Nini ilikuwa kusudio la rais kukutana na wazee wa CCM Dar?

JATELO1

JF-Expert Member
Oct 31, 2011
1,230
301
WANAJF;Toka jana mara tu baada ya Hotuba wa Rais nimekuwa nikijiuliza maswali mengi sana kuhusu KUSUDIO LA MAONGEZI YA RAIS na wale Wazee wa CCM wa DSM. Ni hakika sijapata jibu la kusudio wa mkutano ule. Hivi Rais wetu alikuwa serious kuongea na wale wazee ambao wengi wao wanashinda kwenye Kahawa kuongea mambo ya uchumi na mambo ya kisiasa ikiwemo na mchakato wa suala la Katiba? Hivi wale Wazee waliokuwa pale kupiga vigelele na makofi hata ukiwauliza chochote walichoambiwa wataweza kukuambia? Mimi nashawishika kuamini kwamba Mh. Rais hakika mambo yameshamshinda hivyo amebaki akitafuta kundi fulani katika jamii ambalo kwa hakika haiwezi kuhoji chochote na badala yake wao wanafurahi kuwa na maongezi na Rais. Sina hakika kama kweli posho haikutolewa kwa wale Wazee kwa KAZI NZURI WALIYOMFANYIA RAIS, kwani Rais wetu kwasasa anatafuta Cheap Popularity. Kwani naona Rais aliishia kutoa vitisho vingi sana kwa wale wanaompinga.Viongozi wa Upinzani na wanaharakati; CHONDE CHONDE MSIRUDI NYUMA NI HAKIKA TUMECHOKA NA SASA TUNAHITAJI KATIBA MPYA SI yale aliyokuwa akieleza Rais jana. Hatuhitaji kufanya kazi kwa mazoea na badala yake tunahitaji UBUNIFU katika mambo ya msingi kama KATIBA. Hatuwezi kukubaliana na Rais kwamba hata Viongozi waliopita walikuwa wakifanya hivyohivyo. Ndiyo maana nimekuwa nikisisitiza Rais wetu uwezo wake umefikia mwisho, kwani hawezi kuwa na UBUNIFU TENA. Haya mambo ya Kukopi ndiyo maana hata Ufisadi ameukopi? Narudia tena kwa UCHUNGU; HATUNA WKT MWINGINE WA KUDAI HAKI ZETU HASA KATIBA MPYA ISPOKUWA SASA; Na wananchi tukiamua hakuna wa kutuzuia. Kikwete hawezi kuwatisha wananchi wkt hataki kufanya kama wananchi wanavyotaka.Nawasilisha Wadau!
 
Tena kuna wengine ni wastaafu wa afrika mashariki washasahau walivyopigwa mabomu kazi kukenuka tu...
 
Nia yake ni kuaminisha umma kuwa wana nia nzuri ya kuleta katiba mpya ila kuna watu wanataka kuvuruga huo mpango!

Natumai kuwa watu wenye akili zao hawakudanganyika.
 
Hivi mpaka sasa wapinzani hawajatoa hotuba yao kujibu/kufafanua ile ya mh JK? Maana at least ina upotoshaji flani. Kuhusu kuchagua hadhira yake cjui kwa nini isiwe wasomi wa vyuo na badala yake akachagua "wazee" wa ccm ambao anawaita wa DSM.
 
Nafikiri kwa chadema wanaweza kujibu hotuba hiyo baada ya mkutano wa kamati kuu.tusubiri tuone jamani
 
So pathetic! Decisions are on your hands. He is a person who doesnt learn. The same wazee cheered him when he was adressing on the issue of TUCTA last year before election. Do you know what happened? He got a difficult time in convincing civil servants in his campagn for his second term in office, and actually people did not vote for him as he was expecting.
This time we will see how they will convince the people to pass the new Katiba.
 
Nimependa system ya mheshimiwa kutafuta kundi la kuongea nalo ili kufikisha ujumbe kwa jamii ya watanzania Ila napenda kumshauli kitu kimoja ili awe na uhakika na kitu alichokiongea kama kinamvuto na ni kitu cha maana kiasi gani Anapo chagua kundi napendekeza aidha aongee na wanafunzi wa vyuo vikuu,wanaharakati,wafanyakazi au vijana bila kujali ni chama gani tats my advice anaweza kupigiwa makofi na vigelegele visivyo na msingi.
 
huyo ni mfamaji anayetapatapa, anajaribu kujionyesha yakwamba yeye ni mtu mzuri na ana nia ya kuleta mabadiliko ya kweli ilhali hajui matokeo ya matendo yake.
Jamii haioni jipya katika njia zake za kipropaganda za ushabiki na kiswahili cha mipasho.
 
Anaogopa yaliyotokea huko Arabuni; Amewaambia Wazee wa Dar yeye sio Dickteta anawapa watu Uhuru kupita kiasi

Yeye ni Mwema haswa...
 
Kuudanganya umma wa Watanzania.

Alichagua aina ya watu ambao ni rahisi kudanganyika aongee nao na wale wa kukodiwa ili washangilie ili UMMA uamini anachokisema. HATUDANGANYIKI
Mbona asiongee na Tanganyika Law Society? UDASA, etc?
 
Lengo kubwa lilikuwa ni ku pre-empty findings za kamati teule ya bunge kuhusu Jairo.
Mind you huo mkutano na wazee wa DSM ulikuwa Ad-hoc (uliitiswa ghafra). Hiyo ni baada
kua kamepata taarifa kuwa kamati ya bunge imeikaanga Ikulu na vipenzi vyake Luhanjo na Jairo.

Common sense inatuambia kwamba kama hiyo hotuba angaliitoa baada ya findings za kamati
teule ya bunge, CDM wangekuwa vindicated kuhusu hoja ya Rais kuteua, tume, kutoa hadidu
za rejao, maoni kuwakilishwa kwake kwanza kabla ya kutangazwa. Kwani tume teule ya Bunge
imetuonesha pasipo na shaka wateule wa Rais wanawajibika kwa Rais, sio kwa masilahi ya wananchi,
a case study ni hiyo CAG Utaoh alivyojaribu kuficha ukweli ili kumlinda Jairo na Ikulu.

Rais kuteua wajumbe wa tume ya katiba na maoni kuwakilishwa kwake kwanza ni KOSA kubwa ambalo
sisi watanzania wa kizazi hiki tutalijutia maisha yetu yote, hata CDM wakiingia madarakani. Na hakuna
fursa nyingine ya kutengeneza tena katiba mpya in 50 years to come.
 
huwezi kutenga wazee ktk mambo muhimu ya taifa, kwani katika kila chama, na asasi zote kuna wazee

mimi siamini kuwa wazee peke yao ndio wanabusara na kingine taifa hili siyo la wazee pekeyao jamani wapo vijana ambao ndio mnawaita nguvu kazi ya taifa.inashangaza sana kuona haohao vijana katika mambo ya msingi wanawekwa pembeni.huyo jk anatakiwa aweanawaita watu wote kuongea nao tuone kama atashangiliwa.
 
"Leo nataka kuzungumzia hali ya uchumi na mchakato wa kupata Katiba Mpya. "

Kikwete 17-11-2011
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom