Nitabaki na mke wangu na wanangu, kumbe ndugu ni kenge tu

Tupo duniani ili kuishi na si kupata mafunzo; we ukiona kenge yeyote hayuko upande wako, piga chini na usonge mbele na wale wanaotambua umuhimu wako.
 
Mbona ungewaza hili wakati unamuoa ungekua mbali sana?! Hivi, ni kwa nini kwa wenzetu waliosogea kimaisha,hizi biashara za uroho wa mali hawanaga? Utakuta mke na mme wanakaa kwa wazazi,na huchukuliwa kama watoto nyumbani,hakuna cha ajabu. Vitu vyote, huwekana sawa.
Huku,wakija tu, majungu yanaanza sijui uchawi,mali, nini na nini.

Ila kuzaliwana na umasikini kichwani na kwenyewe shida. Mtu unakaa unasubiri ndugu yako akate upepo ndo upate. Kweli? Mkewe na watoto watajua wenyewe,akifa nyumba na mali ndugu wagawane. Bulshit
 
Hata watoto wako wanaweza wasiwe upande wako

Naamini Ndugu wa kweli wakati wote kama hukuingia chakike wakati wa uchaguzi ni MKE/MUME wako.

Watoto wanaolewa wanabadilishwa
Watoto wanaoa wanabadilishwa

ila MKE/MUME kama ulicheza karata zako vizuri ukachagua aliekuchagua mkachaguana Huyo ndio Ndugu pekee ulienae hapa duniani.

Mpende/Muheshimu Mkeo/Mumeo

Lakini pia usisahau kutimiza wajibu wako kwa watoto wako ila usiwe na mategemeo makubwa toka kwao.

Pole Mkuu.
 
H
Pole chief, sometimes ndugu ni viazi sana.. labda mama yako mzazi tu ndo anaweza kua mwema kwako, lakini ndugu wa kawaida mpaka baba yako mzazi anaweza kukupiga tu kwa hali yoyote ile
Hakika kuna madingi wanatuombea njaa mbak unashangaa huyu ni mshua kweli?
 
Ndivyo inavyokuwa, sasa jaribu kufumba macho uchukulie ndo umekufya, ingekuwaje ?

Weka kila kitu sawa japo kuugua siyo kufya. Andika kwa mwanasheria.

Niliwahi kupitia hiyo hali 😭😭

Hayo mahela yote hayo au ndo uliingia hilo chama la wana ?
 
KUNA WATU HAWANA SONI ILA NITAWAFURAHISHA, MNAJIITA NDUGU ZANGU KUMBE NI KENG*E TU!

Kama unavyojua familia za Kiafrika, mmoja akishatoka kimaisha basi unachagua na ndugu zako kuja kuwasaidia. Hiyo ndiyo ilikuwa kwangu, nilihangaika na maisha ya ndugu zangu mpaka wote wakamaliza chuo.

Bila mkopo nilisomesha wadogo zangu wanne, wamemaliza chuo suala la ajira sasa nikawa sina namna, sina connection, hawana kazi ila kila mmoja anahangaika na maisha yake mjini na mimi nikasema nahangaika na yangu.

Nimejitahidi nimejenga kanyumba kangu na kununua kausafiri kangu. Vyote hivi nafanya na mke wangu, yeye anafanya biashara mimi ni muajiriwa, hata pesa ya kuwasomesha kiasi kikubwa ilikuwa inatoka kwenye biashara yaani ni kama mke wangu ndiyo alisomesha ndugu zangu.

Si biashara kubwa ila imesaidia, mwaka jana mwezi wa tisa nilianza kuumwa, niliumwa sana nimelazwa hospitalini kuanzia mwezi wa tisa mpaka mwezi wa kumi na mbili.

Kila kitu nafanyiwa sijitambui, mke wangu alihangaika sana, ndugu mwanzo walikuwa na mimi lakini mwishoni alibaki mke wangu peke yake. Kutokana na kuhangaika na mimi ilibidi watoto kuwapeleka kwao.

Kumbuka nina ndugu zangu hapa Dar, maisha najua ni magumu lakini wangekuwa wameshindwa kuishi na watoto wangu hakuna mtu anataka kabisa, ila ndiyo hivyo kila mmoja alikuwa bize na kazi zake, mara sina mfanyakazi, mara sijui nini basi ikawa hivyo.

Nimetoka hospitalini nikiwa bado na hali mbaya, sema ni ile nimerudishwa tu, nadhani ni kama unaambiwa kafi*e nyumbani. Nimerudi mke anahangaika, mara dukani mara kuniuguza. Mara napata nafuu nashangaa ndugu wanakuja sasa, wanakuwa karibu.

Ni kama walikuwa hawaamini kuwa nitapona. Basi mimi nikawa sina shida ndiyo maisha, kama mwanaume unajua kuwa kupambana ni wewe na mke wako. Basi juzi wakati sasa naangalia vitu vyangu nakuta hati ya nyumba siioni.

Namuuliza mke wangu ananiambia hajui, kadi ya gari sioni, mke wangu ananiambia sijui. Nilipaniki sana nikahisi kuna binti wa kazi aliyekuwepo akaondoka nikajua ni yeye. Basi nikampigia simu kumuuliza, aisee nilichosikia!

Ananiambia mbona Shangazi, alikuja nyumbani na kuchukua kila kitu wakasema wanahifadhi kwa kuwa Mama anaweza kuondoka navyo. Kwa maana ya dada yangu mkubwa, ana ndoa yake, wamekuja na ndugu wengine, wakaingia mpaka chumbani kwangu.

Mke wangu yuko hospitalini eti nikif*a hawatapata kitu mke wangu anaweza kuvificha! Aisee, hasira nilizopata nikiangalia hata sijaka sawa wanangu hawana pa kukaa, aisee! Mke wangu kaingia madeni tena kwa ndugu zake hawa mbuzi wanawaza mali zangu!

Namfuata dada namuambia kuhusu vitu vyangu anajiuma uma, aisee nilichukua pang*a, nikamuangalia jicho moja alitoa kila kitu!

Halafu hawa Mbuzi wasio na akili sasa hivi wanatangaza mke wangu ndiyo kaniloga ndiyo maana nimekuwa makali, naomba uandike hapa wanakusoma waambie waache kuhangaika na maisha yangu maana nitawafurahisha kama wakitaka kumfanya chochote huyu mwanamke!

Nishamaliza nimejua rangi zenu! Yaani haka kanyumba ndiyo mnataka kuhangaika, dada hata kukaa na wanangu tu ili mke wangu ahanagike na hospitali ni shida wakati mtoto wako aliumwa nusu kuf*a mpaka nikauza pikipiki yangu ili apone, nasikitika Mungu nitakuwa sawa ila jueni tu kuwa haitakuwa sawa tena!View attachment 2862305

Too late, hii busara huwa inapatikana when it is too late
 
Pole sana mkuu Mungu akuponye ndugu lawama
 
Back
Top Bottom