Nitaendelea kuongoza CHADEMA wanachama wakiamua - Mbowe

Ukomo wa uongozi ni jambo bora na lenye demokrasia kwa ngazi yoyote katika chama cha siasa na hata chama cha kuweka na kukopa. Kama hakuna watu wengine wanaoweza kushika nafasi kubwa katika chama, basi hapo kuna udhaifu mkubwa kwa viongozi waliokuwepo. Katiba za vyama vyote hususan vya siasa ziwe na vipengele vya ukomo wa uongozi.

Naomba na ningependa Kamanda Mbowe aache legacy na kuingiza ama kupendekeza kipengele hiki katika katiba yao...kama bado kuna nafasi ya kufanya hivyo!!
 
Ubinafsi na njaa ya madaraka vimekumaliza mbowe

Hana tofauti na idd amin, mugabe, museveni, gadafi, na madikteta wengine uwajuao

Atachaguliwa na mtei

Hapo ndo anaharibu kabisa huyu, kama ndo kasema hvo basi zzk kaonewa!

Bora uwe masikini wa mali kuliko akili na fikra ni umasikini mbaya sana lkn kwa sasa muda wenu mchache uliobaki R.I.P CDM :A S-confused1:

nimejitoa cdm rasmi leo kwa kuchoma kadi niliyochukua moshono arusha mwezi may mwaka jana,rip cdm nilikupenda ila udini ukabila na ukanda umekupenda zaid

Nilishasema hapa mkanitukana na maneno yenu ya kejeli!Mbowe hafai kuwa kiongozi hata wa kijiji bali mhamasishaji wa muziki!Haya sasa kazi kwenu Mugabe Huyoo ndani ya bongo

KWA HIYO YEYE HAFUATI KATIBA?DICTATOR HUYO.akafie mbali
Azote, Easymutant, Mangandula, Nchaby ..tunalazimika, Mangandula, simbilisi, FaizaFoxy, and fyonko like this.
Simbilisi hawa bado wako msalani
 
Hivi niulize Mbona Prof. Lipumba na Maalim Self ni Mwenyekiti na katibu respectively kwa miaka mingi toka nikiwa Shule Primary na sasa Nimemaliza Chup kikuu. Hapa Kuna kitu Kimejificha na CCM ilitaka Kusambaratisha CHADEMA.
Hakuna aliyepata kuzuiliwa asigombee uenyekiti CUF kama alivyozuiliwa Zitto na baba mkwe wa Mbowe. Uchaguzi uliopita huyo kada wenu aliyekuwa anatangaza kujiondoa CUF kila mwezi kwa miezi sita mfululizo naye aligombea nafasi akaja kushindwa kwa kura (alipata kura zisizofika hata 1%). CUF hawajapata kuwa na katiba ya chama iliyoweka vikomo vya muda wa kuongoza. Chadema walikuwa nacho lakini kikaondolewa ili mkwe aendelee kushikilia madaraka.
 
Ndio tatizo hapo kwenye ukomo! Kwa nini uongozi usiwe na mwisho? Mbowe aache siasa za zamani

Tuambie ni chama gani chenye ukomo wa uongozi kwenye katiba yake.ccm yenyewe yenye mabalozi wa mashina mengi hadi kwenye mbuga za wanyama, wanaosaidiana na jangili kinana kuua tembo kule ndio haina kipengele hicho sembuse chadema inayojijenga huku ikiwa na watu wachache wenye sifa barabara za kufiti kwenye uongozi? Acha hizo bana!
 
Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe amesema ataendelea kuwa Mwenyekiti wa Chadema endapo kama wanachama wataendelea kumhitaji.

Kiongozi huyo mwenye ushawishi mkubwa ndani ya chama chake amesema kamwe chama chake hakizuii watu kutamani uenyekiti lakini akatahadharisha zitumike njia za kidemokrasia na uwazi.Amesema katu Chadema hakitaruhusu watu kutumia njia za kihuni kinyume na Katiba.

Mwenyekiti huyo ambaye ni mhimili mkuu kwa chama chake ameshangaa watu kukimbilia madaraka kwa njia ovu na za kihuni.Amesema kuongoza upinzani si lelemama na wala si wa kukimbiliwa.Amesema kuongoza upinzani ni kukubali kufungwa,kupigwa mabomu na kuzushiwa kila kashfa kila uchao.

Kiongozi huyo amesema kwamba kamwe hawatakubali Chadema kusambaratishwa kwa njia yoyote.

Kuhusu Ukomo wa uongozi amesema Katiba ya Chadema haina kipengele hicho kwa ngazi yoyote na kama mtu anafaa wanachama wataendelea kumchagua bila kujali muda atakaokuwa ametumikia chama.

Source:Nipashe Jumamosi.


Sasa kama hakuna ukomo wa uongozi WANA HAJA GANI YA KUHUBIRI DEMOKRASIA??

MTEINISIMS AT ITS BEST LEVEL...!!
 
Sikuwa nimejua, kumbe hakuna kipengele cha ukomo wa madaraka?
Basi huu ni udhaifu mkubwa wa chama tulichokiamini, na ambacho tunategemea kituingize nchi ya ahadi, ijaayo maziwa na asali. Bado naipenda chadema. Ila kipengele hicho kirekebishwe haraka iwezekanavyo, maana inalea udikteta. Tuna marais watatu Tz waliostaafu, tusifikiri walikuwa hawapendwi, bali ilifika ukomo wao, hata kama walikuwa wametufaa sana. Mfano mzee wa uwazi Ben Mkapa, pamoja na makasoro ya ubinafsishaji holela, alitufaa sana.
Mbowe tafadhali usijifiche kwenye kipengele ambacho labda kwa makusudi hamkuweka, ama mlikisahau. Ukomo wa madaraka ni muhimu uwepo. Wapo watu wengi wenye uwezo. Inapendeza hata kutazama ukiwa pembeni. Ebu jaribu hili Mbowe. Kumbe ndio maana kuna vifujo fujo. Mbowe tunakupenda sana lakini muweke ukomo ili tumwone na mwingine .... Hivi na kwa katibu mkuu ndo the same thing? Ndo maana ZZK alianza harakati za chini kwa chini kuwaondoa.... sio vizuri hivyo. Tumewaamini. Hadi sasa pamoja na makasoro yote, hakuna chama kingine cha upinzani cha kuitoa ccm madarakani, na kutuletea ukombozi, isipokuwa Chadema, ila msiendelee kutuhuzunisha kwa hili bwana. Ukomo wa madaraka ndo demokrasia yenyewe. Mnataka kuwa kama Ghadafi, Museveni, Mugabe? Mbona tutaingia choo cha kike?
Mkuu kipengele hicho kilikuwepo lakini kikatolewa kwa uhuni. Ukisoma huo waraka unaodaiwa umeandaliwa na Zitto wanaeleza kuwa wakati wanajadili kurekebisha katiba hawakupata kujadili kipengele za ukomo wa uongozi lakini ilipochapishwa katiba mpya hicho kipengele kikabadilishwa. Sasa unaweza kuwaamini uongozi wa watu wanaofanya uhuni wa namna hii kuendesha vyama vyao? He wakipewa nchi itakuwaje?
 
Jukwaa libaki kuwa jukwaa, hadhiyake inakubalika, ghilba uongo uzandiki na usanii usanii wa taarifa hautatusaidia kufahamu hatma ya nchi
 
Kuna swal dogo sana la kujiuliza anaye mchagua mwenyekit ni nani? Kama ni wananchama kinachowaumiza watu vichwa ni nn? Kama bado cdm inamhitaji mbowe watamchagua la atakaa pemben. Uchaguz wa cdm ni 2014 leo mbowe kang'ang'ania madaraka yep? Then hakuna kitu kinanikera kama kuskia chama kina udin, kwa hiyo ili watu wakukubal lazima uwe mkristk au muislam? Watu wnakera humu mpaka bas
 
Back
Top Bottom