Nishaurini nisiumie tena jamani..

@ Madam T. Mimi ninajitahid sana kujishusha kwake ili tusiachane ila nawaza tena c unajua hawa kaka zetu wakishajua wanapendwa sana wanazidisha pozi na manyanyaso?

we yaelekea una nyodo sana,tena ningekua huyo jamaa,ningekupga chini mazima.
 
@ Seneter sio kwamba nina nyodo no ila tukiangalia ukweli wa maisha ya sasa wadada wengi wanalia kwenye mapenzi kisa Boy akishajua anapendwa analeta mambo ya ajabu.. Siko hivyo jamani.
 
tatizo lako hutaki kujinyenyekeza kwa mpenzi.kwa ufupi wewe unaendekeza ligi na ushindani..yaani akiacha kitu na wewe unaacha,akikata simu wewe unazima! Usipojilekebisha na kukesha ukitafuta gender balance nakuakikishia utatendwa hadi uchuje uwe na makunyanzi usoni. Ni hayo tu.
 
Umefanya vyema kuzingatia msimamo wako na kuondoka, ungeonyesha unyonge mkubwa sana kama ungebaki hata baada ya kutishia kuondoka. Ujue kila alichofanya alikuwa anakujaribu tangu simu ya mwanzo, tatizo hukugundua na hukuonyesha msimamo imara hata baada ya kuona hutoliwahi gari. Ile ya kwenda kumsaaidia kufua ungeipotezea, yy alikuwa anatakaa wende tu ukamuone na akusimulie mambo ya Club yalivyokuwa na kukupima kama uta-ract vipi. Sasa mie nakushauri, uwe na misimamo katika maamuzi yako, na hiyo itakujengea heshima, mfano punguza kupiga simu kwake, na usizime simu yako ukiwa huru iache tu akipiga msikilize. Na usikubali akuvute upande wa tabia yake: Acha utani ambao hauna maana, mjengee msimamo.
 
wewe hujui matumizi ya (aya, vituo, full stop, viulizo, mshangao!! )

Kwanza rudi shule ukasome haya matumizi za aya na vituo halafu ndio
uje jamvini kwani haisomeki hata kidogo halafu kwanini we uondoke kirahisi hivyo?
 
hahaha yani MKAROLINA hii habari yako jinsi ilivyo na uandishi wake nimejikuta naangua kicheko ..pole mdada..Naona wewe na mwenza wako mnapenda mizaha..
msamehe akusamehe muendelee na utani wenu wa kila siku..
 
We mkarolina ebu ni PM namba yako ya simu kwanza,ili nkushaur vzr.
 
Pole sana. Wewe 21 na mwenzako 24, mmekuwa wapenzi kwa mda gani? Mnapenda tamthilia gani?! Kwa picha ninayoona hapo nyie bado mpo kwenye maigizo, hata mkioana sasa ni comedy kwa kwenda mbele. Hadi hapo sijaona mwanaume, labda una mvulana unayejidanganya kuwa mna future pamoja.
 
People's minds are changed through observation and not through argument.
Will Rogers

COPY THAT .... KUWA MPOLE OMBA MSAMAHA ATAELEWA TU ..................
POLEE
 
@ Madam T. Mimi ninajitahid sana kujishusha kwake ili tusiachane ila nawaza tena c unajua hawa kaka zetu wakishajua wanapendwa sana wanazidisha pozi na manyanyaso?

Bwana kama unaona anakunyanyasa anza kamchakato kakutafuta mwingine mapema asije akakupotezea muda bure..siku ukija kuamua umri umeshaenda...pole lakini kama hutapendezwa lakini ndio ushauri wangu hasa wa kutoka moyoni... haya majitu hayatabiriki bwana..
 
Asanteni wote kwa ushauri wenu na nimeufanyia kazi mpaka sasa mafanikio niliyopata ni mazuri kwani kashanisamehe.MUNGU awariki wote na nilio waudhi mnisamehe.
 
@ Maganga Thread haijafungwa ila nimetanguliza shukrani ili kuonyesha kuwa mawazo yenu yamesaidia sana. Ila mpaka sasa nategemea ushauri zaidi utakao nikuza zaidi na zaid.
 
wote nyie watoto . . . Ila keti nae mzungumze kuoñdoa tofauti zenu. Msomane tabia ili msikwazane. Pia mmoja kati yenu ajishushe aanzishe mawasiliano.
 
Back
Top Bottom