Nishaurini nifanye nini?

TrueLove

Senior Member
Jan 12, 2012
124
37
Hodi humu ndani! Salamu wote wana Jamii Forum. Nianaomba msaada jamani.
MM nina Boyfriend wangu tumedumu kwa mwaka mmoja, tunapendana sana, na anaonyesha jitihada za kuwa na mm kama mke na mume, ameshanitambulisha kwa Mama yake, Dada zake na Kaka zake ila kwa kutumia simu kwan kwao ni mbali na tunapofanyia kazi kwahiyo umbali umechangia kuto onana face to face. Mara nyingi ndugu zake hao huwa wananipigia simu tunawasaliana na mm pia huwa nawapigia simu.
Mpaka hapo Mama yake anaonyesha upendo mkubwa sana wa mimi kuendelea kuwa na kijana wao. Ndugu wakinipigia simu wanakuwa wanani sihi sana kutulia na kumpenda kijana wao kwa moyo wote. Na mimi ki ukweli ninampenda sana kijana wao.
Week mbili zilizopita tulikutana kimwili na huyu Boyfriend wangu ambaye kwa sasa ni Mchumba mtarajiwa.. Baada ya siku kama tatu nikataka kumpima kama kweli anaupendo wa dhati kwangu au ni mambo ya ujana tu, nikamwambia nahisi kama nimepata ujauzito, kijana wa watu akaonyesha kufurahishwa sana na kauli ile akaniomba niende kupima ili niwe na uhakika kwan tupo wilaya tofauti hatuonani mara kwa mara, nikamwambia sawa nitaenda kupima, kesho yake nikampa majibu kuwa ni kweli nimepima na ninaujauzito. NILIKUWA NAMTANIA. Akaniambia sasa upendo wake kwangu umeongezeka mara dufu kwani anaamini nitakuwa mke wake.
Akampigia mama yake simu akamueleza juu ya jambo hilo na mama yake akamwambia basi hakuna shida atawaeleza baba zake wadogo ili wajiandae waje kwetu kutoa posa na taratibu nyingine za uchumba zifanyike ili tuoane mapema iwezekanavyo. Nikapigiwa simu na Mama yake akaniambia hongera mwanangu nimepewa taarifa zote na Mchumba wako kwa hiyo naomba usiogope sisi tunashughulikia swala la kuja huko kwenu.. Nilishtuka sana kwan Mchumba alikuwa ajaniambia kama amemwambia mama yake.
Na mimi nikamsikiliza mama yake mpaka mwisho. Swali langu je nimwambie mchumba kuwa nilikuwa namtania sina ujauzito? Na je atanichukuliaje? Na je wanaweza kusitisha zoezi la kwenda kujitambulisha nyumbani? Na mama yake atanionaje mimi? Nisaidieni mawazo ndugu yenu ntaumbuka mimi.
NB. Nilimtania ili kujua atachukua hatua gani baada yakujua mm ni mjamzito.
Ushauri wenu ndio silaha ya kuokoa ndoa hii itarajiwayo. Na Mungu atawabariki.
 
kila kona MAPENZI, watu kibao MAPENZI,dunia nzima MAPENZI? daah wat is this now?

okey usiwe unajaribu kutaniatania watu, jaribu kutafakari kwanza hasa kwa mtu aliyembali nawe.sasa angalia sijui utajiteteaje kwamba ulkuwa unatania,
ngoja waje wahusika wa hili jukwaa wakupe mambo mpaka mwenyewe utakubali, usikimbie tafadhali.
 
Kuna vitu vya kuita utani ila ulichofanya wewe sio utani. Vitu kama hivi hutakiwi kumwacha mtu akae nacho hata kwa masaa mawili achilia mbali siku nzima na ya pili juu kabla ya kumwambia ulikua unatania maana kama ni reaction yake umeshapata.

Kitendo cha wewe kuendelea kumwaminisha hivyo mpaka kesho yake alafu sasa hivi unasema 'sikujua angemambia mama yake' ni uzembe (nimetamani kutumia neno lingine ila ni kali zaidi). Nwy. . .jiandae kuwaomba samahani mana una kazi ya kumweleza mchumba kwamba ulikua unamtania, nae anakazi ya kumwelewesha mama yake kwamba alikua anataniwa , ambae nae anatakiwa awaeleweshe hao baba wadogo kwamba the whole thing was a joke. Kwa kitendo ulichofanya tegemea kutochukuliwa serious pale utakapokua serious. Anaweza akawa anaitika vitu ukimwambia ila akilini mwake havikai. Usishangae hata mama mkwe akipunguza ukaribu na wewe.

Kila la kheri.
 
Fanya fasta kutana naye mtengeneze mtoto manake wakigundua kuwa uliwadanganya watapoteza sana imani na wewe!
 
pole sana kwa kazi nzito iliyopo mbele yako,,, kwa vile yameshatokea tafuta njia ya kusovu! na wala usijilaumu! tl una chance ya kumconvice mchumba wako na akakuelewa,,,! tumia convincing power yako yote uliyonayo! ucichelewe kwani jambo litakuwa zito zaidi! bt next tyme kuwa makini
 
Kwana pole,ila nawe bidada hujui hata njia salama za kupima upendo wa mpnz wako?
Nakushauri fanya mpango wa kuipata hiyo mimba fasta kabla hujaharibu hali ya hewa,
Jaman jaribu kujiamin kuwa unapendwa,usiwe unapenda kufanya majaribio ya kiwango cha mapnz hakipo kbs dunian hasahasa utakuwa unajidanganya na kujipa presha bure na kuhatarisha mahusiano yako.
 
  • Thanks
Reactions: Sal
Thanx Dada Lizzy kwa ushauri.. ila bado nabaki njia panda kwamba je nikiwaambia ukweli watasitisha zoezi la kuja kujitambilisha nyumbani?

Kuna vitu vya kuita utani ila ulichofanya wewe sio utani. Vitu kama hivi hutakiwi kumwacha mtu akae nacho hata kwa masaa mawili achilia mbali siku nzima na ya pili juu kabla ya kumwambia ulikua unatania maana kama ni reaction yake umeshapata.

Kitendo cha wewe kuendelea kumwaminisha hivyo mpaka kesho yake alafu sasa hivi unasema 'sikujua angemambia mama yake' ni uzembe (nimetamani kutumia neno lingine ila ni kali zaidi). Nwy. . .jiandae kuwaomba samahani mana una kazi ya kumweleza mchumba kwamba ulikua unamtania, nae anakazi ya kumwelewesha mama yake kwamba alikua anataniwa , ambae nae anatakiwa awaeleweshe hao baba wadogo kwamba the whole thing was a joke. Kwa kitendo ulichofanya tegemea kutochukuliwa serious pale utakapokua serious. Anaweza akawa anaitika vitu ukimwambia ila akilini mwake havikai. Usishangae hata mama mkwe akipunguza ukaribu na wewe.

Kila la kheri.
 
Asante Mdau wala siwezi kukimbia ninahitaj njia ya kutatua tatizo

unia nzima MAPENZI? daah wat is this now?

okey usiwe unajaribu kutaniatania watu, jaribu kutafakari kwanza hasa kwa mtu aliyembali nawe.sasa angalia sijui utajiteteaje kwamba ulkuwa unatania,
ngoja waje wahusika wa hili jukwaa wakupe mambo mpaka mwenyewe utakubali, usikimbie tafadhali.[/QUOTE]
 
Nilitaman iwe hivyo ila sasa naona kama siku za kupata uwo ujauzito nao nitakuwa kazini kwan nipo mbali nae.

Ila ntajaribu kufanya hivyo kama nikipta ujauzito nitashukuru sana Mungu.
 
Asante. Ni kweli siku nyingine nitakuwa makini sana kwan nimeona madhara yake. Yani sina Amani nimebakai nawaza mpka nahisi kukonda.

pole sana kwa kazi nzito iliyopo mbele yako,,, kwa vile yameshatokea tafuta njia ya kusovu! na wala usijilaumu! tl una chance ya kumconvice mchumba wako na akakuelewa,,,! tumia convincing power yako yote uliyonayo! ucichelewe kwani jambo litakuwa zito zaidi! bt next tyme kuwa makini
 
Wewe kichwa maji kabisa jambo dogo hivyo. Mwambie hivi unaumwa tumbo, na baadaye neda kaongee na dokta akuandikie cheti kuwa mimba imetoka la sivyo, your going to die.

Mwambie ulikuwa kenye daladala watu wakakubana vilivyo, wakambana mtoto tumboni na mimba imetoka.

Baada ya hapo nenda Kanisani au Msikitini ukatubu

Byeeeeeeee
 
Shukran Mdau. Naomba uniweke kwenye maombi ili nitakapo kutana nae basi nipate hiyo mimba maana Mama Mkwe ndo kang'ang'ana na kubembeleza nijitahidi kula.

Kwana pole,ila nawe bidada hujui hata njia salama za kupima upendo wa mpnz wako?
Nakushauri fanya mpango wa kuipata hiyo mimba fasta kabla hujaharibu hali ya hewa,
Jaman jaribu kujiamin kuwa unapendwa,usiwe unapenda kufanya majaribio ya kiwango cha mapnz hakipo kbs dunian hasahasa utakuwa unajidanganya na kujipa presha bure na kuhatarisha mahusiano yako.
 
Wewe kichwa maji kabisa jambo dogo hivyo. Mwambie hivi unaumwa tumbo, na baadaye neda kaongee na dokta akuandikie cheti kuwa mimba imetoka la sivyo, your going to die.

Mwambie ulikuwa kenye daladala watu wakakubana vilivyo, wakambana mtoto tumboni na mimba imetoka.

Baada ya hapo nenda Kanisani au Msikitini ukatubu

Byeeeeeeee

nimecheka hadi peke yangu huku shambani.....mimba haina hata mwezi mmoja tayari kimeshakuwa na kufikia hatua ya kubanwa!!!?? hata zygote stage bado hakijamaliza!!!!

mpe ushauri mwingine huu haufai.....
 
Hili nalo neno. Asante kwa ushauri. Je nimwambie baada ya wao kwenda kujitambulisha au kabla? na kama ni kabla haiwezi kuleta delay ya wao kuendelea na process?

Karibu tena tafadhali.

Za mbayuwayu. Akili za kupewa changanya na zako....
 
Hili nalo neno. Asante kwa ushauri. Je nimwambie baada ya wao kwenda kujitambulisha au kabla? na kama ni kabla haiwezi kuleta delay ya wao kuendelea na process?

Karibu tena tafadhali.

Yani unataka kuendeleza uongo?

Shauri lako. . . . ngoja yaje kukulipukia ndio utashangaa.
Leo hii akikuoa ukashindwa kuzaa , mkaenda kwa wataalam wakasema haiwezekani wewe kupata mimba utajieleza vipi kuhusu iliyotoka ikiwa vipimo vitaonyesha huna wala hujawahi kua na uwezo? Je mpenzi wako akikutwa hana uwezo wa kukupa mimba utamwambia hiyo 'iliyotokaga' uliipata wapi?

Kua mwangalifu sana. . .usije ukaturudia hapa unalia.
 
KILAZA kweli ww!! siku ya mwanzo ulivyomwambia si uliona reaction yake? sasa ulivyopima ulitaka riaction ipi ya zaid!! badala ndio ungemwambia umepima umekuta huna ....... kama jamaa yako yupo mbali njoo mimi nipo karibu nikusidie kutengeneza mtoto wa kiukweli.
 
Shukran Mdau. Naomba uniweke kwenye maombi ili nitakapo kutana nae basi nipate hiyo mimba maana Mama Mkwe ndo kang'ang'ana na kubembeleza nijitahidi kula.
Usijali nitakuombea ila nawe ujiombee,
Cha kufanya piga hesabu zako vizuri ili uvizie siku muafaka ya kupata mimba na usifanye makosa kbs,
Yani ikiwezekana km jamaa yuko mbali msafirie umfate huko huko!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom