Nini kazi ya hizo Sayari zilizobaki ukiondoa Dunia?

myself scenario

JF-Expert Member
Jul 5, 2015
347
213
Sidhani Kama Mungu Aliamua Kutuweka Katika Sayari Ya Dunia Halafu Sayari Nyingine Zibaki Kama Mapambo.

Ninachoami Kwenye Hizo Sayari Nyingine Kuna Viumbe Wanaishi Na Either Wana Mungu Wao Au Ni Huyuhuyu Mungu Wa Dunia Ndiye Wanaemuabudu.. Pia Kuna Uwezekano Na Wao Pia Wana sheria Zao Za Kumtii Mungu Na Kuna Wasomi Pia Wenye Akili Na Maarifa Kutushinda Sie Wanadamu..

Nawaza Tu, Kuna Sayari Kubwa Kushinda Dunia,labda Humo Kuna Viumbe Wengi Zaidi, Ila Hatuwezi Kuwaona Kutokana Na Mpango Wa Mungu #freeman
 
Sayari moja tu katika mfumo wa jua ndio ina viumbe hai nyingine zote hazina kutokana na environmental conditions zao!

Tatizo kubwa la nyie wanasayansi mnakata kilicho duniani ndio kiwe sawa kabisa na kilicho kwenye sayari nyingine, nadhani jibu lako lingekuwa inawezekana kukawa na viumbe wengine ambao watakuwa tofauti na sisi kwa sababu ya utofauti wa kimazingira, sio kila kiumbe lazima viwe kama vya hapa duniani, inawezekana kukawa na watu ambao wako tofauti sana na sisi, labda hawaitaji sana oxygen, hawaitaji maji, hawaitaji chakula, nk wapo kama marobot tu

so viumbe vinaweza vikawepo huko
 
Basi kama haviko sawa na sisi hivyo sio viumbe tena! Mleta mada ameulizia kama kuna viumbe wengine nami nimemjibu kutokana na alivyouliza....
 
Kwani neno kiumbe maana yake nini? Mungu ameumba viumbe tunavyoweza kuviona na tusivyoweza kuviona, tena hata tunavyoweza kuviona anaruhusu mwenyewe kuviona/kuvumbua/gundua kutokana na wakati. Mfano Mwanzo ilijulikana dunia ni kama meza, kumbe ni mviringo. Kuna watu walitangaza laana kwa wale walokwenda kwenye mwezi kwa kuwa wanaenda kumchokoza kwenye makao yake, walifikiri mbinguni ni juu ya utosi wao, leo ni safari za kawaida. Na vyombo vya masafa vipo zaidi ya Pluto sayari iliyozaniwa ni ya mwisho kumbe zipo nyingine kibao kwa jina la Gallaxy, kuna wakati Joshua 'alisimamisha jua', kumbe dunia ndo iliacha kuzunguka, jua halitembei wala kuzunguka!

Mungu hashindwi kitu, Funguka ufahamu!kuna viumbe kama nyungunyungu wanaishi ardhini,hewa wanapate, lkn wanaishi,kuna bacteria,virus etc, mfumo wao wa kuishi ni tofauti kabisa na sisi, funza chooni, seal chini ya maji ambayo juu yameganda barafu huko Canada, Alaska nk. Wameanza kuonekana UFO, Alliens nk. Kuna Wanefil na Waanaki nk.

Je majini, Shetani, Maroho, Mizimu, Voudoo, Angles etc. Nenda kwa ma Yoga na Budhaa(google) huko ndo utachanganyikiwa! Naamini, vile Mungu aliziumba hizo sayari pia kunaweza kuwa kuna viumbe vya namna yake, ni jambo ka wakati tu kuvigundua tena pale atakapotufunulia Yeye.
 
Acha kukariri, kwa hiyo kikiwa sio sawa na wewe ndio sio kiumbe?

Mkuu Kituko naomba unielewe ninaposema sisi kama mleta mada alivyolitumia hilo neno najumuisha viumbe vyote vyenye uhai vilivyoko duniani hapa nahusisha Flora and Fauna.

Sisi soe tunafahamu sifa ya viumbe hai ni kwanba ni lazima azaliane, apumue, amove, akue n.k vipi kama hiko kiumbe hakina sifa hizo je kitakuwa ni kiumbe hai tena?

Kwanini sio viumbe?

Mkuu niliposema ''sisi'' nimejumuisha viumbe vyote vilivyo hai duniani ikiwemo wanyama na mimea
Ikiwa havitakuwa na sifa kama za viumbe hai basi sio viumbe hivyo hapo tutakuwa tunazungumzia kitu kingine tena...

Kwa mfano gesi ya Nitrogen Duniani ipo na Mwezini ipo... Vipi kama Mwezini kungekuwa hakuna gesi bali kuna vitu vingine tofauti na gesi ungelisema mwezini kuna gesi??
 
Last edited by a moderator:
nachokiamin mimi huko nako kuna viumbe ila hatuwez kuwaona na wao wanaendana na mazingira ya huko,sitak kuamin kama pluto,jupiter n.k ni mapambo tu
 
Sayari moja tu katika mfumo wa jua ndio ina viumbe hai nyingine zote hazina kutokana na environmental conditions zao!

Kuna maelfu ya sayari zimegunduliwa zikizunguka nyota (jua ni nyota).

Na makaditio ni kwamba kuna mabilioni ya sayari katika ulimwengu, ambazo kati ya hizo, mamilioni zina uwezekano wa kuwa na conditions kama za dunia.
 
And why don't we go there!!? Or even try!?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom