NSSF hodari wa kudai na kufuatilia michango lakini wazembe kulipa mafao ya Wastaafu

Mchanya

JF-Expert Member
Jul 29, 2015
976
1,526
NSSF ninayoifahamu ni wakali sana mwajiri akichelewesha michango, wakali sana mwajiri asipowasilisha michango ya wanachama lakini NSSF ni wazembe, wavivu na watesi wa wanachama wao pale wanapokuwa hawana michango na wanapofuatilia mafao yao, hata fao la kukosa Ajira tu.

Unakuta mtu anachangia miaka kumi, ishirini hata 25 lakini atateseka miezi wakati hana ajira na ana mamilioni yamelala tena yanawekezwa na NSSF kwa faida yao wao NSSF na si kwa faida ya wanachama wachangiaji.

Mwanachama anakumbana na adha ya kwanza ya foleni kwenda kupeleka fomu baada ya kuijaza. Unakuta watu wanahitaji huduma tofauti lakini mtaitwa kwa makundi kama kundi moja hata mkiwa mia na ishirini. Kwa faida wanazopata kutokana na hela za wanachama kwa nini wasiweke hata mashine kama za benki kila mmoja aende kwa namba katika shida yake tofauti? Maana anayekusanya fomu akipeleka kama ukiwa wa kwanza fomu zinageuzwa unakuwa wa mwisho.

Hii imetokea NSSF kinondoni ambao ofisi zao ziko Ubungo Plaza. Na mkusanya fomu na anayesimamia kuingiza wenye shida anawaona kama watoto wakati wengine wanaweza hata kumzaa au kuwa mjukuu. Kwanini mnawadhalilisha wanachama kwa kiasi hiki?

NSSF Kinondoni ni janga. Ukishawasilisha madai unaambiwa ndani ya mwezi hela yako itaingia, tena wanasema "zikipita wiki mbili hujapata rudi hapa" lakini ukienda baada ya wiki mbili utaambiwa 'faili linashughulikiwa rudi tena baada ya wiki mbili'. Ukija utakuta faili lina makosa lakini hukuitwa maana kuna mtu kalikalia.

Utarekebisha au kutoa maelezo. Utaambiwa 'njoo baada ya wiki mbili' ukienda pale unapotakiwa kuuliza hatua gani faili limefika unaambiwa kaunge foleni uchukue namba unajikuta wewe ni mtu wa Mia moja na kumi. Ukifika unaambiwa njoo baada ya wiki mbili. Hizo wiki mbili zinakwenda miezi. Rudi baada ya wiki ni lugha ya kawaida sana kwao.

Utaamua kuwaandikia email. Utajibiwa 'suala lako linashughulikiwa'. Ukitaka kujua linashughulikiwa limefikia wapi? Unapewa namba kwamba suala lako limeripotiwa kwa reference namba fulani lakini huambiwi ni hatua gani limefikia.

Ni wazi kwamba yanatengenezwa mazingira ya rushwa. Kwa kweli hili inawezekana limeshasabisha matatizo ya afya ya akili kwa wanachama kadhaa waliostaafu.

Waziri Mwenye Dhamana Upo? Rais Upo?
 
Back
Top Bottom