Nitagombea nafasi ya Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Shinyanga

Wewe jamaa bado unasumbuliwa Na stress??
Hata mwezi haujIsha tangu uweke bandiko hapa la kuihama CCM!!
 
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI NA UMMA WA TANZANIA KUHUSU KUGOMBEA NAFASI YA MWENYEKITI WA CCM MKOA WA SHINYANGA.

Ndugu Watanzania wenzangu tunaopenda Amani na Haki ya Taifa letu katika Demokrasia na ukweli thabiti, mimi Deogratius Nalimi Kisandu leo natangaza Rasmi kuwa nitagombea nafasi ya Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Shinyanga pale vigezo vitakapo kidhi.

Binafsi ni mzaliwa wa mkoa wa Shinyanga wilayani Kahama, kijiji cha Busoka inyembe, ninaijua Shinyanga vizuri sana na viunga vyake vyote, kisiasa mkoa wa Shinyanga bado unahitaji viongozi tajirishi wa Chama Cha Mapinduzi katika kutajirisha fikra mpya za kuweza kupambana na mabadiliko ya fikra kwa rika zote ili kufikia CCM Mpya tunayoitaka.

Nafasi hii ya Mwenyekiti wa mkoa kwangu ni kama fadhila ya kuwatumikia na kuwajenga upya wana Shinyanga wenzangu ili tuwe imara katika kupambana na ujio gandamizi kutoka upinzani. Nitaifanya Shinyanga kuwa Mpya kwa kila idara ndani ya CCM na nitawaunganisha Vijana wote mkoa mzima na kina mama, sambamba na wazee, aidhaa nitazibiti mifumo mibovu ndani ya mkoa inayoweza kuyumbisha chama chetu na mkoa wetu kwa ujumla.

Nina uzoefu mkubwa sana wa kuongoza vyama si tu katika maandishi bali pia katika matendo, nimekuwa kiongozi wa vyama vya upinzani katika ngazi za Taifa mpaka za wilaya kwa vyama tofautitofauti na ili hali sasa ni mwanachama wa CCM, ni na uhakika wa kufanya vizuri zaidi tapopewa dhamana hii kuongoza mkoa. Wasukuma tunamsemo wa kujengana usemao “ulu uding’wa, dimanaga gete” yaani unaposhikwa shikamana, hivyo nina uhakika wana shinyanga wenzangu mtanishika vizuri katika nafasi hii ya uenyekiti wa mkoa. Naamini kwa nafasi hii sitafanyiwa fitina kabisa na wala shetani hatapata mwanya wake tena, hivyo nitaitumikia vyema nafasi iliyoachwa wazi na Ndugu Mgeja.

Sina mengi sana zaidi nahitaji sapoti yenu watanzania wote ikiwemo kunisapoti kiuchumi niweze kuchukua fomu ya kugombea nafasi hiyo na mchakato mzima na Mungu atawabariki sana.

MWL. Deogratius Nalimi Kisandu.

Mtumishi Mdogo Sana wa Mungu

Mwanachama Mvumilivu wa CCM.

29/12/2015
Kisandu mbona unahangaika sana?? Kwani kile chama chako unachokipigania kianzishwe umeona hakifai ama umeona idea imefail??

Ila Mwalimu kwa cv yako hadi ya kufundisha tuition na kusahihisha mitihan ya form Two kwa ufupi huna sifa
 
Napata Mashaka na watu wanaotoka katika hii kanda.Japo ni Watani zangu lakini nikikumbuka ya Shibuda,wewe kisandu na Huyu ..... Nashindwa kuwaelewa
 
kuna mgonjwa wa akili alilazwa hospitali ya wenye matatizo ya akili Mirembe,akawa chumba no. 25.
baada ya miaka 2 akaruhusiwa kurudi nyumbani baada ya madaktari kuona amepona.
ilipopita miezi 3 akapiga simu kule Mirembe na kumuuliza nesi aangalie kama chumba no.25 kina mgonjwa.
alipoambiwa kuwa hakina mgonjwa akajibu: sawa nilikuwa tu nataka nipate uhakika kuwa kweli nimetoka au bado niko humo!
 
Mkuu,
Inawezekana nimechanganya jina, Sio wewe nilikusoma hapa unalikuwa kwenye mkakati wa kuanzisha chama cha siasa?!
 
Mtemi Nailimi Kisandu
Salam,
Sisi wanachama tarajiwa wa chama unachokiasisi cha ACU tunakuliza kulikoni?
Ndio umeshakimbia chama chetu?
 
Back
Top Bottom