Nissan Dualis: Msaada mwenye uzoefu na hili gari naomba ufafanuzi

Kweli kabisa atamimi nipo rafiki yangu alinunua kampuni tofauti na Toyota paka leo unaenda mwaka wa 6 hajawahi kubadilisha spear zaidi ya service ya kumwaga oil
Na ukijaribishaa magari tofauti na mjapanii hutojutiaa...
 
Habari wana JamiiForums, poleni sana na majukumu ya hapa na pale.

Kama kichwa cha habari kinavyojieleza, nimetokea sana kuvutiwa na kulipenda gari aina ya Nissan Dualis lakini sina information za kutosha husu ili gari so nimeonelea nije apa kwa wadau mana najua humu ndani kuna fani za aina mbalimbali na pia wapo ambao wanalitumia, washalitumia na wana details za kutosha kuhusu hii gari.

Ninachotaka kufaham ni:-
1- Ulaji wa mafuta ukoje,
2- uimara wa gari,
3- Engine ya gari inasumbua ama ikovizuri,
4- upatikanaji wa vipuri ukoje.

Karibuni sana wadau.
Kama umewahi kumiliki Nissan x trail, hii dualis wala isikutishe....
Japanese vehicles zinavaliana spea nyingi sana hususani spea za sehemu za siri...
 
Toyota ARV4?
Nina RAV4 kilitime tangu mwaka 2008 bado sijajutia.Pia nina Nissan Serena tangu mwaka 2015 nimebadilisha hydrolic (4l kwa 200,000) mara moja tu,mbali na oil sijagusa kingine chochote
General conclusion,
Gari lolote ni matunzo na kulijali..

kaNISSAN kangu sasa kana miaka 6 na miezi 2..
Mile age inasoma 157,600.. and the car Is running smoothly..

Kuna IST za washkaji zina less than 50,000 km.....lakini zinanguruma kama TATA..
 
Nissan ni kama simu za samsung, hizo ni gari za kiduwanzi sana ukinunua leo baada ya mwezi utakuja kuuza robo bei. Hiyo dualis mwaka jana ilikua ni milioni 23 -28 milioni, Nissan Qashqai iilikua 34-38 soko la leo ukiagiza japan mpaka kuiingiza barabarani dualis ni 12-14 milioni Qashqai ni 18M-20M. Extrail mpaka milioni 8 unapata kudaadeki gari gan hizo? Bado service yake ni gharama sana.
Tofautisha...

Si kila anayenunua ana wazo la kuuza kwa faida kama ilivyokasumba ya wwngi..
Wenginne wananunua magari wanayoyapenda, hawajalishi watakuja kuyauza bei gani..
 
Mkuu naongea kwa uzoefu. Wakati nimenunua gari yangu ambayo sio toyota, watu walinishangaa sana.. kuna jamaa alidiriki kunifata kabisa akaniambia aisee umeingia choo cha kike! Akaniambia hiyo sio gari bora ungenunua (akanitajia rundo la magari ya toyota).

Huu ni mwaka wa tano unaenda, gari haijawahi kusumbua chochote cha ajabu, spea nikifunga mara moja nasahau na nimeapa katika maisha yangu sitakuja kununua toyota! Kilichonifurahisha zaidi yule jamaa alienisimanga, yeye alinunua ARV4 ambayo tangu ainunue yenyewe inaishi gereji kila siku anagongea usafiri kwangu.

Ukiweza kuhama toyota ni ngumu sana kuja kurudi. Binafsi nilishasema bye 5yrs ago nasijioni nikirudi tena.
 
Kumbuka pia gari ni Asset... sasa unapochukua gari ya milion 35 alafu baada ya mwaka huwezi kuiuza japo hata kwa nusu bei.. inaleta frustration aisee . ILa kama ni la Pensheni after 30+ years of service ni sawa tu hahah

Mwambie huyo jamaa maana hajawaza interms of monetary value. Anawaza gari kama gari. Gari lazma iwe na resale value kubwa na ndo thamani ya gari inavyo pimwa. Kwenye post yangu Nilitoa mfano wasimu Leo iphone X lazma ununue kwa milioni moja laki tatu na Samsung note 9 note 8 hata kwa laki 3 unapata wakati simu zote zilitoka kipindi kimoja kwa bei linganifu. Leo toyota ist inathamani kubwa kuliko nissan xtrail pamoja na ukubwa wote ule, ist haiji kushuka thamani. When you choose a car angalia market value
 
Unanunua gari ili uuze au utumie? Kuna wanaokaa na magari miaka hata 8.

Kichwa chako kiko sawa?
 
Nissan ni kama simu za samsung, hizo ni gari za kiduwanzi sana ukinunua leo baada ya mwezi utakuja kuuza robo bei. Hiyo dualis mwaka jana ilikua ni milioni 23 -28 milioni, Nissan Qashqai iilikua 34-38 soko la leo ukiagiza japan mpaka kuiingiza barabarani dualis ni 12-14 milioni Qashqai ni 18M-20M. Extrail mpaka milioni 8 unapata kudaadeki gari gan hizo? Bado service yake ni gharama sana.
Unanunua gari ili uje uuze. Umaskini tabu
 
Unanunua gari ili uuze au utumie? Kuna wanaokaa na magari miaka hata 8.

Kichwa chako kiko sawa?
Vitu vingi tunanunua kwa matumizi binafsi ila kama hujawai kuuza kitu chako hata kimoja iwe ni kiwanja, electronics, mavazi, au furniture and etc basi hongera Mkuu ndugu na ntakubali hiyo *hukumu ya kichwa changu*.
 
Uko sawa mkuu...
Ila mpaka mtu awe na uwezo wa kununua gari la 35m nadhani huyu hana njaa ya kununua na kuuza....
ni kweli Mkuu sema njaa hainaga hodi si unajua watu waliokua na mipunga yao before 2015 wakaja kusombwa na vyeti feki saivi wapo mtaani wanatuuzia maziwa mtindi na waliokua na toyota zao ziliwasave kipindi kile cha mpito na wengine bado zinawasave mpaka sasa hasa waliokua Toyota Noah.
 
Mwambie huyo jamaa maana hajawaza interms of monetary value. Anawaza gari kama gari. Gari lazma iwe na resale value kubwa na ndo thamani ya gari inavyo pimwa. Kwenye post yangu Nilitoa mfano wasimu Leo iphone X lazma ununue kwa milioni moja laki tatu na Samsung note 9 note 8 hata kwa laki 3 unapata wakati simu zote zilitoka kipindi kimoja kwa bei linganifu. Leo toyota ist inathamani kubwa kuliko nissan xtrail pamoja na ukubwa wote ule, ist haiji kushuka thamani. When you choose a car angalia market value
Ndio namwelewesha huyu gari ni asset kubwa inayotakiwa kukusave kiasi flani utakapokua na need for quick money.
 
Kama nimeandika pumba sawa nunua nissan lakn ukija na uzi unalialia kwamba unaiuza humu na hupati wateja sisi tutaupita tu kama tunakanyaga mashimo hakuna atakae kua na interest nayo by the way
Sina biashara ya kuuza magari, likichoka nagawa
 
ni kweli Mkuu sema njaa hainaga hodi si unajua watu waliokua na mipunga yao before 2015 wakaja kusombwa na vyeti feki saivi wapo mtaani wanatuuzia maziwa mtindi na waliokua na toyota zao ziliwasave kipindi kile cha mpito na wengine bado zinawasave mpaka sasa hasa waliokua Toyota Noah.
Ni kweli mkuu njaa haina baunsa...ila kuna kitu kinaitwa mahaba.....na mali zangu nilizowahi kuuza ni laptop moja tu..

Binafsi mimi huwa napenda kitu kinachoufurahisha moyo wangu,

Huko mbele kikizingua mbeleni, tutaelewana mbele kwa mbele..

Leo nipo NISSAN, kesho usishangae nikiwa na Mazda japo Toyota Brevis na Crown nazikubali sana..
 
Nissan ni kama simu za samsung, hizo ni gari za kiduwanzi sana ukinunua leo baada ya mwezi utakuja kuuza robo bei. Hiyo dualis mwaka jana ilikua ni milioni 23 -28 milioni, Nissan Qashqai iilikua 34-38 soko la leo ukiagiza japan mpaka kuiingiza barabarani dualis ni 12-14 milioni Qashqai ni 18M-20M. Extrail mpaka milioni 8 unapata kudaadeki gari gan hizo? Bado service yake ni gharama sana.

Unalimiliki Mkuu? Tunaotumia nissan miaka na miaka tunakuangalia tu!
 
Back
Top Bottom