Nitazungumza na Watanzania kuomba ridhaa ya kuwania Urais

Status
Not open for further replies.
Kila la heri dogo, kaza buti ila uzoefu ndani ya chama chako ni kasoro ya kwanza.
 
Mwigulu Nchemba umesafisha mdomo wako na moyo wako uliojaa matuzi kwa dawa gani . Wakati wa uchaguzi mdogo wa madiwani Arusha mjini maeneo ya Kijenge Chini kwenye mkutano wa kampeni wewe na Shoza ulitutukana matusi ya nguoni eti kwa sababu tunaonekana ku support Chadema. Uliwafananisha wananchi wa Arusha na mitetea inayopandwa na Jogoo.

Bado tunakumbuka saaana na ilituuma sana na kwa hiyo hatuoni kama wewe busara zinakutosha kuwa rais. sisi tunakufananisha na makondakta ambao wakiwa barabarani wana mwagika matusi lakini Jumapili wako kanisani wakijidai watakatifu.
Moyo wako umejaa matusi tena mabaya na sioni ni kwa nini upoteze muda kutudanganya kuwa unaweza kutuongoza
 
Last edited by a moderator:
Wewe sio presidential material,hivi kwa matusi uliyowahi kutoa bungeni unafikiri una hadhi tena ya kuwa rais!Don't waste your time
 
Itisha kura ya ndy au hapana hapa jf..uliza: je mi mwigulu nafaa kua raisi wa nchi hii?majibu yatakupa mwelekeo,nchi hii sio ya wajinga bali ni ya wasomi!!
 
Nakupa big up, kwanza wewe ni msomi, pili nimeona baadhi ya mambo yaliowashinda wengi umejitahidi kuyafuatilia japo wizarani, ila kuna maswali nasikia kutoka kwa wadau ati, mara kuhusika kwenye mabomu, mara kupanda kwa dola na kushuka kwa thamani ya shilingi, naomba uwajibu wadau kwa hayo wakati unatoa hiyo hotuba yako, otherwise nakusupport unajua kujenga hoja.
 
Serikali haiwezi kumtegemea mtu mropokaji,Lissu hana sifa ya kuwa kiongozi kwakuwa na hulka chafu ya uropokaji na ukurupukaji.Nasema tena japo mm bado ninayo kadi ya cdm lakini Laana ya kumtukana mtu mwenye umri mkubwa kuliko baba yake Itamtafuna tu.Huwezi kmtukana mtu mkubwa mwenye mchango mkubwa kwa taifa lako tena tayari ni marehemu halafu ukasalimika.
Huna hoja...............ILA MASUALA MENGINE NIKO SAWA!!
Lissu kwa taarifa yako serikali inamtegemea katika kutatua mambo tata ya kisheria......Fuatilia escrow na mambo mengine bungeni jinsi serikali inavyomsikiliza Lissu.
Muulize zitto aliposhinda na kuwa mbunge wa mahakama alafu kibao kilipokuja kumgeuka alafu kwa sasa ulizia taarifa zake anapatikana wapi
 
kwenye top 5 lazima atapita,mwigulu,ngoma itakua kwenye mchakato wa mwisho,na wakicheza anaweza kupenya

Kwenye siasa kila kitu kinawezekana ..nakumbuka kwenye siasa za marekani 2008 Hilary ndie aliyekua na mtandao Mkubwa ,pesa za kutosha lakini kijana mdogo na asiyekua na pesa na mtandao Mkubwa akamshinda nguvu ya ushawishi Hilary na mwishowe akawa Rais
 
Mtu hauna hata uwaziri unawaza urais, huku si kupotea njia kama sio kuchanganyikiwa kabisa?

Utendaji hata katika chama upo very low, ndio maana ukaamua kuikimbia aibu yako kwa kujiuzulu, urais ndio utauwezea wapi?

Ulichofanikiwa mpaka sasa ni kukwapua wizarani na kuwanunulia magari masalia ya CHADEMA, kuchukua rushwa kwa wahindi kupitia kivuli cha EFD, pamoja na kushusha thamani ya shilingi yetu na kuipandika dola ya kimarekani maana ww ndio wakala hao hapa nchini na unataka kuiuza nchi kwao.

Wewe bakia na ubunge wako tu, haya mengine waachie watendaji wenye maamuzi magumu, ya msingi na sahihi.
 
Mwigulu Nchemba

Mabadiliko yako kwa AKAWA tu na ndo tumain la Watanzania kukombolewa kutoka kwa wakoloni weus, wenye lindi la umaskin haliyakuwa Nchi yao inautajiri wa Rasilimal tulizona.

Mafisad wa ccm ndo wanazozifaida rasilimal za Nchi hii, sasa ni wakat wa ccm kupumzika mmeshindwa kuwaletea Maedeleo wananchi ndan ya miaka 53,
Oct ndo mwisho wenu.
 
Last edited by a moderator:
Nitazungumza na Watanzania kutoka Makao Makuu ya Nchi-Dodoma, Mazungumzo yangu nanyi yatajikita kuomba ridhaa ndani ya Chama ya Kugombea nafasi ya Uras wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Tukiwa tunaianza safari ya Kuelekea Miaka 50 tena ya Taifa letu, Naomba usipitwe na Mazungumzo yangu yatakayokuwa LIVE kupitia Redio na Televison Mbalimbali hapa Nchini.

Siku ya Jumapili, Saa 9 Alasiri hadi 12 Jioni, Chuo Cha Mipango Dodoma.

Ukumbi: Mwl.Nyerere Hall "

WAKATI NI SASA,MABADILIKO KWA VITENDO"
hongera kwa kutumia haki ya kikatiba vizuri, maoni yangu ni kuwa ukiacha siasa za maji taka unafaa kuwa waziri mkubwa na sio urais kwa sasa.
 
Muheshimiwa

Kuliko LOWASA bora WEWE mara MIA

ila usisahau ajenda ya UFISADI, AJIRA NA UCHUMI

kILA LA HERI!!
 
Nitazungumza na Watanzania kutoka Makao Makuu ya Nchi-Dodoma, Mazungumzo yangu nanyi yatajikita kuomba ridhaa ndani ya Chama ya Kugombea nafasi ya Uras wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Tukiwa tunaianza safari ya Kuelekea Miaka 50 tena ya Taifa letu, Naomba usipitwe na Mazungumzo yangu yatakayokuwa LIVE kupitia Redio na Televison Mbalimbali hapa Nchini.

Siku ya Jumapili, Saa 9 Alasiri hadi 12 Jioni, Chuo Cha Mipango Dodoma.

Ukumbi: Mwl.Nyerere Hall "

WAKATI NI SASA,MABADILIKO KWA VITENDO"


Wale vijana wanaoandika jina lako pembeni mwa barabara, kwenye mawe na na sehmu nyingine, kuwa Mwigulu Nchemba Rais 2015, umewatuma wewe? kama umewatuma unawalipa sh ngapi kwa kazi ile ngumu?
 
Nitazungumza na Watanzania kutoka Makao Makuu ya Nchi-Dodoma, Mazungumzo yangu nanyi yatajikita kuomba ridhaa ndani ya Chama ya Kugombea nafasi ya Uras wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Tukiwa tunaianza safari ya Kuelekea Miaka 50 tena ya Taifa letu, Naomba usipitwe na Mazungumzo yangu yatakayokuwa LIVE kupitia Redio na Televison Mbalimbali hapa Nchini.

Siku ya Jumapili, Saa 9 Alasiri hadi 12 Jioni, Chuo Cha Mipango Dodoma.

Ukumbi: Mwl.Nyerere Hall "

WAKATI NI SASA,MABADILIKO KWA VITENDO"

Tunaokufahamu tunasema unafaa sana wewe ni mtu wa vitendo,nasi watanzania tunahitaji mabadiliko ya vitendo.Kila la kheri brother,najua hii ni ndoto yako tangu ulipokuwa Mazengo sekondari.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom