WANAJF;Toka jana mara tu baada ya Hotuba wa Rais nimekuwa nikijiuliza maswali mengi sana kuhusu KUSUDIO LA MAONGEZI YA RAIS na wale Wazee wa CCM wa DSM. Ni hakika sijapata jibu la kusudio wa mkutano ule. Hivi Rais wetu alikuwa serious kuongea na wale wazee ambao wengi wao wanashinda kwenye Kahawa kuongea mambo ya uchumi na mambo ya kisiasa ikiwemo na mchakato wa suala la Katiba? Hivi wale Wazee waliokuwa pale kupiga vigelele na makofi hata ukiwauliza chochote walichoambiwa wataweza kukuambia? Mimi nashawishika kuamini kwamba Mh. Rais hakika mambo yameshamshinda hivyo amebaki akitafuta kundi fulani katika jamii ambalo kwa hakika haiwezi kuhoji chochote na badala yake wao wanafurahi kuwa na maongezi na Rais. Sina hakika kama kweli posho haikutolewa kwa wale Wazee kwa KAZI NZURI WALIYOMFANYIA RAIS, kwani Rais wetu kwasasa anatafuta Cheap Popularity. Kwani naona Rais aliishia kutoa vitisho vingi sana kwa wale wanaompinga.Viongozi wa Upinzani na wanaharakati; CHONDE CHONDE MSIRUDI NYUMA NI HAKIKA TUMECHOKA NA SASA TUNAHITAJI KATIBA MPYA SI yale aliyokuwa akieleza Rais jana. Hatuhitaji kufanya kazi kwa mazoea na badala yake tunahitaji UBUNIFU katika mambo ya msingi kama KATIBA. Hatuwezi kukubaliana na Rais kwamba hata Viongozi waliopita walikuwa wakifanya hivyohivyo. Ndiyo maana nimekuwa nikisisitiza Rais wetu uwezo wake umefikia mwisho, kwani hawezi kuwa na UBUNIFU TENA. Haya mambo ya Kukopi ndiyo maana hata Ufisadi ameukopi? Narudia tena kwa UCHUNGU; HATUNA WKT MWINGINE WA KUDAI HAKI ZETU HASA KATIBA MPYA ISPOKUWA SASA; Na wananchi tukiamua hakuna wa kutuzuia. Kikwete hawezi kuwatisha wananchi wkt hataki kufanya kama wananchi wanavyotaka.Nawasilisha Wadau!