no girls allowed, strickly for men

MKATA KIU

JF-Expert Member
Nov 22, 2010
2,861
6,222
Heshima kwenu brothers and poleni na majukumu,

Nahitaji kushare mawazo na wenzangu naomba wapondaji wakae kimya is only ushauri needed,
Mi ni kijana wa 25 yrs graduate and working somewhere in town, kuna msichana around 21yrs I have interest on her but nakosa kwa kuanzia kutokana na scenario behind us, huyo binti yupo chuo first year now hapa dar, nakosa pa kuanzia kwa sababu my brother alikuwa anadate na dada yake na alimkuja kumtosa vibaya na kuoa mwingine na hii alileta kama chuki kwa familia yetu lakini ukweli ye ndo sababu as alikuwa anacheat wakati bro yupo nje kimasomo na anahisi si ndo tulisababisha asiolewe, sasa huyu binti hajui kama mimi ni mdogo wa X aliyemfanya dada yake atake kujiua those days,

Na mimi naamini sina nia mbaya na binti hiyo if God wishes tujenge nae familia, nashindwa nimset vp atleast for a date as sitaki dada yake ajue hadi mambo yatapochanganya, I think ninavyo vigezo vya college ladies vya kijinga as a car, a job, etc but nakosa point as her sister hanipendi, huyo binti nimekutana nae juzi nikafanikiwa kupata namba sasa next step ndo issue as dada yake akijua ni balaa

Wadau tupeane tips nitoke vipi
 
si useme tatizo lako sio dada yake bali ni udomo zege wako....:shetani:
 
inaonesha ww ni domo zege......avatar yako inakureflect the way kweli ulivyo..nitarudi..
 
Mkuu naona unaogopa kutoswa hata kabla hujatoswa
Ingia hapo na fanya the way The Boss ameshauri hapo
Fanya kweli na usiogope lile ambalo halipo maana umeanza kuliogopa hata kabla halijawa issue
 
hapo hakuna tatizo
msichana ukimkoleza hata uwe ulimtukana baba yake utasamehewa

wewe anza kumkoleza taratiibu

Yaani wewe the boss ndo real brother, mi naomba ushauri wanaanza kuponda tu domozege, I play a lot with her sisters but hapa nimenasa hadi nimekuwa domozege, hawajui sehemu ukipenda kweli ujanja unaisha, hebu funguka brother hizo step as binti na dada yake wanapatana sana
 
anza ku datenae kwa kumuita
aje ulipo kama ni bar au cinema
unaanza out nae taratibu
jifanye na wewe humjui dada yake
siku ikijulikana jifanye hukujua na huoni why usimuoe kwa ajili hiyo
 
Yaani wewe the boss ndo real brother, mi naomba ushauri wanaanza kuponda tu domozege, I play a lot with her sisters but hapa nimenasa hadi nimekuwa domozege, hawajui sehemu ukipenda kweli ujanja unaisha, hebu funguka brother hizo step as binti na dada yake wanapatana sana

Mkuu kwani date yako ya kwanza unampeleka home kwao
Si mpange mkutane sehemu muongee ya kwenu kwanza na mmalizane
hayo ya kuja kufahamu kuwa wewe ulikuwa ndugu yake na ex wa dada yake ni mambo ya baadae aise
Pambana kwanza kuwin her heart then ndipo sasa utakuwa na uwezo wa kufunguka na wala sehem nyingine usiseme kabisa aje agundue baadae mwenyewe kuwa kuna uhusiano huo
 
Mkuu naona unaogopa kutoswa hata kabla hujatoswa
Ingia hapo na fanya the way The Boss ameshauri hapo
Fanya kweli na usiogope lile ambalo halipo maana umeanza kuliogopa hata kabla halijawa issue

Mahabuba hebu mpatie zile tricks zako ulizonilegeza mie mpaka nikasahau ugomvi wa wazazi wetu......usimbanie banaaa
 
Na mimi naamini sina nia mbaya na binti hiyo if God wishes tujenge nae familia,

Wadau tupeane tips nitoke vipi

Mkuu since dhamira yako ni long term relationship na sio hit and run.., ni vema ukaweka your cards on the table kuanzia mapema.., kosa sio lako ni la mtu wa familia yako.., hivyo basi mapenzi ya kweli ya mwenza hujengwa na TRUST na utakuwa mtu wa upeo mfupi kama ukificha kitu ambacho soon or later kitajulikana (hivyo basi nakushauri kama hutaki kula tunda kwa muda mfupi.., unataka kuaminiwa for long-term trust mueleze kwamba upo related na yule mtuhumiwa and you are sad about what happened na wewe hautafanya hio issue na unaomba awe upande wako kwa ndugu zake kuonyesha motive yako ni nzuri
 
Kweli wewe domo zege hata usibishe,hujui hata kumkoleza binti anyway cha kwanza be a gentleman,take her out open the door for the chich fanya vitu ambavyo vitakutofautisha na teenagers sawa then take it from there,akija kujua wewe ni nani kwa treatment ulizompa inakuwa rahisi kukuelewa kama alivyosema The Boss
 
Kama umepata namba yake ya simu then hapo ndo pakuendelea naye, anza hata kwa sms and trust me if she is interested with you atajibu. Msichana hafikirii sana kama siye wanaume, hata kaa ungemtusi mamaake, ye akiingia relini huwa haoni hasikii, just do it.
 
Mahabuba hebu mpatie zile tricks zako ulizonilegeza mie mpaka nikasahau ugomvi wa wazazi wetu......usimbanie banaaa

mahabuba wangu nimekumiss niaje
Yaani naona kama muda hauendi vile
Huyu mwache kwanza maana naona ndio kwanza anaingia kwenye anga za mapenzi bado kabisa hajajua kuwa mapenzi yanaendaje
Zile mbinu ni za hali ya juu sana
 
Kaka mtemee cheche...kwamba dada yake alitoswa,halina mashiko so far halina nafasi kwenye mambo yenu...ila nikukumbushe kumaanisha!
 
Heshima kwenu brothers and poleni na majukumu,

Nahitaji kushare mawazo na wenzangu naomba wapondaji wakae kimya is only ushauri needed,
Mi ni kijana wa 25 yrs graduate and working somewhere in town, kuna msichana around 21yrs I have interest on her but nakosa kwa kuanzia kutokana na scenario behind us, huyo binti yupo chuo first year now hapa dar, nakosa pa kuanzia kwa sababu my brother alikuwa anadate na dada yake na alimkuja kumtosa vibaya na kuoa mwingine na hii alileta kama chuki kwa familia yetu lakini ukweli ye ndo sababu as alikuwa anacheat wakati bro yupo nje kimasomo na anahisi si ndo tulisababisha asiolewe, sasa huyu binti hajui kama mimi ni mdogo wa X aliyemfanya dada yake atake kujiua those days,

Na mimi naamini sina nia mbaya na binti hiyo if God wishes tujenge nae familia, nashindwa nimset vp atleast for a date as sitaki dada yake ajue hadi mambo yatapochanganya, I think ninavyo vigezo vya college ladies vya kijinga as a car, a job, etc but nakosa point as her sister hanipendi, huyo binti nimekutana nae juzi nikafanikiwa kupata namba sasa next step ndo issue as dada yake akijua ni balaa

Wadau tupeane tips nitoke vipi
Ondoa inferiority complex kutokana na tatizo ambalo haukulisababisha wewe wala huiyo mpenzi wako. Mapenzi ya kaka yako na dada yake wala hayana uhusiano na mapenzi yako wewe na yeye. Fuata ushauri wa Boss, lakini angalia sana hisia zako za jinsi kaka alivyomtenda dada yake zisije kuwa kikwazo hapo baadaye. Focus kwenye mahusiano yako wewe na huyo binti, hayo ya kama yako na dada yalishapita zamani na hata mkiyajua, mweleweshe binti kuwa hayana uhusiaono wowote kati ya wewe na yeye
 
Mkata kiu umebagua na wataka tu wa kaka/baba hapa. But nina la kusema pia tokana na mtazamo wangu. Hapa nadhani haijalishi tena ni kwanini kakako alimbwaga huyo dadake unae m admire. Inaweza onekana mzaha, ila from experience na the way nimeona kwa wengi Mapenzi hayawi in Isolation. Kwamba maadamu wewe na huyo dada mwapendana basi inatosha…. Hapana.

Kama unampenda na una hope na Imani kabisa kua unafikiria siku moja umuoe then kwa kweli inabidi mresolve hio issue ya chuki kwanza. Waweza hata mtafuta dadake kuomba uongee nae kuona ana msimamo gani dhidi ya mawazo yako. Kama ni kwa ajili tu haya mambo ya Girlfriend na Boyfriend na hamna hakika na the future of the relationship then naamini hapo mwaweza ingia katika mahusiano. Hata hivo hapa umetoa hali halisi….. Ila kama hutajali MKATA KIU wewe shida ipo wapi saana? Ni kipi cha kupa hofu ya kukwamisha hayo mahusiano?
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom