Niulize chochote juu ya tiba za Mitishamba

Tutafute na dawa bora ya mitishamba inayotibu hiki kitu kinaitwa UTI .. huu ugonjwa umekuwa maarufu sana na unaumiza wengi kila uchao
Ningeshangaa kama nisingeona comment yako kwenye huu uzi.

Yaan baada ya kuona heading tu nikasema ngoja nitafute comment ya mshana kisha nirud kuusoma.
 
Tutafute na dawa bora ya mitishamba inayotibu hiki kitu kinaitwa UTI .. huu ugonjwa umekuwa maarufu sana na unaumiza wengi kila uchao
Hapa kwenye UTI ni suala la uelewa pia.Unaweza kufikiri ni muathiriko kwenye njia ya mkojo tu,kumbe ugonjwa umeshapiga hatua mbele.

Mfano wanawake wengi hupata maambukizi katika njia zao za mkojo,lakini maambukizi hayo hupelekea kupata fangasi sugu inayoweza kusababisha hata maambukizi katika mji wa mimba (PID),sasa mara nyingi wanapopima katika maabara hizi za kawaida huonwa na bakteria katika mkojo lakini secondary problem iliyoletelezwa na hao bakteria huwa haionekani kirahisi.

Wanaume hubeba bakteria hao kwa njia ya kujamiana na inakuwa kama magonjwa ya zinaa na dalili ni zilezile endapo ugonjwa utakomaa,utawashwa kwenye mshipa wa uume,utatokwa uchafu mweupe na wakati mwingine utapata shida ya kukojoa huku homa kali na unyonge vikikuandama.

Kwa wanawake suala linapofika hatua kubwa uchafu utaanza kutoka sehemu za siri na utaambatana na harufu mbaya,na inaweza kupelekea uchafu kuwa wa kijani alert ambayo ni mbaya zaidi kuna uwezekano wa kansa.

Kama mtu yuko kwenye ndoa na ana tatizo hili ambalo sasa imezoeleka ni UTI lazima mme na mke watumie dozi wote vinginevyo ni kujitapelivmwenyewe. Zipo dawa za mitishamba ambazo husafisha kabisa matatizo haya.
 
Mpata kufa ni dawa bora ya UTI
Watu hawasemi tu,ila tulioko kwenye fani hii ni ndiyo tunajua maana tunawasaidia wahitaji kila mara.Mbunye nyingi za wanawake zinaandamwa na harufu na uchafu mwingi kiasi kwamba ndoa ni changamoto tena.Jamani msiogope tiba zipo.Maana watu wameshachoma sindano mpaka wakatuliza ball maana baada ya muda tu kitu kinarudia.
 
Hapa kwenye UTI ni suala la uelewa pia.Unaweza kufikiri ni muathiriko kwenye njia ya mkojo tu,kumbe ugonjwa umeshapiga hatua mbele.Mfano wanawake wengi hupata maambukizi katika njia zao za mkojo...
Mkuu hizo dawa za mitishamba zinazosafisha kabisa ndio mimi nazihitaji.

Nazipataje?
 
Tutafute na dawa bora ya mitishamba inayotibu hiki kitu kinaitwa UTI .. huu ugonjwa umekuwa maarufu sana na unaumiza wengi kila uchao
Mkuu Mshana Jr. Bado Tuko kwenye Oktava ya Mwaka mpya 2022. Happy New yr.🤣 aithee.

Huo mti uliooneshwa hapo kwenye picha wenye maua makubwa mekundu SIO Mjafari.

Mjafari huku Umasaini ni mingi sana na Unaitwa Oloisuki. Baadhi ya makabila wanauita Mlungulunguani, Wahehe wanauita Mkhunungu. Unamatumizi-dawa mengi sana.

Majani yake machanga huweza kutumika kama mboga(Mlenda). Matunda yake yaliyokomaa yanafanana sana na pilipili manga. Hukaushwa na kusagwa na hutumika kama Tangawizi kwenye chai- hutibu matatizo ya kifua kinachobana. Mizizi yake iliyokaushwa na kusagwa hutumika kutibu maumivu ya viungo/mifupa ikiwepo arthritis, mgongo, kiuno n.k. n.k.

Mti huo picha yake ni hii hapa:
Angalia maua yake yalivyo ni tofauti na yale mekundu katika picha iliyooneshwa. Picha (Mti) uliyooneshwa wenye maua makubwa mekundu huku Umasaini tunauita mti huo Olng'aroji.

IMG_20220107_094940.jpg


IMG_20220107_094920.jpg


IMG_20220107_094741.jpg
 
Back
Top Bottom