uhalalishe kuwaleta watu wako uliokua nao huko? Hii ni timu ya kujipanga kwa mkao wa kula
 
Jifunze kufanya utafiti si kila kitu una buni buni, ukitaka kujua fanya utafiti kama mwenzio vitu vipo wazi. Toka usingizini
William Eriyo, umeandika yote ila umesahau kusema kuwa wewe ni mtoto wa dada ya Benjamin William Mkapa. Mkapa ni mjomba wako, na hicho pekee ndiyo sifa yako ya kutumia PPF na sasa NSSF.

Nani anaweza kuwa na data hizo kama siyo William Erio mwenyewe.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Binafsi nafurah sana kuona shirika hili limebadilika hata utendaji wake umekua thabiti kabisaaaaaaa.. Erio anafanana na Awamu ya 5 inavyotaka. NO JANJA JANJA TIME. Yani unapata unachostahili sik unachotaman.. yani ni mwaka tu na nusu hivi lakinj mnyoosho unaonekana live kuwa mambo yamebana waliozoea slope

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Jifunze kufanya utafiti si kila kitu una buni buni, ukitaka kujua fanya utafiti kama mwenzio vitu vipo wazi. Toka usingizini

Sent using Jamii Forums mobile app
Wewe una kifafa cha mimba ndiyo kinakusumbua. Utafiti gani alofanya ? Erio kachukua fake ID eri Baraka Selemani halafu kasaidiwa na wapambe wake wa3 aliotoka nao PPF kuji promote humu JF
 
Lakini huo ushauri wa kutomalizia mradi wa Dege Eco village naona si sahihi, kama makosa yalishafanyika mwanzo ila kwa sasa hakuna budi kumalizia ule mradi.

Sehemu ni kubwa sana na majengo mengi tayari structure imekamilika utaachaje pale ilipo? Ndo maana watu saev wanaiba material pale

Sent using Jamii Forums mobile app
Hv nani atakaa kwenye yale majengo yakikamilika?
 
Daaah Erio bhna, Benja atakuita kukuonya akiona hii habari yako hapa umeandika hivi.

Umesema korido za NSSF zilibadilika zikawa kama msikitini, ungekuwa unajua kuwa waislamu wanaswali sehemu safi wala usingeandika ule upuuzi kuhalalisha udini.

Umesema sasa NSSF inafuata maagizo ya Rais, je huko NSSF hakuna utaratibu wake? hakuna mpango kazi na malengo ya taasisi mpaka inafikia hatua kufuata maagizo ya mtu?

Kwako wewe, kuwa wafanyakazi wengi ndio ufanisi sio?

Unajua kama kutokufuata sheria ni uhujumu uchumi pia? NSSF ya sasa hivi inachelewesha stahiki za watu na ni ya hovyo kabisa halafu unakuja kusifia uozo?

Hizo aya za mwisho umejisifia sana mpaka hata huyo aliyekuteua akiona atashangaa, ila kwa kuwa na yeye anapenda hivyo basi sio mbaya.
Daaah Erio bhna, Benja atakuita kukuonya akiona hii habari yako hapa umeandika hivi.

Umesema korido za NSSF zilibadilika zikawa kama msikitini, ungekuwa unajua kuwa waislamu wanaswali sehemu safi wala usingeandika ule upuuzi kuhalalisha udini.

Umesema sasa NSSF inafuata maagizo ya Rais, je huko NSSF hakuna utaratibu wake? hakuna mpango kazi na malengo ya taasisi mpaka inafikia hatua kufuata maagizo ya mtu?

Kwako wewe, kuwa wafanyakazi wengi ndio ufanisi sio?

Unajua kama kutokufuata sheria ni uhujumu uchumi pia? NSSF ya sasa hivi inachelewesha stahiki za watu na ni ya hovyo kabisa halafu unakuja kusifia uozo?

Hizo aya za mwisho umejisifia sana mpaka hata huyo aliyekuteua akiona atashangaa, ila kwa kuwa na yeye anapenda hivyo basi sio mbaya.
suala la korido kugeuzwa misikiti wala sishangai. inaweza kuwa kweli. ukienda ofisi za The Joint Finance Commission utayakuta sana mambo haya ya kuswali ofisini. ndugu zangu waislam badilikeni.
 
NSSF Ubungo Plaza kuna kamama kamoja kembamba flani hivi na keupe kiasi. Age ni kama 53+ hivi. Kanaongea speed ako na hakataki kusikiliza wateja kwa makini. Wale jamaa nililazimika kuacha visenti vyangu vichache kwa maana hata kadi tu waligoma kunipa. Tokea June mwaka jana wanadai mashine imeharibika, yaani hakana uongo mwingine kila siku kananambia hivo. Kuna huyo mmama mweusi anavaa ushungi, anaongea taratibu huyo anadeal hasa na kuandikisha na mstaarabu kiasi flani.
 
Back
Top Bottom