Nini hupelekea Wasomi wa Tanzania kukimbilia siasa?

Ndugu watanzania, siasa ni chanzo au cha kufikiri kutafuta suluhishi au kupanga miundo mbinu ya urekebishwaji staili za maisha katika nchi fulani.

Katika siasa kosa likifanyika kinachotokea ni migogoro inayochukua muda kuisha.

Katika nchi ya Tanzania, kwa ukaribu inajionesha kwamba siasa sasa inaingia kwenye elimu. Kitendo cha kupangwa alama na madaraja ya ufaulu na wadau mbalimbali wa siasa ni dalili tosha za vurugu ndani ya wizara ya elimu.

Kawaida anayehusika kupanga au kufanya mabadiliko ndani ya wizara ni wataalamu wa wizara husika.

Watanzania tunashangaa, juzi tu division five, leo kufutwa. Hiki ni kizungu mkuti kwa wananchi.

Serikali inapaswa sasa ijipange na kuweka miundo yake vizuri na kuwaachia kazi wahusika. Mimi siponi kosa kwa waziri husika, bali anayumbishwa na viongozi wengine wa juu.
 
Back
Top Bottom