Kalunguine
JF-Expert Member
- Jul 27, 2010
- 2,543
- 134
Moja ya sababu inayotufanya tuende shule ni kupata pesa,so kwakuwa taaluma hazina pesa ya kutosha ndo maana wasomi wengi wanakimbilia bungeni ndo kwenye pesa.
Argument zako ni very flimsy. Umeandika thread hii bila kufanya utafiti wa kutosha. I can't do it for you for sure.Please go back to the drawing board.
Hint:
Wasomi wa kweli hawako kwenye siasa, kwasababu hawawezi siasa. Wao ni watu wa facts. Walioko kwenye siasa huku wakidai ni wasomi ni matapeli wa elimu, sio wasomi.
The Best Politiciana duniani ni wale waliokuwa na elimu ya chini ya chuo kikuu,watu kama Abraham Lincoln,Winston Chuchill na hata madikteta wakubwa kama Hitrel na Mussolin walikuwa na elimu ndogo sawa na innovators na kama Bill Gates na Marehemu Mac wote hao ni College dropout.Hivyo kitendo cha Maprofesa wetu kuingia kwenye siasa hakina tofauti na na Profesa Binaisa kuwa Rais Uganda.Hata wewe sikubaliani na wewe. Nitajie nchi moja tu duniani ambayo wanasiasa wake ni watu ambao hawajaenda shule! In fact ni Tanzania tu ambako idadi kubwa ya wanasiasa ni mbumbumbu wanaojua kusoma na kuandika tu: madiwani, wabunge n.k. Tunaendeshwa na semi-illiterates.
Cheki Spika wetu, ana elimu na uelewa stahili wa kuwa Spika? Just imagine akikutana na akina Lord Carrington kwenye vikao vya Maspika wa Commonwealth, Spika Makinda atajenga hoja gani?
Unakusudia mwalimu Nyerere au Mzee Ali Hassan Mwinyi?
Prof. Baregu au Prof. Sarungi?
Dr. Mwakyembe? Prof. Mwandosya?
Prof. Kapuya? Prof. Mu..ongo? Dr. Kawambwa? Dr. Lamwai? Dr. Mirigo?
Sasa tujadili nini? Hivi mtu hana haki ya kubadili kazi? Unataka wafe katika kula na kuvuta hewa yenye vumbi la chaki?
Unawaonea hao graduate tu.. hao madaktari na maprofesa vipi?
Nani afanye kazi ya siasa?
Umewataja wengi sana na ninakubaliana na wewe , lakini hukutaja sababu hasa za wao kuingia kwenye siasa ! Kwamba Profesa kweli anaingia kwenye siasa kwa ajili ya nini hasa ? Hujasema sababu .
Umewataja wengi sana na ninakubaliana na wewe , lakini hukutaja sababu hasa za wao kuingia kwenye siasa ! Kwamba Profesa kweli anaingia kwenye siasa kwa ajili ya nini hasa ? Hujasema sababu .
Taifa letu liko kwenye kipindi kizito sana kuvuka kwenye nyanja ya siasa na uchumi.Lakini tumefika hapa kivipi?Jibu langu kwa kujiuliza huko swali hilo na kujifunza kupitia kuona na kusoma tatizo la msingi na kubwa walilonalo watanzania ni la wasomi wengi wa Taifa hili kuwa ni majisifu, ufithuli, kujigamba, wenye kujitwalia bila haki ,jipachika hasa bila haki, jitwaza,jipachika utukufu wa Taifa kwa mgongo wa siasa kufaidi matunda ya uchumi.[Allogance and Arrogate]
Someone who is arrogant behaves in a proud, unpleasant way towards other people because they believe that they are more important than others.
If someone arrogates to themselves something such as a responsibility or privilege, they claim or take it even though they have no right to do so.
Leo hii Mtanzania aliyesomeshwa kwa mamilioni yapesa kwenye taaluma husika wamekimbilia kwenye siasa kwa kujua watakaa kwenye maamuzi na kuwa na kofia ya kujitwalia keki ya Taifa kimya kimya.Ni kwa wao kuingia kwenye kofia ya maamuzi leo Taifa halina watu wa kulishape [Think Tank],Wataalamu wa kilimo,maengineer,maprofesa, madaktari wa vyeo na madaktari wa Taaluma,walimuna wanasheria wote wamelundikana Bungeni na hatimae kuwa wana itikadi baada ya kuwa wanawataifa.
Kwa wenzetu taaluma pia umpelekea mtu kuwa ni aina gani ya mwanasiasa katika ulingo wa siasa,wasomi wa masomo ya political economy,mausiano ya kimataifa, wanasheria,watu wa masoko na wachumi ndio ambao kwa namna fulani wamejikuta kuwa wanasiasa.Leo hii kwa Tanzania sivyo.
Tumezalisha lundo la wasomi kila mwaka hawakai ofsini kuwa engineers wa kujenga Nchi kwa Taaluma zao bali wanatayarisha michakato ya kugombea ubunge ili atimae achaguliwe kuwa waziri hatimae kupata upofu wa si hasa.
Tuangalie vyanzo vya matatizo yetu,ebu pitieni CV za wabunge wa Taifa letu kila mmoja wekeni hapa,pimeni wahusika wangetumika sehemu husika pengine leo tusingekuwa na wanataaluma kwenye foleni queue ya kukusanya pesa ya umma kupitia miradi ya serikali ili kuwania ubunge na presidential appointment huku Taifa likiwa limesimama kwa kukosa watu wa kuengineer mambo ya kusogeza Taifa mbele kwa kuanda mikakati.
Je na wewe ni Mwanataaluma msomi?