Njia ipi nzuri ya kumtoa mtu kwenye uraibu wa imani ambayo sio sahihi?

Youngblood

JF-Expert Member
Aug 1, 2014
18,967
55,070
Habarini Great thinkers wote.

Lengo la uzi si kumtoa mtu kwenye imani yake

"Religion is an opium" sote tunakumbuka hii tulisoma kipindi cha sekondari,tena namkumbuka yule mwalimu wangu wa GS pale shuleni.Hii sentensi sio tu kwenye religion hata kwenye kuamini vitu mbalimbali.

Ili maisha yaweze kuwa na maana lazima mtu awe na kitu cha kuamini, waislamu wanaamini wataenda peponi, wakristo vivyo hivyo,wengine wanaamini wakifa watafufuliwa tena, wengine wanaamini ukifa ndio basi tena. Kile mtu anachoamini akilini mwake ndio kinakuwa foundation ya kila kitu anachofanya hapa duniani,kwamba matendo yake yote atafanya ili aweze kutimiza malengo ya imani yake.

Imani inawemfanya mtu aamini kitu kimoja kwa kiwango ambacho kitafanya asiamini vitu vingine ambavyo haviendani na kile anachkiamini.Muda mwingine wengine wanaenda mbali zaidi mpaka wanafikia hatua ya kuona wengine ambao wana imani tofauti na wao kama maadui au wanepotea(extremist,msimamo mkali)

Katika jamii tunayoishi kila mtu ana imani yake na vitu fulani.Mfano wakristo,waislamu,wahindu etc.
Lakini sote tunafahamu kila kitu lazima kifanyike kwa kiasi fulani (na usahihi) laa sivyo kinakuwa kama Addiction au hatari kwa maisha ya muhusika.

Kipindi nasoma Sekondari kuna mshikaji wangu alikuwa vizuri tu form ,ila mpaka anafika form six urafiki wetu ulikufa baada ya yeye kuwa amejiingiza kwenye imani above average,alikuwa anashinda msikitini,analala huko,ansomea huko,na matokeo ya form six hakufaulu.

Mbaya Zaidi mtu ambaye yuko kwenye Imani fulani ni ngumu sana kumuelimisha au kumrudisha kwa njia ya kumuelewesha kwa maana kwamba imani yake inamwambia yeye yuko sahihi kuliko wewe.

Mfano.Kuna watu huwaambii kitu kuhusu mwamposa, wale wanaojitoa muhanga,Mackenzie,Kibwetere,ijapokuwa unajua kabisa wamejazwa imani mbaya au wanatapeliwa,kibaya zaidi watakushawishi wewe uungane nao pindi unapojaribu kuwaelimisha.

Swali,Je ni njia gani inafaa kwa ajili ya kumtoa mtu huko?
 
Kila mmoja ana Imani yake na kuingilia Imani ya mtu inataka uwe mtu wa kuingilia yasiyokuhusu

Kama ulivyosema sio tu dini hata ulevi pia
Kumuambia mtu acha pombe jibu lake atakuambia unaninunulia?
Nini kifanyike kama mtu ni mlevi na ulevi unaathiri maisha yake mwenyewe,lakini bado anaona kama kulewa ni uhuru wake?
 
Kwahiyo unataka kuwabadilisha watu wote Duniani waishi kama Malaika? Mbona unajipa kazi ambayo hata Mitume waliishindwa?

Pitia huu uzi nadhani utapata mantiki ya swali langu
 
Pitia huu uzi nadhani utapata mantiki ya swali langu
Angalia maisha yako,ukifuatilia maisha ya wengine utachelewa sana au unaweza usifike kabisa,Mind ur own business.
 
Nadhani ungejikita kwenye mada ingekuwa vizuri sana.
Kunishambulia mimi sioni kama ni sahihi,zaidi inaonyesha uko mwepesi kama karatasi kichwani
Mada ya kijinga kama ulivyo wewe upstairs,utaweza kuwacontrol watu wadunia nzima? Wenye imani za dini,walevi,watumia drugs,wauaji....Hivi upo sawa kweli wewe?

Nchi kubwa Duniani mpaka leo zinahangaikia hayo mambo na hazijaweza.
 
Wapi nimesema nataka ku control watu wote duniani kwenye huu uzi wangu?
Nimezungumzia mfano watu wanaojitoa muhanga,wanaimani kwamba kile ni kitu sahihi kwao, lakini upande mwingine wanauwa watu wasiokuwa na hatia wanapotekeleza matendo yao hayo,swali langu ni kwamba ni namna gani inaweza kufanyika ili kumnusuru mtu asifanye hivyo?

Je hapo nimesema kitu kibaya,au nimetaka ku control watu wote duniani?
 
Kumbe huelewi hata ulicho post hapa,
Hao walevi au wenye imani ya dini hawapo Dunia nzima? Hao wauaji hawapo Dunia nzima? Binadamu hawafanani,ndio maana kuna Pepo na Moto kwa wenye kuamini.
 
Back
Top Bottom