Nipo tayari kujiuzuru endapo itathibitika-waziri wa miundombinu

itabidi na waziri muhusika wa bara nae ajiuuzuru, maana meli imesajiliwa bara(ingawa haikupaswa ipate usajili kutokana na uchakavu wake), na imeanzia safari yake bara tayari ilikuwa imejaza kupita huwezo wake. jeshi la polisi nao inabidi wakuhuu waachie ngazi, maana taarifa walizipata mapema iweje waende saa 12 na siyo hiyo saa saba usiku. hii ajali ni pure uzembe hakuna kazi ya mungu wala nini, yani pure uzembe, wengi tuuu wanaotakiwa kujiuzuru hapo tena mara moja kabla hata ya hiyo taarifa ya tume, mtu inapaswa ujipime mwenyewe unahusikaje na kuachia ngazi.
 
  • Thanks
Reactions: SMU
Ili kuonyesha uwajibikaji, ilipaswa tayari awe ameshajiuzuru. kusubiri atajwe na tume itaondoa dhana nzima ya uwajibikaji.
 
Nilijua tayari ameshajiuzuru kumbe mpaka ikithibitika watu wamekufa kwa DNA aliyosema JK au anataka ithibitike nini?
 
Si vizuri kuwahukumu hawa tu kwani uzembe wa viongozi wetu wote ndio utamaduni wetu. List ya ajali za barabarani zilizotokea Tanzania tangu MV Bukoba ni ndefu sana lakini utaona kuwa zote zinajirudia kila kukicha. Tiba ya ugonjwa wetu siyo kunywa apsirini na kuendelea na shughuli za kila siku, bali tunahitaji operation na kulazwa wodini kwa muda wa siku kadhaa kabla hatujaanza shughuli zetu tena.

Mara kwa mara vyama vya upinzani ikiwemo CUF wamekuwa wakiwataka mawaziri kujiuzul yanapotokea majanga ya kizembe kama haya. Sasa kwa kuwa CUF ndio wameanza kuingia katika Serikali jumuia nzima ya wapinzani tunataka kuona vitendo katika madau haya ya muda mrefu labda itawafanya hata CCM kujifunza kitu kwa waziri huyu kujiuzulu.
 
Uondoke kwa heshima. Kama utabaki nitakuwa sioni tofauti kati ya viongozi wangu wa ccm na wapinzani kama cdm na cuf wote madaraka 1

Badilim jina sana naoana kiama ile Malaria Sugu imepona na unatumia akili badala ya Masaburi. Big Up!!
 
Ila sijui yule waziri anatoka CUF au CCM,maana hata CUF bara siwasikii wakizaungumzia kujiudhuru,,,,,na si kawaida yao,,,,hata akijiuzuru,kesho atakuwa BALOZI WA TANGANYIKA NCHINI UKRAIN
Mara kwa mara vyama vya upinzani ikiwemo CUF wamekuwa wakiwataka mawaziri kujiuzul yanapotokea majanga ya kizembe kama haya. Sasa kwa kuwa CUF ndio wameanza kuingia katika Serikali jumuia nzima ya wapinzani tunataka kuona vitendo katika madau haya ya muda mrefu labda itawafanya hata CCM kujifunza kitu kwa waziri huyu kujiuzulu.
<br />
<br />
 
Mbona bado yupo mpaka sasa? Imeshathibitika ni uzembe wa wizara anasubiri nini?
 
Nkidhani huu ndiyo wakati wa CUF kuonyesha tofauti kati yao na CCM. Huyo bwana anaonyesha ametafuta uongozi siyo kuwatumikia wananchi. Huyo ni mchumia tumbo!
 
Kuna kiongoz mchumia mgongo?????
Nkidhani huu ndiyo wakati wa CUF kuonyesha tofauti kati yao na CCM. Huyo bwana anaonyesha ametafuta uongozi siyo kuwatumikia wananchi. Huyo ni mchumia tumbo!
<br />
<br />
 
Kwa kuweka rekodi sawa, Mwinyi hakuwajibishwa, aliwajibika. Na barua ya kujiuzulu ilisifika kwa kiswahili fasaha alichotumia. Ni aghalabu sana viongozi wa Afrika kuwajibika kwa kujiuzulu, Mwinyi aliweka mfano Tanzania.

Sio Mfako kwa Tanzania tu nadhani kwa Afrika yote aliweka Mfano...

Lakini aliporudi Madarakani kwanini aliteleza na kuanzisha Azimio la Zanzibar? kuondoa JKT na Sasa Wanaliweka Tena?

Atatupa kiswahili fasaha kuhusu Jambo Hilo?
 
Kwa kuweka rekodi sawa, Mwinyi hakuwajibishwa, aliwajibika. Na barua ya kujiuzulu ilisifika kwa kiswahili fasaha alichotumia. Ni aghalabu sana viongozi wa Afrika kuwajibika kwa kujiuzulu, Mwinyi aliweka mfano Tanzania.

Bahati mbaya sana ni kwamba hakuna mtanzania mwingine yeyote aliyeweza kuiga mfano wa mzee ruksa, hata mtoto wake mwenyewe dr. Hussein mwinyi ameshindwa kujifunza kwa baba yake.

Labda atokee mwingine na aandike barua kwa kiingereza sanifu, huenda wakajifunza kitu naona kama vile hawa waswahili hawaelewi kiswahili.
 
Mwinyi alijiuzulu lakini baadaye alirudi kwa tiketi ya urais na hivyo kupoteza kabisa umaana wa kuwajibika kwake awali. Mimi sioni kama Afrika kuna kuwajibika na wala sioni sababu ya kumbebesha lawama huyo waziri. Isitoshe matatizo na ajali zetu zinatokana na umasikini wetu sasa watu watajiuzulu wangapi kila siku. Si tunateuwa mawaziri kila siku?
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom