Nini tunahitaji kwanza? - (tazama picha na amua)

Hapa umri sio kitu. Hekima tu. Kuanzisha kitu sio kitu kigumu. Kitu kigumu ni ku-maintain.

Ukiangalia posti za ndugu Mwanakijiji zote zipo kwenye uanzishaji. Katika kipindi cha miaka kumi ya uhuru serikali kwa kusaidiwa na hao hao wakoloni ilianzisha miradi mingi. Lakini hakuna Sustainability ya miradi hiyo.
Hivi unachosema kina ukweli? Miradi mingi ilianzishwa na Watanzania wenyewe kuliko na wakoloni! Nyerere aliposema tujitegemee alijua kuwa mojawapo ya mambo magumu ni kujifunza kuachana na kuwategemea wakoloni. Kwa kadiri tulivyopata wataalamu wetu wenyewe ndivyo vivyo hivyo wataalamu wa kigeni walivyozidi kupungua.

Tunaviangalia vitu kutoka katika pembe tofauti hapa. Mnaangalia vitu kwa sababu vilianzishwa. Mimi naangalia kuanzishwa na kuendelezwa.

Hapana, mimi kwa upande wangu wangu naangalia kuwa vitu vilianzishwa na vikaendelezwa ni hadi baadaye sana ndipo wengine wakavivunja. Si umesikia suala la shamba la mpunga la Mbarali? Kuna mifano mingi kweli. Sasa hawa wasipoendeleza leo tumlaumu Nyerere kwa kuanzisha na kuendeleza hadi alipofikia wakati anatoka?

Nyerere alifanya kiile ambacho aliweza kufanya, ni jukumu la waliompokea Nyerere kuendeleza "mema" na kuyaacha mabaya. Tatizo ni kuwa wao hata yale mema wameyatupa. Tatizo ni kuwa wewe unataka tumlaumu Nyerere kwa hawa kuivunja misingi ya taifa letu. Ni lini utaanza kuwawajibisha hawa waliochukua madaraka miaka 25 sasa tangu Nyerere aachie Urais? ama tusubiri miaka 50 baadaye ndiyo tuanze kufikiria labda tunawajibika na vitendo vyetu wenyewe?

Hivi wahisani wakikata misaada si tutarudi kwenye maisha ya pre-colonial :confused:

Hii ndiyo point yangu, wakisitisha misaada labda tutaanza kutumia ubongo wetu!
 
Hili ndilo swali ambalo wewe ungelifikiria, kama kwa miaka karibu 40 chini ya Mkoloni Tanzania ilikuwa hivi (x) lakini baada ya miaka kumi tu baada ya uhuru nchi ilikuwa vile..sasa inakuwaje mabadiliko makubwa yametokea ndani ya miaka kumi kuliko arobaini bila kuangalia nafasi, mchango na uwezo wa Nyerere?

this is haste generalization.. unaposema hakuna mwenye uwezo wa kubadili mazingira, husemi kweli, kwa sababu walikuwepo watu wenye uwezo wa kubadilisha mazingira na waliweza. Sijui kama unakumbuka masuala ya "kampeni ya Mtu ni afya", mambo ya "Nyumba Bora", n.k Sijui unajua ni kwa kiasi gani tuliweza kuelemisha watu wazima wetu na kuwapa elimu ambayo ilifungua mambo mengi kwao, mambo ya kilimo cha maksai, matumizi ya mbolea (samadi na ya kisasa), ujenzi wa visima vya kisasa n.k

Kuna mambo ambayo yamefanyika kuonesha watu wameweza kuyabadili mazingira yao. Wakati ule tuliweza kufanya mambo haya sisi wenyewe kwa kujituma, na kwa pamoja. Siku hizi bila NGO hakiendi kitu! So are we better today than we were 40 years ago?

Mwanakijiji:

Bado unazunguka mbuyu tu. Nimekuuliza hizo resources zilizofanya hayo mambo zilitoka wapi :confused:

Usiniambie kuwa kahawa, chai na pamba ni iliyofanya mabadiliko ya haraka haraka.

Kumbuka kuwa serikali nyingi za wahisani zilikuwa zinapeleka moja kwa moja pesa serikali kuu na hiyo ndio maana kubwa ya NGO kutoonekana kipindi cha miaka ya nyuma.

Lakini kutokana na wahisani wengi kugundua kuwa NGO ni cheap kuziendesha na wakati mwingine efficient kuliko serikali wamehamua kutumia NGOs.
 
Kutokana na ramli langu namwona Kikwete atachukua tena Urais..kumwondoa itakuwa kazi kubwa na mpya kabisa isipokuwa tunachoweza kufanya ni kutafuta mbinu inayozunguka Urais huo kutokana na katiba yetu...

You are giving up too easly and too quickly. Kama tutashindwa kumuondoa Kikwete licha ya kuboronga kiasi hiki, basi inabidi upinzani ufe. Kama tunataka kumuondoa JK inabidi kuamua ni nani awe mgombea wa uraisi kwa upinzani hivi sasa na kuanza kampeni hadi vijijini kuwaeleza jinsi JK alivyoshindwa nchi. Jk amejizatiti lakini sidhani kama wananchi wakieleweshwa alivyoburunda kama anaweza kushinda. Timu ya say Dr. Slaa + Prof. Lipumba kwenye uraisi +makamu, inaweza kushinda tatizo ni kipengele cha Mzanzibari kuwemo.

Njia pekee na rahisi zaidi ni sisi wapinzani kwa vyama tofauti iwe hata Wapinzani ndani ya CCM tuchukue Ubunge wa wilaya karibu zote, hivyo Kikwete hata kama atashinda itambidi achague baraza la mawaziri nje ya mtandao..

Kuchukua majimbo mengi zaidi, YES, it is doable and very necessary. Ila kwa Kikwete kuteua wapinzani ni day dreaming, unless wapinzani wakubali kula rushwa kama washikaji zake.

Pili, kuna dalili ya Kikwete kuweza kufanya mageuzi na pengine kusikia kilio cha wananchi isipokuwa amebanwa na wabunge wa CCM ambao kwa wingi wao miswada mingi na hoja nyingi zimepigwa chini bungeni...

With due respect Mkandara, Kikwete is part of the problem and therefore can not solve anything. Kama unaamini kuwa hakuingia ikulu kwa kutumia some of the EPA moneys, then expect him to take care of rushwa ambalo ndio tatizo namba moja Tanzania. He just have to go.
 
Zakumi,
Kumbuka kuwa serikali nyingi za wahisani zilikuwa zinapeleka moja kwa moja pesa serikali kuu na hiyo ndio maana kubwa ya NGO kutoonekana kipindi cha miaka ya nyuma.
Lakini kutokana na wahisani wengi kugundua kuwa NGO ni cheap kuziendesha na wakati mwingine efficient kuliko serikali wamehamua kutumia NGOs.
Mkuu samahani hapa kidogo..nashindwa kuelewa swala la Wahisani na NGOs... kwa sababu navyoelewa mimi budget yetu leo hii inategemea misaada (wahisani) kwa asilimia 40+ or minus, sasa hapa huwa kuna NGOs gani zinazohusika..Naomba somo kusema kweli nilikuwa sijui.
 
mkandara hapa umeniwahi tu.. na mimi nilikuwa na swali hilo hilo, kuwa ni lini wahisani waliacha kusupport bajeti yetu moja kwa moja? Halafu, akumbuke kuwa kuna wakati sisi tuligomea misaada hiyo hasa mikopo ya IMF na WB amnbayo ilikuwa ni ya kututia kitanzi..
 
MakaayaMawe,
Shukran lakini swala la kuwaweka Dr. Slaa na Lipumba kiti kimoja ni gumu kuliko hata kumsimamisha Mkandara Urais. Picha nzima tuitazame kwa uwezekano uliopo, kweli nakata tamaa haraka sana lakini ndivyo tulivyo kwani kama muungano wa vyama pinzani umeshindikana - nitegemee nini zaidi ya kutazama possibility nyinginezo.
Dr. Slaa anaweza kabisa kusimama na Kikwete kama wagombea binafsi lakini tukiweka CCM na Chadema nyuma ya majina yao Kikwete mshindi kwa sababu CCM wajuzi sana wa kuharibu jina la mtu ktk propaganda zao..
Kuchukua majimbo mengi zaidi, YES, it is doable and very necessary. Ila kwa Kikwete kuteua wapinzani ni day dreaming, unless wapinzani wakubali kula rushwa kama washikaji zake.
Kwani katiba inasema vipi kuhusu kuteuliwa kwa Mawaziri?.. Je, CCM wakishindwa majimbo yote bado Kikwete anaruhusiwa kuchagua wabunge walioshindwa kushika nafasi ya Waziri!
Naomba somo
With due respect Mkandara, Kikwete is part of the problem and therefore can not solve anything. Kama unaamini kuwa hakuingia ikulu kwa kutumia some of the EPA moneys, then expect him to take care of rushwa ambalo ndio tatizo namba moja Tanzania. He just have to go.
Naelewa hilo sana, He has to go....ndicho nilichokuwa nikiamini zamani kabla ya muungano wa upinzani kuvunjika..na kama utakumbuka nilikuwa mshabiki mkubwa wa muungano huo ili tupate mabadiliko ni LAZIMA kuchukua kiti cha Urais kutokana na mazingira ya tawala zetu za Kiafrika.. Mifano ya Kenya na Zimbabwe ni somo kubwa kwa siasa za Kiafrika..
Lakini baada ya kifo cha umoja huo nimefikiria labda Bunge ndio option ya pili na iliyobakia...
Hivi kweli bunge lote likikubaliana kuwasimamisha watuhumiwa wa EPA kizimbani, huyo Kikwete ataweza vipi kuzuia hilo Kikatiba iwapo hana support ya wabunge..
 
Well spoken! whose faults is this then? Nyerere aliyefanya lililobora kusomesha watu? au wale waliosomeshwa lakini they do not use their 'brains'

Au unasema Nyerere alipaswa kuwa na uwezo wa kujua/kutabiri kuwa atakaowasomesha hawataweza kubadili mazingira?

Au unasema kuwa asingesomesha kabisa, so taifa letu liwe la wajinga na tusiwe na watu hata wanaoweza kupost-comments kama wewe!

Au hujui kuwa wewe na we ni result ya Nyerere? unless kama umezaliwa na kukua nje ya TZ, wazazi wako hawajuguswa na matokeso ya Nyerere-in other words-utakuwa sio mtanzania!

He did his best parts, he did all for good reasons, though some went wrong........japo amekufa miaka 10 iliyopita still anaonekana amekuacha mbali sana.

wait.....ungekuwa wewe ndiyo Nyerere unapata urais wa kwanza wa TZ,ungefanya nini, ili hali ya leo iwe nzuri
?

Waberoya:

Nadhani ukizisoma sana posti zangu, unaona kuwa nime-avoid kumtaja Nyerere. Lakini kila nikijibiwa naona Nyerere
anajitokeza kitu ambacho kinanizungusha kichwa.

Hata serikali ikiwa inaongozwa na malaika, false starts zitakuwepo.Sasa kama false starts na makosa mnayaweka katika kundi moja sioni kama tutafika mbali.

Kulikuwa hakuna taifa linaloitwa Tanzania, Tanganyika au Zanzibar kama entity inayojitegemea yenye viongozi wenye uzoefu.

Ilikuwa ni kawaida ya waingereza kuwapa madaraka ya ndani wananchi kabla ya uhuru. Lengo la madaraka ya ndani ilikuwa kutoa uzoefu.

Ghana kabla ya kupata uhuru walipewa miaka sita ya madaraka ya ndani, lakini walipopewa uhuru na wao walikuwa na false starts zao.

Nchi za Afrika mashariki zilipewa madaraka ya ndani kwa kipindi cha chini miezi 18. Hivyo basi kulikuwa hakuna uzoefu wa kuongoza nchi na false starts zilikuwa ni nyingi katika mazingira hayo.

Kwa mtaji huo hata mimi ningekuwa rais wa kwanza ningeboronga.
 
Zakumi,

Mkuu samahani hapa kidogo..nashindwa kuelewa swala la Wahisani na NGOs... kwa sababu navyoelewa mimi budget yetu leo hii inategemea misaada (wahisani) kwa asilimia 40+ or minus, sasa hapa huwa kuna NGOs gani zinazohusika..Naomba somo kusema kweli nilikuwa sijui.

Kuna miradi ya maendeleo na matumizi ya serikali. Unaposema mashule yalijengwa, mabarabara yaliongezeka, vituo vya afya vilijengwa unazungumza miradi ya maendeleo. Tukija kwenye matumizi ya serikali ni kama vile kulipa mishahara ya wafanyakazi serikalini.
Katika miradi ya maendeleo ya jamii wahisani wengi wamejikita wenyewe kusimamia ndio maana ya ongezeko na NGOs. Kwenye matumizi ya serikali, ndio hiyo misaada bado iliyo kwenye bajeti. Hivyo wakikata 40%, mishahara itashindwa kulipwa.
 
Why do discussions like this end up gravitating towards Nyerere?

Because he's the "father of the nation" and naturally when one messes up questions regarding the father are always raised, whether the father is to blame for all of the child's misdeeds is something else...
 
Hmmm...we're something else coz I never hear anybody bring up George Washington for the vestiges of slavery which have dogged America for years and years...
 
Zakumi,
Mkuu hapa bado unajichanganya tu..hiyo misaada ya NGOs -iwe maendeleo ya jamii au mishahara haihusiani kabisa na serikali iwe kwa Maendeleo au Matumizi yake.. na wala sio somo tunalozungumzia hapa kuhusiana na wahisani. Ebu nambie kitu kimoja nini tofauti kati ya Wahisani na Wafadhili?..
Mathlan, Maleysia walipokata kuchukua misaada ya wahisani lakini bado NGOs zilikuwa zinaingia na kufanya kazi kama kawaida..hakuna mchumi aliyesema Maleysia bado wanachukua misaada.
Majuzi tu huko Gaza serikali ya Hamas waliteka malori ya misaada ya UN na limeibuka soo...hivi vitu havihusiani kabisa na sidhani ndicho Mwanakijiji alikuwa akizungumzia..
 
MakaayaMawe,
Shukran lakini swala la kuwaweka Dr. Slaa na Lipumba kiti kimoja ni gumu kuliko hata kumsimamisha Mkandara Urais. ........lakini tukiweka CCM na Chadema nyuma ya majina yao Kikwete mshindi kwa sababu CCM wajuzi sana wa kuharibu jina la mtu ktk propaganda zao..

Ilikuwa vigumu kuungana, lakini unapoona Mrema, Mbowe n.k., wanakimbilia kwenye ubunge, hapa inaonyesha dalili za makubaliano kuwezekana. Muhimu ni kuendelea na majadiliano kwani bila kuungana kwa angalau vyama vikuu, hata ubungeni tutashindwa. Kumbuka Vunjo CCM walishinda kwa 44%, wakati jumla ya Chadema (11.9%), NCCR (11.5%) na TLP (31.2%) tu ilikuwa 55%, ambao ungekuwa ushindi mkubwa sana, lakini tukashindwa. JK hawezi kushindwa kirahisi, lazima tuwe creative, persistent na ikibidi stubborn kum-confront.

Kwani katiba inasema vipi kuhusu kuteuliwa kwa Mawaziri?.. Je, CCM wakishindwa majimbo yote bado Kikwete anaruhusiwa kuchagua wabunge walioshindwa kushika nafasi ya Waziri!
Naomba somo

Sidhani tunaweza shinda majimbo yote au kama mawaziri watasaidia kuibadili serikali ya CCM. Bali kuongeza upinzani bungeni ni muhimu lakini pia tuangalie uwezekano wa kumuondoa JK. Cha kufanya ni kuanza mapema kuteua wagombea wazuri kwenye majimbo na kuanza kuwanadi mapema, badala ya kusubiri 2010 maana wa CCM tayari wanajulikana.

Naelewa hilo sana, He has to go..... Mifano ya Kenya na Zimbabwe ni somo kubwa kwa siasa za Kiafrika...Lakini baada ya kifo cha umoja huo nimefikiria labda Bunge ndio option ya pili na iliyobakia...

Nafikiri umoja ulizimia tu, lakini bado kuna uwezekano wa kuu-resuscitate kutokana na ukweli kuwa ndio tegemeo leo tu kwa upinzani, na wote tunaelewa hilo hivi sasa.

Kitu kimoja tu ninachoona hatufanyi ni kutokuwa active zaidi katika kumshinikiza JK ili aweze kuonekana kuwa ndiye kikwazo. Badala yake tumekuwa tukiwalaumu tu mafisadi na kufanya kama vile JK is clean, au anafanya kazi bora.

Ushauri wangu ni kuwa tu-list mambo ambayo CCM wameyafanya kuharibu nchi, chini ya JK, then tuanzishe maandamano na hata migomo nchi nzima ili kumshinikiza JK kuchukua hatua na kwa kufanya hivyo wananchi wataweza kufahamu ubora wa upinzani na ubaya wa CCM. Katika hili, wale tunaoteua kugombea majimbo mbali mbali itabidi ndio waongoze maandamano huko majimboni kwao.
 
Zakumi,
Mkuu hapa bado unajichanganya tu..hiyo misaada ya NGOs -iwe maendeleo ya jamii au mishahara haihusiani kabisa na serikali iwe kwa Maendeleo au Matumizi yake.. na wala sio somo tunalozungumzia hapa kuhusiana na wahisani. Ebu nambie kitu kimoja nini tofauti kati ya Wahisani na Wafadhili?..
Mathlan, Maleysia walipokata kuchukua misaada ya wahisani lakini bado NGOs zilikuwa zinaingia na kufanya kazi kama kawaida..hakuna mchumi aliyesema Maleysia bado wanachukua misaada.
Majuzi tu huko Gaza serikali ya Hamas waliteka malori ya misaada ya UN na limeibuka soo...hivi vitu havihusiani kabisa na sidhani ndicho Mwanakijiji alikuwa akizungumzia..

Mkandara:

Vitu vingi viko Self Explanatory. Na sidhani kama utanielewa kwa sababu emotions zako ni nyingi.
 
Hmmm...we're something else coz I never hear anybody bring up George Washington for the vestiges of slavery which have dogged America for years and years...

Because the slavery was never the problem to America,Slavery build America America,slavery was the the big businesss,Slavery benefit America at the time and now no more slavery.
THINK TWICE

SAHIBA.
 
Because the slavery was never the problem to America,Slavery build America America,slavery was the the big businesss,Slavery benefit America at the time and now no more slavery.
THINK TWICE

SAHIBA.

Say what!?!?
 
Back
Top Bottom