Elections 2010 Nitaifanyia nini tanzania-shirki kulinda kura kama wakala

Jatropha

JF-Expert Member
Apr 9, 2009
1,151
199
Kwa zaidi ya miaka mitano wapenda mabadiliko tumekuwa tukiapashana habari, kubadilishana uzoefu n.k kwa kutumia njia mbali mbali ikiwemo jamii forum. Kwa hakika kupitia jf tumenufaika sana na kuelimika kwa kiwango cha juu sana.

Sasa umefika wakati wa kila mmoja wetu kutimiza wajibu wake popote alipo. Wajibu huo ni kupiga kura na kulinda kura za chadema nchi nzima. Jukumu la kulinda kura za chadema ni letu sote. Hivyo wakati wa kukaa hapa jf na kuchonga umekwisha, kila mmoja wetu anatakiwa kujiunga na kikosi cha mawakala wa chadema popote alipo ili kusaidia katika ulinzi wa kura.

Utafiti unaonyesha ni vigumu sana kuiba kura pasipo kumshirikisha wakala katika kituo cha kupiga kura. Baada ya mawakala kukubali ndipo wapiga kura mamluki hutumika kupiga kura katika vituo ambavyo mawakala wamekubali kufanya hujuma.

Mawakala wakikubali ndipo kura zenye kumpendelea mgombea fulani huingizwa katika masanduku ya kura katika kituo/vituo hivyo. Mawakala wakikubali ndipo matokeo ya mgombea/wagombea fulani hupunguzwa na wengine kuongezewa.

Hivyo ni muhimu sana chadema kuwa na mawakala wenye elimu, upeo, uwezo na maadili ya kuweza kusimamia ukombozi. Na idadi kubwa ya mawakala wa aina hii haiwezi kupatikana bila ya wapenda mabadiliko wenye sifa hizo kujitolea (kuvolunteer) kuchukua majukumu hayo.

Ipo aina ingine ya mawakala ambao hukaa nje ya vituo kwa ajili ya kuwasaidia wapiga kura wasiojua kusoma na kuandika, wasioona na wenye ulemavu wa aina mbali mbali. Hawa nao ni muhimu sana kuwepo wa kutosha katika kila kituo kwa ajili hiyo.

Aina ingine ya mawakala wanaohitajika ni wale wakulinda barabara zote zinazoingia katika eneo husika ili ccm isisombe watu kwa magari, pikipiki na usafiri wa aina ingine yoyote kwa ajili ya kupiga kura.

Ni muhimu mawakala wa aina zote wakawa wamejitayarisha kimawasiliano, wakiwa na vyanzo mbali mbali vya mwanga, kuwa na maji na vyakula vyao wenyewe na mahitaji mengine kwa ajili ya kujitayarisha na hali yoyote itakayoweza kujitokeza katika vituo vya kupiga kura kama vilie kukosekana taa, umeme, kuweza kuwasiliana na viongozi na wagombea n.k wakati wote wa upigaji kura , kuhesabu na kutangazwa kwa matokeo

mawakala wanapaswa kuhakikisha kuwa katika kipindi hiki pia wanaepuka kula kula na kunywa kunywa ovyo ili kupunguza haja ya kwenda haja za aina mbali mbali na kutoa mwanya hujuma kufanyika.

Kwa mujibu huo idadi ya walinzi wa kura wanaohitajika katika kila kituo, mtaa, kijiji, kata. Jimbo n.k ni kubwa sana. Hivyo kila mmoja wetu anayetaka kuona uchaguzi huu unatupatia mabadiliko tunayoyakusudia ni lazima awasiliane na uongozi wa chadema katika eno analoishi kwa ajili ya kujitolea kushirikia katika ulinzi wa kura.

Chdema kama chama kimetimiza wajibu wake ipasavyo kwa kutayarisha wagombea na kuwasimamisha, kutayarisha ilani, sera na hptuba ziazokubalika kwa wananchi wengi, kufanya kampeni ya nguvu na ya kutosha n.k

kilichobaki ni watanzania kupiga na kulinda kura ili kuleta mabadiliko. Iwapo tutashindwea kutimiza wajibu kila mmoja weti popote alipo ili kukabiliana na mafisadi amabo sote tunajua wana mbinu mbali mbali kujihakikishia uhakika wa kuendelea kutunyonya. Tutakuwa hatuna wa kumlaumu ili sisi wenyewe kwa kushindwa kutimiza wajibu wetu.

Kama moshi mjini, tarime, kigoma, mpanda na kwingineko walikopiga na kulinda kura ipasavyo na kupelekea chadema kuibuka kidedea mwaka 2005. Wale tulioshindwa kutimiza wajibu wetu 2005. Sasa tumepata fursa ingine ya kufanya mabadiliko/

mungu ibariki tanzania!!!!!!!!!!!!!!!

Tunaomba wale wapenda mabadiliko wenye mbinu mbali mbali za wizi wa kura vituoni, tunawaomba waendelee kutumwagia habari hizo ili tujitayarishe ipasavyo kulinda kura zetu.
 
Mbinu mojawapo itumikayo ni kuweka mawakala mamluki wa vyama vingine. Mnaweza kuwa mawakala 16 kumbe mawakala 15 ni wa chama kimoja, hivyo kuwapa mwanya mkubwa wa kufanya hujuma endapo wakala 1 aliye pekee atatoka kwenda haja au kula akiamini kuna mawakala wenzake wa vyama vingine watalinda kura. Wakala wa Chadema inabidi asimwamini wakala mwingine yeyote wa chama kingine hata kama ni wa chama cha upinzani.
 
kwa jinsi thread hii ilivyopata wachangaji wachache sana, niana hakika kuwa watanzania bado hawajajua umuhimu wa kujitolea na kujitoa. Hivyo kila mtu anataka kureap the benefits of changes lakini hawataki kutake part in the process of bringing that change. Ndio maana speculators wengi wanajiunga ccm hata kama katika mioyo yao hawaamini wahat is being preached by ccm nad its leaders. What keeps them together is personal interests.
 
kwa jinsi thread hii ilivyopata wachangaji wachache sana, niana hakika kuwa watanzania bado hawajajua umuhimu wa kujitolea na kujitoa. Hivyo kila mtu anataka kureap the benefits of changes lakini hawataki kutake part in the process of bringing that change. Ndio maana speculators wengi wanajiunga ccm hata kama katika mioyo yao hawaamini wahat is being preached by ccm nad its leaders. What keeps them together is personal interests.

Mtoa mada inabidi atoe ujumbe mfupi uliobeba maana kubwa maana threads ziko nyingi hiii yake ina ujumbe however isn't user friendly though
 
Back
Top Bottom