Njoo tujadili namna ya kutengeneza zaidi ya mil 100 ndani ya mwaka mmoja

khaliciouz

JF-Expert Member
Nov 12, 2013
579
210
Habari wakuu....... Itifaki imezingatiwa!

Rejea kichwa hapo juu!


Nianze na swali hili hivi ni biashara gani au kwa kiwango gani au kwa plan gani mfanyabiashara anaweza kurtengeneza pesa hiyo kuanzia mil 100,000,000/=?

Naomba niweke mrejesho wakuu kwamba nimepata biashara ya kutengeneza zaidi ya million 100 kwa mwaka.

Na biashara yenyewe ni ya blogging kupitia adsense.. kwa watu wanaingia kwenye blog yako wakiclick unapata pesa.. jinsi watu wengi wanavyoingia kila siku kwenye blog ndio unajiongezea kipato.

Mwanzo ilikuwa ngumu kupata hao viewrs lakini nikaamua kuweka pesa sasa na advertise blog yangu kupitia facebook niliweka dola 250 matokeo yake nimepata dola 1000 + na bado wanaendelea kuja.
 
Karibia biashara yoyotr inaweza kutengeneza kiasi hicho, hiyo ni chini ya 50,000 usd sio nyingi kama unavyofikiri. Watu wanatengeneza hiyo kwa mshahara tu.
 
Karibia biashara yoyotr inaweza kutengeneza kiasi hicho, hiyo ni chini ya 50,000 usd sio nyingi kama unavyofikiri. Watu wanatengeneza hiyo kwa mshahara tu.

Hayo ndio mambo mkuu.... Kazi gani hizo zinaleta mshahara zaidi ya hapo?

Na je mfano wa biashara ambao at minimum amount unaleta maximum kuliko others?
 
Mie nimeelewa unataka kutengeneza milioni 100 ndani yamuda mfupi au kwa mkupuo, kama sivyo ulivyomaanisha nikosoe.
Mara nyingi mwanzo mgumu na milioni 100 ni pesa ndefu kuifikia shurti use na ngazi za kupanda.
Ushauri wangu, lenga kutengeneza milioni moja ila anza na kuzalisha hata laki kwa mwezi kama si milioni hapa itategemea na uwezo wako Wa mtaji na nguvu ya ucharipikaji. Kuwa Tu mbunifu na waweza anza na eneo unaloishi, angalia wakazi Wa eneo hilo sana changamoto gani ambayo anahitaji utatuzi? Hii changamoto itafutie uchambuzi kisha unaipeleka hapo kwa kuwauzia aidha Huduma au bidhaa kwa pesa ambayo watamudu kulipa na kukupa wewe faida. Ukitunza faida ndani ya mwaka 1 unaunda milioni 100.
Usiku mwema.
 
Habari wakuu....... Itifaki imezingatiwa!

Rejea kichwa hapo juu!


Nianze na swali hili hivi ni biashara gani au kwa kiwango gani au kwa plan gani mfanyabiashara anaweza kurtengeneza pesa hiyo kuanzia mil 100,000,000/=?

Ahsante

Hiyo hela kuandika ni nyingi ila hamna kitu inapatikana tu.
 
cha msingi ni kuwa na biashara nyingi ambazo ukicombine kwa pamoja unapata hiyo pesa kwa mda mfupi tu.....By mkurugenzi wa kampuni ya mjasiriaakili enterprises
 
Back
Top Bottom