Nisaidieni ndugu zangu; napitia mateso wakati NSSF wanayo pesa yangu. Nachukuaje michango yangu?

mimi mtakatifu

JF-Expert Member
Oct 11, 2019
207
482
Sina kazi karibu mwaka wa pili sasa. Kula yangu ni ya shida pakulala ni shida kila kitu kimekuwa shida.

Nimekuwa na mipango mingi lakini nashindwa fanya lolote sababu pesa sina kabisa.

Lakini nina pesa yangu ipo NSSF baada ya kupoteza kazi yangu walinipa mafao ya 33% kwa miezi 6 then baada ya hapo sijapewa lolote.

Nimeandika barua kwa branch manager naambiwa kila nikienda nivute subira nitajibiwa lakini nazungushwa tu miezi sasa.
Nimeshakaa miezi zaidi ya 18 kwa nini hawataki kunipa pesa zangu jamani.

Mwenye ushauri, mbinu au connection anisaidie jamani maisha ni magumu yakiamua kukupiga hakuna ujanja utafanya.

Nisaidieni nadhalilika hapa DSM nipate pesa nifanye biashara au nifuge kuku.
 
Pole Sana! Ukiwashtaki Vipi hawawezi kujitafakari!

au Muungane Wawili watatu wenye Shida Zinazofanana Hlf Fungueni Mashtaka!

Mie Mwenyewe Wananikera Sana! Natafakari niwaibukie Vipi?
 
Pole Sana...! Ukiwashtaki Vipi hawawezi kujitafakari ..!

au Muungane Wawili watatu wenye Shida Zinazofanana Hlf Fungueni Mashtaka..!

Mie Mwenyewe Wananikera Sana! Natafakari niwaibukie Vipi..?
Mkuu hapa hata hela ya kula mgogoro nitawashtaki gharama nitatoa wapi
 
Una umri gani na kila mwezi ulikuwa unapewa kiasi gani na walikuambia ni nini hiyo ya kila mwezi na walikuambia itadumu kwa muda gani? Ukiulizwa jibu
Nina miaka 36... walikuwa wananipa asilimia 33 ya mshahara wangu niliokuwa napokea mara ya mwisho...hiyo walikuwa wanaita fao la kukosa ajira nililipwa miezi sita mfululizo. Baaada ya hapo nimekaa zaidi ya miezi 18 ambayo niliskia ukifikisha unapewa hela yako sasa hawanipi wananizungusha kuna dada pale akaniambia kuna barua za wenzako toka mwaka jana hazijibiwi mimi sina cha kukusaidia ni juu ya uwezo wangu dirisha namba 4 ubungo mnene mweupe
 
Pension schemes in Africa ni majanga tu, na kushauri kama hujapata kilema chochote na uko 36yrs, weka asilimia ndogo kupata hayo mafao yako, plz begin new life wewe bado kijana, utatomboa tu, wewe leta uzi wakutafuta mishe za kazi na weka cv yako, tukupe michongo ya kutoboa, you ur still younger Dude.

Kuna watu wamefilisiwa na mwendazake kwa wivu walikua 40s na 50s ila sasa hivi wameanza kusimama tena usiwe muoga wa naisha, achana na fikra za kukesha kwenye maombi unachelewa kuamuka kutafuta kazi, ulokole ni upuuzi wa hali ya juu
 
Huu ujinga upo Tanzania pekee. Wakati wa kuchangia sio hiyari, ni lazima. Lakini unapofika muda wa kuchukua pesa yako, wanatka uwabembeleze kijinga utafikiri pesa hiyo wanakupa msaada.
 
Sidhani kama scheme ni mbaya,ujanja ujanja wa watu wachache kutaka kujineemesha kwa kucheza na pesa za hiyo michango ya wanachama wake ndio umefikisha hiyo taasisi hapo ilipo,hili ni moja ya maeneo ambayo Raisi wetu anatakiwa kulivalia njuga ......
 
Toka wachukue kadi ya mwanangu kwa ajili ya kulipa likizo ya uzazi Ni miezi 6 Sasa..Nikifuata kadi yangu wananiambia Subiri utalipwa mara Pesa yako ipo tayari Mara lete benk statement..UKWELI NSSF WABABAISHAJI SANA.
 
Pension schemes in Africa ni majanga tu, na kushauri kama hujapata kilema chochote na uko 36yrs, weka asilimia ndogo kupata hayo mafao yako, plz begin new life wewe bado kijana, utatomboa tu, wewe leta uzi wakutafuta mishe za kazi na weka cv yako, tukupe michongo ya kutoboa, you ur still younger Dude.

Kuna watu wamefilisiwa na mwendazake kwa wivu walikua 40s na 50s ila sasa hivi wameanza kusimama tena usiwe muoga wa naisha, achana na fikra za kukesha kwenye maombi unachelewa kuamuka kutafuta kazi, ulokole ni upuuzi wa hali ya juu
Mkuu napenda sana kuanza upya ila sio rahisi ku-survive bila kuwa na kitu mfukoni. Hiyo pesa ningeipata nilikuwa naweza hata kuwa na factory ya kuzalisha chakula nna uwezo wa kuwa na mini supermarket au hata kununua babaj nizungushe chombo mwenyewe mjini uku hela nyingine naweka akiba.
 
Huu ujinga upo Tanzania pekee. Wakati wa kuchangia sio hiyari, ni lazima. Lakini unapofika muda wa kuchukua pesa yako, wanatka uwabembeleze kijinga utafikiri pesa hiyo wanakupa msaada.
Yani wanavyoringa na hizo pesa utafikiri sio zako unaenda kuomba msaada
 
Back
Top Bottom