Nipo tayari kujiuzuru endapo itathibitika-waziri wa miundombinu

Hahahahaaaa,,,,nafurahi sana umetumia lugha ya kifasihi,,,,,,,na wakishafanyiwa UPASUAJI WAENDE ICU
Si vizuri kuwahukumu hawa tu kwani uzembe wa viongozi wetu wote ndio utamaduni wetu. List ya ajali za barabarani zilizotokea Tanzania tangu MV Bukoba ni ndefu sana lakini utaona kuwa zote zinajirudia kila kukicha. Tiba ya ugonjwa wetu siyo kunywa apsirini na kuendelea na shughuli za kila siku, bali tunahitaji operation na kulazwa wodini kwa muda wa siku kadhaa kabla hatujaanza shughuli zetu tena.

Waziri wa miundombinu wa zanzibar hamad masud mh.Hamad Masudi amesema yupo tayari kujiuzuru
Sosi:bbc

anasubiri nini mpaka sasa? si apishe uchunguzi ikibainika hakuhusika katika usimamizi wake wa wizara atarudishwa?

aache mbwembwe huyo, tamaa ya uwaziri ndiyo iliyowafanya wakakubali serikali ya umoja wa kitaifa, kwani kwa nini hawakuhusisha na vyama vingine?

uroho wa madaraka, wala hakuna umoja wa kitaifa bali umoja wa CCM na CUF tu,

Anasubiria tume ? nini maana ya kujiuzuru sasa ?
Kama tume ikionyesha ana kosa , huyo si wa kujiuzuru tena , bali wa KUFUKUZWA

waambie maana wengine hawajui kuyatumia haya maneno. kujiuzulu ni hatua ya awali kupisha uchunguzi huru. uchunguzi huru ukifanyika ukiwa hujajiuzulu, kifuatacho ni kutimuliwa kazini au mwenyewe kuacha kazi kabla hujatimuliwa.

ni makosa makubwa sana kusubiri mpaka utajwe, ukitajwa utatoka kwa aibu kuu.

Je huu ni utamaduni wa watawala wetuuuu,,,,,wee jana hujasikia wakipongezana??????

waambie maana wengine hawajui kuyatumia haya maneno. kujiuzulu ni hatua ya awali kupisha uchunguzi huru. uchunguzi huru ukifanyika ukiwa hujajiuzulu, kifuatacho ni kutimuliwa kazini au mwenyewe kuacha kazi kabla hujatimuliwa.

ni makosa makubwa sana kusubiri mpaka utajwe, ukitajwa utatoka kwa aibu kuu.

Bro,hatuna utamaduni huo,,,yeye kasema anasubiri TUME,na iwapo tu atatajwa kwenye taarifa ua TUME

Ndio maana nikatoa maoni niliyotoa ili kuvunja huo ukuta wa "hatuna utamaduni huo". Hatuna utamaduni kwa sababu vyeo kwetu si dhamna bali ni "mtaji kutokana na ajira chafu".

Ni mangapi hayakuwa utamaduni wetu na leo tumeyakumbatia? Au ni kusema tunaiga yale tu ya kukosa heshima kama mavazi, heshima kwa wazazi n.k?

Kwa mtu mwenye heshima na haya zake, kwa tukio kama hili anajiondoa hata kama hakuhusika moja kwa moja, anajiondoa kwa sababu hakubaliani na mfumo wa kulindana, anajiondoa ili kupisha uchunguzi huru. Kwa mtu mwenye utu na heshima zake anaona aibu kwa tendo analolifanya mwengine.

• Thanks
Reactions: SMU
Sidhani kama suluhisho ni yeye kuondoka,nafikiri serekali inatakiwa kufanya jambo zaidi ya kufukuza watu na kuwafunga..

Maana halisi hasa ya kujiuzulu ni kuheshimu na kukubaliana na utawala wa sheria,hivyo timiza wajibu wako kwa maana halisi ya uwajibikaji. Kama dhamira yako inakusuta basi hapo inabidi ujiuzulu. Lakini kama utasubiri uchunguzi na halafu ukakutwa na hatia basi hapo si kujiuzulu tena ila itakuwa umewajibishwa kwa kufukuzwa kazi.

Mh waziri ni muda muafaka sana huu wa kujiuzulu na wala usingoje hadi ufanyike uchunguzi. Onyesha ukomavu wa kisiasa kwa chama chako cha CUF na serikali ya mseto (CCM + CUF). Chukua hatua mh waziri.

NOTE:
Usisahau kuacha kutumia huduma za vodacom, tena utangaze hadharani kwani wameidharau sana Zanzibar hawa jamaa wa vodacom. Nakuomba sana mh waziri paza sauti yako ya juu mataifa yoote yakusikie, hapo utakuwa umeacha angalau historia ya kufanya watu wa Zanzibar wakukumbuke kwa hilo. Paza sauti kubwa na unene kwa kuwaambia wazanzibar wakataeni vodacom kwa kitendo chao cha dharau. Kataeni kiabisa kutumia huduma zao.

Kwenye hili la mwisho asisahau pia kuwaambia wananchi jinsi CCM ilivyowadharau Wazanzibari kwa kuzindua kampeni Igunga siku ya Jumamosi. Wasiishie kuikomalia Vodacom pekee bali waikatae pia CCM kwa kitendo chao cha dharau.

Tena unachekwa kabisaaaaa,,,,,,ila huu si uamaduni wetu wadauuuuu
Kwa Tanzania hili la mwisho ndio lafaa zaidi. Kwani ukijiuzulu unajidhuru bure tu hakuna uwajibikaji hapa.

Mdau,kwa hotuba za shein na jk za jana zinaonesha dhahiri kuwa hilo swala walaaa halitazungumzwa,wao wamepongezana kwa ushirikiano na pia wamehimiza umoja wa muungano,wala hawajasema kuwa endapo tume itatoa ripoti na kama kuna uzembe nin kifanyike
Ndio maana nikatoa maoni niliyotoa ili kuvunja huo ukuta wa "hatuna utamaduni huo". Hatuna utamaduni kwa sababu vyeo kwetu si dhamna bali ni "mtaji kutokana na ajira chafu".

Ni mangapi hayakuwa utamaduni wetu na leo tumeyakumbatia? Au ni kusema tunaiga yale tu ya kukosa heshima kama mavazi, heshima kwa wazazi n.k?

Kwa mtu mwenye heshima na haya zake, kwa tukio kama hili anajiondoa hata kama hakuhusika moja kwa moja, anajiondoa kwa sababu hakubaliani na mfumo wa kulindana, anajiondoa ili kupisha uchunguzi huru. Kwa mtu mwenye utu na heshima zake anaona aibu kwa tendo analolifanya mwengine.

Waziri wa miundombinu wa zanzibar hamad masud mh.Hamad Masudi amesema yupo tayari kujiuzuru
Sosi:bbc

Ukimsikiliza kwa makini jinsi alivyokuwa akiongea utaona ni mnafiki tu. Kwa mtu makini hana haja ya kusubiri tume. Taarifa za awali tayari zinaonesha uzembe (vz idadi ya abiria vs uwezo wa meli, ukaguzi etc) uliotokea chini ya wizara yake. Hili peke yake linatosha kuanza kuchukua hatua. Kuwajibika sio lazima iwe yeye ndiye aliiruhusu meli ipakie kuzidi uwezo wake!

Viongozi wa Kiafrika ni matatizo sana .Maneno mengi sana lakini matendo hakuna .Unaweza kuwaona wako speed pale tu penye kupenyezwa rupia lakini kwenye haki na uwajibikaji lazima ibwabwaje .Aibu sana kiongozi mkubwa kama Shein kusimama na kusema kuzama kwa meli ni mipango ya Mungu utadhani Mungu ndiye aliye overload mizigo na watu kwenye meli .

• Thanks
Reactions: SMU
Mheshimiwa Waziri, Kama ungekuwa unafanya kazi yako kwa umakini, basi hata idara hiyo ya usafiri majini ingekuwa makini, na hayo yaliyotokea yasingetokea. Sasa ni kipi unachosubiri kidhibitishwe? Naomba utujuze hapa jamvini.

Kwa kuweka rekodi sawa, Mwinyi hakuwajibishwa, aliwajibika. Na barua ya kujiuzulu ilisifika kwa kiswahili fasaha alichotumia. Ni aghalabu sana viongozi wa Afrika kuwajibika kwa kujiuzulu, Mwinyi aliweka mfano Tanzania.
kumbe sometimes zipo kichwani mwako eeeh!

Viongozi wa Afrika wana matatizo kweli. Anajua kuwa tume haitamtaja direct kama mhusika, na pia raisi hataweza kumuambia ajiuzulu. Huu utamaduni wa kujiuzulu ni utashi wa mtu binafsi na si lazma tume ikutaje.

Back
Top Bottom