Nitamwambiaje mchumba wa zamani kuwa sitomuoa tena

Kuwa mkweli tu tena wala usipoteze muda. Haya mambo yanayotokea duniani kote na yanafanywa na jinsia zote na wewe siyo wa kwanza. Itakuwa vizuri kuwa naye ana kwa ana kama una ujasiri wa kufanya hivyo.

Thanks Bubu nashukuru kwa ushauri wako, lakin huyu mtu yuko mbali kwaiyo kuonana itakuwa ngumu zaidi ni kumpigia simu maana tuko nchi tofauti but thanks very much
 
Hajui tunaishi nchi tofauti na ata hivo mawasiliano hayakuwa mazuri kw kipindi kifupi tu km 3 months hivi

Ati?:confused:

Lapse ya 3 months mkuu! Ukaondoa uvivu na kuvuta kitu ingine heheheeeeee!

Wewe kweli chiboko!:eek:

Well naomba utafute kamba yako wewe mwenyewe ya kujinyongea! mti tuna:mad:weza kukuchagulia!:mad:
 
Thanks Bubu nashukuru kwa ushauri wako, lakin huyu mtu yuko mbali kwaiyo kuonana itakuwa ngumu zaidi ni kumpigia simu maana tuko nchi tofauti but thanks very much

Hapo huna jinsi inabidi kuongea naye kwa simu tu. Kila la heri katika maisha yako ya ndoa.
 
Kamanda we kama mwanaume kweli ukafanya maamuzi magumu kumwacha binti uliyemuahidi kumuoa ukachukua mwingine sema wazi kwanini ulimwacha na kwanini umemuoa uliye muoa? Uliye muoa ana nini kumzidi wa mwanzo? kwanini ulifanya siri?

Sikiliza yafuatayo.
1. Mtafute mwenyewe mkae mahali mweleze kuwa hutamuoa.
2.Kuwa makini kwasababu wadada huwa haraka kuzimia na akifa utasaidia polisi upelelezi na lazima unyee ndoo mahabusu kwa kuua bila kukusudia na mzuri uliyemuoa hutamlala watamlaa vijana mtaani.
3. Mweleze mkeo kuwa ulikuwa na mwanamke kabla yake na hukumwambia habari hiyo ili akushauri nanma kumwacha. Atakusaidia wanawake wana mbinu hasa anapokupenda atafanikisha umwache huyo unayetaka kumwacha japo ulichofanya si nzuri na usirudie.
4. Tuambia kilichokufanya umwache ili tukushauri vizuri, nini tabia zake za ndani mpaka umwache je harekebishiki? Je utafanya nini kama tabia ulizokimbia kwa huyo utazikuta kwa kifaa kipya naye utamwacha? Tafakari, chukua hatua!
 
BAK Kirahisi namna hiyo ;)

1st lady huyu jamaa yuko nje ya nchi na inaelekea ex wake yuko Bongo. Kwa maoni yangu kufunfa safari kwenda kumwambia fiancee wako kwamba mimi na wewe basi nimeshapata mrembo mwingine pia kwa taarifa yako nimeshaoa naona kama imekaa kushoto. Sijui lakini maana binadamu tunatofautiana katika maamuzi yetu. Vingineyo ex anaweza kusema kwamba yuko tayari kuwa nyumba ndogo ;) furaha ya njembas wa bongo, unakula huku na unakula kule pia! Maisha raha mustarehe :)
 
Hivi Bubu umeoa babu?

Vipi OPP, una dadaako unataka kunioza? Anajua kupika Ugali, Pilau, Chapati, Wali mweupe wa nazi, Sambusa, Mahanjumati ;), Ndizi mtori kwa kutumia nazi na mafuta na mchuzi mzito wa kuku uliotiwa giligilani? Kama unaye basi we nipigie cross tu mambo yakijipa basi utakuwa Bwa' Shemeji :) tena kwa heshima na taadhima ;) Dini yoyote ile miye sina tatizo….JF itakuwa imetuunganisha kwa kiwango cha juu kabisa ;)
 
Habari zenu wana jamii!
Unamwambiaje mchumba wako wa zamani kuwa hutofunganae ndoa tena? kwasbb umeshaoa naombeni mchango wenu!

I reserve my comment, maana pressure imepanda...nadhani bht na Ama wamerepresent vilivyo.

Question - Have you also told the one you have married kwamba ulikuwa na mchumba? In reality you have deceived 2 women... Na usisingizia sijui eti ishu ya nchi tofauti.

Payback time...veeeeeeeeeeery soon...life is like that
 
Habari zenu wana jamii!
Unamwambiaje mchumba wako wa zamani kuwa hutofunganae ndoa tena? kwasbb umeshaoa naombeni mchango wenu!
ulipoteza mawasiliano naye kwa makusudi ili tu upate nafasi ya kuoa mwanamke mwingine kwa kisingizio cha kutowasiliana, hapo kwanza tambua umefanya uhuni na ufisadi wa ahadi kwa mwenzio, kikubwa ulikuwa na tamaa, hata hivyo una nafasi kumwambia kwa ujasili wemye upendo ndani kama uliotumia kumtongoza hapo awali kuahidi ahadi za Ki-CCM
 
Haya mambo jamani yanatokea mara nyingi na duniani kote. Unapokutana na mtarajiwa ambaye ana sifa zaidi kuliko yule uliyekuwa naye mwanzoni basi hakuna ubaya wowote wa kubadilisha mawazo na kuamua vinginevyo. Kwanini uendelee na yule uliyekuwa naye wakati huyu mwingine moyo wako unampenda zaidi? Kwani huyu alifungwa kamba kwamba ni lazima amuoe huyo mchumba wake wa kwanza?
 
BAK Mkuu
unapkapoint mahali nilimwagia wino ila ...
 
Haya mambo jamani yanatokea mara nyingi na duniani kote. Unapokutana na mtarajiwa ambaye ana sifa zaidi kuliko yule uliyekuwa naye mwanzoni basi hakuna ubaya wowote wa kubadilisha mawazo na kuamua vinginevyo. Kwanini uendelee na yule uliyekuwa naye wakati huyu mwingine moyo wako unampenda zaidi? Kwani huyu alifungwa kamba kwamba ni lazima amuoe huyo mchumba wake wa kwanza?

..........BAK ni kweli yanatokea, ila ni bora kama mtu umeamua kuoa msichana mwingine umwambie ukweli yule wa mwanzo. Sasa huyu kaka kaoa bila kumtaarifu mwenzio, huyo mdada maskini anamsubiria huyu kaka kuja kumuoa kumbe mwenzake alishaoa.
Huyu kaka kafanya ukatili wa hali ya juu, angemwambia mapema binti wa watu ili na yeye achukue ustaarabu mwingine. Utakuta huyu dada anapata wanaume wengine huko tena wa maana anawakataa na kumsubiri huyu aliyeoa.
 
Mrembo Pretty, jamaa yetu labda ilikuwa ngumu kwake kuanza kumwambia ex wake kwamba mimi na wewe basi, ndiyo maana kaja kutafuta msaada hapa jamvini maana kwa jinsi anavyomfahamu kila akipanga maneno ya kumwambia labda hayapangiki na hii kitu inawashinda wengi sana wengine hutuma hata Wazazi au ndugu wa muhusika kwa kuogopa muhusika anaweza kuamua kuchukua hatua mbaya zaidi.
 
Kama ulikuwa hujashiriki naye tendo la ndoa na umekiri ulimwahidi kumwoa basi lazima umemfanyia kitendo cha kinyama. Pili, nini kimekupelekea kumwoa huyo binti unayesema "naye anasifa ya kuwa mke", fafanua ni sifa zipi hizo ambazo zinakingana na huyo wa zamani.

Linc
 
Linc asante sana nimekusoma, ninaposema ata huyu wa ss ana sifa ya kuwa mke namaanisha ni mke mwema pia kitabia maana urembo ni majaaliwa tu, na si kwamba yule wa mwanzo alikuwa na tabia mbaya hapana ata hivo sijawahi kuwanae karibu kiasi cha kuwa ata tabia yake siifaham zaidi! na ukweli ni kwamba mke mwema anatoka kw mungu kwaiyo naamini huyu ndio chaguo la mungu kwangu, mana hakuniforce nimuoe wala sikuforce kumuoa! jamani uchumba wa distance ukizid miaka 3/4 hamjaonana na hamfahamiani zaidi yanakatisha tamaa
 
Ni mchumba ambae sijadate nae hata once ila alikuwa mchumba tu kwa kuwa namuona binti na nampenda, lakini sijashare nae mapenzi naomba nieleweke! zaidi ni sms na kupigiananae simu tu

Sasa hapo ugumu wa kumwambia ukweli uko wapi? Mpigie simu mueleze ukweli najua unaogopa kumuuza lakini tayari umeshaowa mwengine hauna jinsi. Good luck
 
Back
Top Bottom