Nitagombea Urais - Kisandu Deogratius

Marais ni wengi sana, yaani kuna rais wa TFF, FIFA, AKUDO IMPACT nk. Mnakaribishwa pia kugombea huku! Sifa mtu asiye na makundi,aahaa aha!
 
Jk kafanya URAIS kuwa URAHISI..
Hv mtu uwezi kuchangia maendeleo/mabadiliko ya nchi hadi uwe Rais

ukichangia unaambiwa hurusiwi hiyo ni mali ya sirikali ndo maana tumemsusia mkuu wa kaya kama mtu anatakuchimba madini anaambiwa hapo pana muwekezaji huoni hicho ni kikwazo..
 
BILA KUJARIBU HUWEZI KUFANIKIWA.
by KISANDU

Unapofikiria jambo lolote na kuliamini kichwani kwako, ni rahisi kulifanikisha lakini kikwazo kikubwa ni namna ya kulifanikisha hilo lengo lililo kichawani kwako. Sababu kubwa ya kushindwa kukamilisha ni imani unazokuwa nazo kichwani kwako, unapoona watu wengine wakifanikiwa unaanza kujiuliza kwa nini huwezi kufanya hivyo.

Wakati mwingine unaanza ...kutafuta watu wa kukupa mawazo ya namna ya kufanikiwa malengo yako lakini bado unashindwa kubadili maisha yako.

Sababu kubwa inaweza kuwa unafanya mabadiliko ya mawazo yako lakini unaendelea kuishi katika mai¬sha ya kutofahamu nini cha kufanya.

Hii ni kwa sababu unakuwa na ufahamu kichwani kwako lakini mawazo yanajawa na mifumo ya kiimani kuwa huwezi kufanikisha.
Njia kuu ya kufanikiwha malengo yako ni kuwa na uwezo wa kuhamisha ufahamu wako na kufikiria zaidi kule unakotaka ufanikiwe na kuondoa mawazo ya hapo ulipo hivi sasa.

Hii ina maana kuwa ni muhimu utulie na kuondoa misongo yote ya mawazo yanayotokana na na kufanikisha malengo yako ili uone mafanikio ya kweli.
Unatakiwa uwajibike kwa hali hiyo laini unapojiona kuwa wewe ni muathirika wa hali hiyo unaweza kuona maisha hayajakutendea haki.
Hali hiyo inapokuathiri unaweza kujenga tabia ya kulaumu badala ya kufikiria mabo ambayo yanaweza kuwa ni manufaa kwa mafanikio yako.

Unapokuwa na hali hii, utajikuta unamlaumu kila mtu kwa kile kinachokutokea na hivyo kujiweka katika mawazo ya kutoweza kufanya jambo lolote la mafanikio katika maisha yako.

Pia mtu hujiona maisha yake yamejawa na mambo mabaya yanayo mfanya ashindwe kufikiria malengo ya maisha yake.
Kumbuka akili yako inafanya kazi kulingana na wewe unavyo itumia, kama utaijaza imani zisizofaa, utai¬zuia kutoa matokeo mema yaliojaa mbinu za kukamilisha malengo yako.

Kwahiyo ni vizuri kuacha kufikiria kuwa ungefanikiwa kama usingekumbana na vikwazo katika maisha yako.

Kama umejawa na woga huwezi ukawa na uwezo wa kufikiria kwasababu utaamini kuwa kuna jambo linakutawala wakati ni wewe ndiye unatakiwa kutawala mazingira yako..

Uchaguzi uko kwako kwa kila unachohitaji, lazima uchague kutotawaliwa na jambo lolote na badala yake wewe ndiye utawale maisha yako.

Unapokuwa katika safari ya kuelekea mafanikio unaweza kufikiri kuwa utachukua miaka mingi sana kufikia mafanikio hayo.

Na unaweza kufikiria kuwa changamoto ni kubwa sana na vizingiti vinatisha kiasi cha kukuongopesha kufikia mafanikio hayo.

Hata hivyo, unatakiwa kuchukua hatua kidogo kuelekea katika lengo unalolihitaji na hapo utaanza kuona fursa nyingi zikijitokeza.

Hapa pia utakumbana na vikwazo vingi na utalazimika kuvizoea na kuvifanyia kazi ili uwe na uelewa wa namna ya kukabiliana navyo.

Jaribu kuepuka mawazo yoyote yasiyo na msingi ili kukwepa kukwamishwa katika harakati zako za kusaka mafanikio katika maisha.

Ni muhimu kufikiria zaidi katika kile unachotaka kufanikisha katika maisha yako kwa kuwa unachofikiria ndiyo hicho unafanya.

Kama unafikiria mafanikio katika maisha yako basi ni wazi kuwa asilimia 100 ya mawazo yako yatafani¬kiwa, kwa hiyo ni uchaguzi wako kufanya hivyo au la.

Unaweza kujiona umeshindwa kama hutajaribu lakini kama unaifanyia kazi unaweza kubadili kushindwa kwako kuwa mafanikio.

Hata ukimfikiria mtu yeyote aliyefanikiwa ni lazima utagundua kuwa mtu huyu alijaribu zaidi ya mara moja nahatimaye kayaona mafanikio.
 
Wanajamvi kwenye uchambuzi wa Magazeti Star TV Asubuhi kuna habari kwenye gazeti la Majira ya Katibu wa BAVICHA-CDM Mkoa wa Tanga Deogratius Kisandu naye ameungana na Zitto Zuberi Kabwe kutangaza nia ya kuomba ridhaa ya kugombea urais kupitia CDM.

Kwa mujibu wa Kisandu anaamini ana sifa zote za kumwezesha kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

My Take:
-Urais sasa umekuwa rahisi kiasi kwamba, kila mtu anaweza kuutaka bila hata kufanya utafiti wa kutosha kuona ni kwa kiwango gani anakubalika si tu ndani ya CDM bali pia miongoni mwa Wananchi.
-Vijana wa CDM wanahitaji kufundwa sasa maana picha inayo onekana ni ya uroho wa m adaraka tu miongoni mwao.
 
CDM wanatumia strategy hiyo ili kui-water down hoja ya kipuuzi ya Msaliti Fisadi Zitto

Mkuu sidhani kama umakini wa chadema unaweza kudondokea kwenye ku-meltdown hoja ya uraisi kwa aina hiyo! Kwa mwenye akili timamu ushauri wa mzee mtei ndio wa kufuatwa kwa sasa, haya mengine ni watu kutaka kutafuta tu press coverage ili kusafisha nyota, watu wanacho kihitaji kwa sasa sio lundo la majina ya wagombea urais au fulani ana m-support nani, mwanachadema/wana chadema wanatakiwa kuunganisha nguvu ya pamoja kueneza elimu ya uraia ili watu wa vijijini wazidi kuamka na kumrahisishia mgombea atakaye chaguliwa kwa utaratibu (sio anaye jitangaza kwenye media)urahisi wa kupata kura nyingi.

Ukiipima support ya Kisandu ina ka ukame wa maono ndani yake, yeye aligombea ubunge kupitia chadema jimbo la Lushoto, lakini pamoja na Shekifu kuwa hakuwa chaguo
mujarabu kwa wana lushoto bado aliendelea kupata na yeye kushika nafasi ya pili, alichotakiwa kukifanya ni kuangalia changamoto alizo kumbana nazo ili ziwe mbadala kwa raisi ajaye, na moja ya changamoto hata yeye anaijua kuwa ni kuto kufahamika vizuri kwa watu wa vijijini hivyo akaonekana kama mgeni wa kuja na kura zikisha pigwa atatokomea.

Tunahitaji vuguvugu la mabadiliko zaidi ya kujitangaza na ku-support watu kuwa wana faa au hawafai kuwa maraisi! Wapo walio uhemea uraisi kwa mbio za farasi hata kuitwa machaguo ya Mungu. Je wanacho kifanya ndio mapenzi ya Mungu yanayo mgusa kina mwana dongo la Tanzania?!

Uraisi sio makalio kuwa kila mtu anayo au anaweza kuyaona ya mwingine.
 
cdm watoe mwongozo wa haya matamko sasa tuahitaji utulivu na kufocus kwenye m4c
 
cdm watoe mwongozo wa haya matamko sasa tuahitaji utulivu na kufocus kwenye m4c
ndugu kwani wewe hujawahi sikia mwenyekiti mbowe akisema wazi wazi kuwa haongozi kundi la wagombea uongozi anaongoza kundi la ukombozi
 
Molemo, kuna mtu mwingine huku naye anautaka urais.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu sidhani kama umakini wa chadema unaweza kudondokea kwenye ku-meltdown hoja ya uraisi kwa aina hiyo! Kwa mwenye akili timamu ushauri wa mzee mtei ndio wa kufuatwa kwa sasa, haya mengine ni watu kutaka kutafuta tu press coverage ili kusafisha nyota, watu wanacho kihitaji kwa sasa sio lundo la majina ya wagombea urais au fulani ana m-support nani, mwanachadema/wana chadema wanatakiwa kuunganisha nguvu ya pamoja kueneza elimu ya uraia ili watu wa vijijini wazidi kuamka na kumrahisishia mgombea atakaye chaguliwa kwa utaratibu (sio anaye jitangaza kwenye media)urahisi wa kupata kura nyingi.

Ukiipima support ya Kisandu ina ka ukame wa maono ndani yake, yeye aligombea ubunge kupitia chadema jimbo la Lushoto, lakini pamoja na Shekifu kuwa hakuwa chaguo
mujarabu kwa wana lushoto bado aliendelea kupata na yeye kushika nafasi ya pili, alichotakiwa kukifanya ni kuangalia changamoto alizo kumbana nazo ili ziwe mbadala kwa raisi ajaye, na moja ya changamoto hata yeye anaijua kuwa ni kuto kufahamika vizuri kwa watu wa vijijini hivyo akaonekana kama mgeni wa kuja na kura zikisha pigwa atatokomea.

Tunahitaji vuguvugu la mabadiliko zaidi ya kujitangaza na ku-support watu kuwa wana faa au hawafai kuwa maraisi! Wapo walio uhemea uraisi kwa mbio za farasi hata kuitwa machaguo ya Mungu. Je wanacho kifanya ndio mapenzi ya Mungu yanayo mgusa kina mwana dongo la Tanzania?!

Uraisi sio makalio kuwa kila mtu anayo au anaweza kuyaona ya mwingine.

Hivi ndani ya Chadema ni marufuku kutangaza kugombea urais sababu urais sio makalio kila mtu anayo?
 
haya sasa, wale walokuwa wanamponda zito wako wapi?
Mtei atoe tamko lingine.
 
haya sasa, wale walokuwa wanamponda zito wako wapi?
Mtei atoe tamko lingine.

Kuna mwingine humu anasema urais sio makalio kila mtu anayo, naona anampiga madogo Dr Slaa.
 
Back
Top Bottom