Njoo hapa ujifunze namna ya kumtambua mganga feki na mganga konki

OMOYOGWANE

JF-Expert Member
Dec 30, 2016
3,652
9,253
Ukiona mganga yeyote anakufuata akutatulie changamoto yako haijalishi kakufuata pm au ana kwa ana basi jua huyo ni tapeli.waswahili wanasema mwenye shida humfuata mganga. Kama yeye kakufuata basi wewe ndio mganga.

Mganga yeyote anayeweka bango kwenye nguzo ya umeme, kwenye magazeti, kwenye mtandao wa kijamii huyo ni tapeli.

SIFA ZA MGANGA KONKI

Ukifika stendi au kijiji cha mbali ukauliza naulizia kwa flani wakawa wanamjua na kumtambua na kukuelekeza anapoishi hata watoto wadogo wakawa wanamjua basi huyo ni dalili ya kwanza ya mganga konki.

Ukifika kwake ukakuta msululu wa watu au foleni kubwa sana na magali mengi yamepaki nje basi jua huyo ni mganga konki.

Ukienda kwake ukakuta kajenga nyumba nzuri ya kisasa hiyo ni dalili nyingine ya mganga konki.

Ukiwa unaongea nae hakubembelezi anakua kama vile hakuoni huku baadhi ya watu uliowakuta wakimnyenyekea na kujipendekeza kama watoto wadogo huku wengine wakisalimia kwa kupiga magoti tena ni wanaume kabisa basi jua huyo ni mganga konki.

Ukifika kwake ukakuta watu wapo bize na vibeseni huku wengine wakiwa wamevaa boksa tu basi jua huyo ni mganga konki.

Ukimkuta katulia simu yake inaita masaa 24 kwa kupigiwa sana basi jua huyo ni mganga konki.

Ukifika kwake hakuulizi shida yako yeye atapiga ndumba zake akakuambia kilichokuleta basi jua huyo ni mganga konki.

Ukifika kwake ukakuta anawasaidizi wengi basi jua huyo ni mganga konki.

Ongezeeni zingine wakuu mimi nimevhoka kuandika
 
Unaweza hata kuamua kuwa mtafiti kanzu

Nenda kwake akutibu halafu umdhulumu chake 😆😅

Usipofanikiwa na haujamlipa ni lose lose hamna shida.
Ukifanikiwa na haujamlipa, utapata wasiwasi kwamba msala nisipolipa hivyo utarudi umlipe so itakuwa win win.

Ndiyo maana mifumo ya kiasili ya kiganga wakikuyu na wasukuma kwa niliowasoma ni utaratibu kuaguliwa bure ukishapona ndio utalipia katika namna ya zawadi. Win win kila siku.
 
Hakuna mganga konki.

Fikiria watu walivyo na dhiki za maisha, angekuwepo huyo mganga konki anaeweza kutatua tatizo lolote si angetambulika dunia nzima? Si unaona mahospitali kunavyojaa? Watu wanaona wagonjwa wanaenda huko wanapona, ni ushahidi thabiti. Hakuna ushahidi thabiti juu ya uchawi.

Achaneni na njia za mkato, maisha sio marahisi hivyo.
 
Unaweza hata kuamua kuwa mtafiti kanzu

Nenda kwake akutibu halafu umdhulumu chake 😆😅

Usipofanikiwa na haujamlipa ni lose lose hamna shida.
Ukifanikiwa na haujamlipa, utapata wasiwasi kwamba msala nisipolipa hivyo utarudi umlipe so itakuwa win win.

Ndiyo maana mifumo ya kiasili ya kiganga wakikuyu na wasukuma kwa niliowasoma ni utaratibu kuaguliwa bure ukishapona ndio utalipia katika namna ya zawadi. Win win kila siku.
Hii niliikuta mtwara kama utani nilimpeleka mwanangu akaoe basi akaniambia twende hivi akaenda kwa bibi mmoja huyo bibi unaeleza nn unataka anakufanyia dawa na anakuuliza ukifanikiwa utaniletea nini sasa jichanganye useme kitu fulani alaf usipeleke ukishafanikiwa ndio inakua bas tena mafanikio yanayeyuka. Mwanangu aliahidi mbuzi kurudi town akapata tenda ya nyumba akavuta kibunda safi na akapeleka mbuzi alieahidi.

Sitaki mtu pm
 
Hakuna mganga konki.

Fikiria watu walivyo na dhiki za maisha, angekuwepo huyo mganga konki anaeweza kutatua tatizo lolote si angetambulika dunia nzima? Si unaona mahospitali kunavyojaa? Watu wanaona wagonjwa wanaenda huko wanapona, ni ushahidi thabiti. Hakuna ushahidi thabiti juu ya uchawi.

Achaneni na njia za mkato, maisha sio marahisi hivyo.
Tatizo lipo kwenye kufuata masharti mkuu napenda sana kuchunguza mambo nishaona watu waliofanikiwa kwa uganga nishaona walioshindwa na mganga ni huyo huyo na kingine ni chimbuko lako kuna watu wana mizizi isiotaka mambo mengi ukiweka uganga hufanikiwi mpak ukatambike kwanza kwenye mizimu ya familia yenu ndipo mambo yanafunguka.

Wapo wanaotambika wapo wanaologa yaani ujijue ww njia yako ni ipi kuna jamaa yangu alikua hafanikiwi kila afanyalo linabuma na ana jitahidi kweli kupambana akaenda kwa mganga akaambiwa rudi kwenu kasalimie wazee jamaa kwenda wazee wake wakamwambia tulikua tunasubiri uje akapewa baraka za wazee akarudi town akaendeleza mapambano
 
Tatizo lipo kwenye kufuata masharti mkuu napenda sana kuchunguza mambo nishaona watu waliofanikiwa kwa uganga nishaona walioshindwa na mganga ni huyo huyo na kingine ni chimbuko lako kuna watu wana mizizi isiotaka mambo mengi ukiweka uganga hufanikiwi mpak ukatambike kwanza kwenye mizimu ya familia yenu ndipo mambo yanafunguka. Wapo wanaotambika wapo wanaologa yaani ujijue ww njia yako ni ipi kuna jamaa yangu alikua hafanikiwi kila afanyalo linabuma na ana jitahidi kweli kupambana akaenda kwa mganga akaambiwa rudi kwenu kasalimie wazee jamaa kwenda wazee wake wakamwambia tulikua tunasubiri uje akapewa baraka za wazee akarudi town akaendeleza mapambano
Nimekuelewa mkuu ila angalia,

Matatizo mengi yanayopelekwa kwa waganga ni masuala mtambuka, yanategemea vigezo vingi ambavyo vingine viko nje ya uwezo wetu, vingine hatuvitambui. Matatizo kama kusalitiwa na mpenzi, umaskini, nguvu za kiume nk. Kwenda kwa mganga na kufanya matambiko ni kujipa moyo tu hakuna msaada.

Mfano wameenda watu kadhaa kwa mganga kutafuta utajiri, uwezekano wa baadhi kati ya hao kufanikiwa upo ila sio mkubwa kama wa wote kufanikiwa. Wataenda huko watafanya biashara, wachache watafanikiwa kupitia vigezo flani mfano eneo zuri la biashara, huduma nzuri kwa wateja, kushusha bei nk.

Sasa hao waliofanikiwa wataamini mafanikio yao yametokana na huyo mganga, wataanza kumuongelea, mzunguko upo hivyo, ndo biashara ya waganga.

Matatizo yanayotaka suluhisho za moja kwa moja kama magonjwa yasiyoambukiza, ulemavu, magonjwa ya akili nk, waganga hawayawezi. Ni kama hawa kina mwamposa tu.
 
Duh huyu atakuwa zaidi ya Mungu maana hata Yesu mwenyewe pamoja na Mungu wanatangazwa tena mwanzoni walitangazwa kwa upanga.

Huyo mganga ulie muumba kwenye Uzi wako ha exist kwenye dunia hii. Nenda kapekue mpaka chini ya bahari huwezi kumpata.

Mungu mwenyewe na nguvu zake zote lakini anatangazwa seuze mwanadamu kama wewe.

Nimempa demu wangu asome Uzi wako akasema " watu kama nyie ndio mnao lalagwa na waganga" so kuwa makini sana mkuu unapelekea sio pazuri hata kidogo.
 
Tatizo kubwa linaloikabili nchi yetu na wananchi wake ni ujinga (Si upumbavu) walionao watanzania wengi katika kuamini na kujikita sana kwenye imani za kishirikina, kama huyu mleta mada. Muda na nguvu anazotumia kutafiti na kuleta taarifa kuhusu masuala haya ya waganga angeweza kuutumia kufanya mambo makubwa ya maendeleo yake na jamii iliyomzunguka. Mleta mada ni mfano wa watanzania wengi wanaoamini na kushiriki imani za kishirikina lakini kiuhalisia hawana maendeleo yoyote ya maana na hawapigi hatua yoyote katika kujikwamua kiuchumi.

Ili ufanikiwe maishani kwanza unahitaji kuwa na imani binafsi isiyotetereka kwa hicho unachotaka kukifanikisha, unahitaji kujua kusudi lako kuu, uwe na malengo ya muda mrefu, uwe na nidhamu endelevu ya kukomalia hicho unachotaka kufanikiwa. Hakuna uchawi hapo! Imani yako ni muhimu sana hapa, kama huamini hutafanikiwa.

Kwa kuwa wengi hawana imani (Isiyotetereka) hujikuta hawajiamini, wamekata tamaa wakifikiri kwamba hawatafanikiwa, hapo ndipo 'mganga' anapowapata, anachofanya mganga ni kuwapa hiyo imani (Si dawa, si tiba) kwamba 'usiwe na wasiwasi utafanikiwa', unapotoka kwa mganda unakuwa umejijengea imani kwamba 'sasa nitafanikiwa', wakati ulitakiwa kujijengea imani wewe mwenyewe ili ifanikishe mambo yako.

Waganga wanacheza na akili zenu
 
Duh huyu atakuwa zaidi ya Mungu maana hata Yesu mwenyewe pamoja na Mungu wanatangazwa tena mwanzoni walitangazwa kwa upanga....

Huyo mganga ulie muumba kwenye Uzi wako ha exist kwenye dunia hii. Nenda kapekue mpaka chini ya bahari huwezi kumpata.


Mungu mwenyewe na nguvu zake zote lakini anatangazwa seuze mwanadamu kama wewe...


Nimempa demu wangu asome Uzi wako akasema " watu kama nyie ndio mnao lalagwa na waganga" so kuwa makini sana mkuu unapelekea sio pazuri hata kidogo.
Sitasema sana subili watakuja watu kukupa ushuhuda, halafu mtu kumloga mtu mwingine sio lazima awe mganga, hao waganga nlokuwekea sifa wapo wengi sana
 
ivi bado mnaenda kwa waganga? Kwa kifupi waganga wa kweli walisha kufa wamebaki wajukuu ambao wamejirithisha uganga.

mganga wa kweli hana nyumba nzuri...ukimkuta mganga mwenye maisha mazuri hapo shituka utapigwa bill ndefu huto amini.

mganga anae kwambia ili qkutibu lazima umpe zaidi ya 100,000/= 🤣🤣🤣​
 
Mganga toka pande zote za wataalam nipo hapa, wazazi wangu ni watu wa kigoma, mie nimezaliwa pemba, nimekulia sumbawanga, nimeolea tanga, bibi yangu ana asili ya kusini huko.

Niko fiti kalikiti..
Sio tapeli Mshana Jr mganga yoka lini akawa mchaga.. Mganga anakunywa mbege.. Mganga anaoenda VINYEO aahh, vileo 😂🤣

Mshana Jr Kaka nakusalimia mkubwa wangu, mzee wa vinyeo aahh.. VILEO. Vidole vinateleza leo. 😂🤣😂
 
Back
Top Bottom